Habari za Punde

WAANDISHI, WAMILIKI WA VYOMBO VYA HABARI PEMBA WAOMBA USHIRIKIANO NA IDARA YA HABARI MAELEZO

Marzouk Khamis Maelezo Pemba.

Waandishi wa Habari na Wamiliki wa Vyombo vya Habari Kisiwani Pemba wameoimba Idara ya Habari Maelezo kuzidi kushirikiana nao katika utekelezaji wa kazi zao za kila siku

Hayo wameyaeleza leo wakati wakutathmini Utendaji wa kazi wa idara hiyo kwa kipindi cha Miezi kumi iliopita kisiwani Pemba katika Ukumbi wa Kiwanda cha Makonyo Wawi Chake Chake.


Wamesema kuwa kazi iliofanywa na Idara hiyo kwa kipindi hicho ni nzuri kwani imeweza kuwaunganisha Waandishi wa vyombo mbali mbali vya Habari pamoja na Wamiliki wa vyombo Binafsi vya Habari katika kuwapasha Wananchi juu ya matokeo mbali mbali yakiwamo Uhamasishaji wa zao la Karafuu kisiwani Pemba.

Wamesema kuwa ujasiri ulioneshwa na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Zanzibar ni mkubwa na wakupigiwa mfano kwa kuwataka Waandishi wa Habari na Wamiliki wavyombo hivyo binafsi kumtathmini utendaji wake sio jambo rahisi kwani hakuna kiongozi wa Vyombo vyengine vya Habari vya Serikali Zanzibar waliofanya hivyo au kujaribu kufanya hivyo.

Mkurugenzi huyo amewataka Waandishi wa habari kufuata sheria na tataratibu za nchi katika kuandika habari na pia kuwa na Vitambulisho VYA kuandika habari kupitia Idara ya Habari Maelezo Zanzibar kwani kufanya kinyume chake ni kwenda kinyume cha sheria jambo ambalo sio zuri,

Aidha aliwataka Waandishi wa Habari kuendelea kujielimisha ili waweze kutekeleza kazi zao, hiyo ambayo ni muhimu kwa taifa na jamii kwa ujumla.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.