Habari za Punde

MKUTANO WA CHANGAMOTO YA KUONDOA ANALOGI KWENDA KATIKA TEKNOLOJIA YA DIGITALI ZANZIBAR.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Abdillah Hassan Jihad, akifunguwa Mkutano wa Changamoto ya kuondoa Teknolojia ya Analogi kwenda katika Teknolojia ya Digitali ifikamo mwakani,mkutano ulioandaliwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania(TRCA) kwa kushirikiana na Tume ya Utangazaji Zanzibar (ZBC) kulia na Naibu Mkurugenzi wa TRCA Fred Ntobi na Mrajisi wa ZBC Abdalla Mitawi.Mkutano huo umefanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Ocean View Kilimani Zanzibar.
Washiriki wa Mkutano wa Changamoto ya kuingia katika Teknolojia ya Digitali wakimsikiliza Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michecho Zanzibar, Abdillah Hassan Jihad. 
 Mrajisi wa Tume ya Utangazaji Zanzibar Abdalla Hassan Mitawi, akiwasilisha mada ya Changamoto ya kuhakikisha ifikapo mwaka 2012, teknolojia ya Digitali imechukuwa nafasi yake.baada ya kuondoa teknolojia ya Analogi.
Walipa Kodi Zanzibar wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha, Uchumi Mipango ya Maendeleo Zanzibar Omar Yussuf Mzee, akiwahutubia katika sherehe za siku ya Mlipa Kodi, iliofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Ocean View Kilimani Zanzibar.
Naibu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TRCA Fred Ntobi, akielezea jinsi ya changamoto ya kuhama kutoka Teknolojia ya Analogi na kuhamia katika Digitali, wakati wa Mkutano uliowashirikisha Wafanyakazi wa TRCA na ZBC na Wamiliki wa Vituo vya TV na Redio Zanzibar.

Picha na Ali Othman

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.