Na Haji Nassor, Pemba
ZFA wilaya ya Mkoani imeendelea na kuwaadabisha wachezaji watukutu baada ya kuwatia kifungoni wachezaji watatu wa timu ya Young Eleven ya Mkanyageni kwa kumtwanga makonde muamuzi siku ya mchezo wa ligi daraja la pili.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, Mwyneyekiti wa ZFA Mkoani, Seif Mohamed Seif, alisema, siku ya mchezo kati ya timu hiyo na Black Wizard, wachezaji hao ambao hakuwataja majina walimtwanga muamuzi, Faki Khatib na kumsababishia maumivu makali.
Alisema, kufuatia tendo hilo ndiyo ZFA kwa kutumia sheria na kanuni za soka ikwaadhibu kwa kuwafungia msimu mzima kutocheza soka.
Seif, alieleza, pamoja na adhabu hiyo kwa wachezaji na timu husika imetakiwa kulipa shilingi laki kabla ya Disemba 3 mwaka huu ambapo wametakiwa kulipa nusu na salio lilipwe si zaidi ya Januari 7 mwakani na wakishindwa adhabu nyengine itafuata.
Aidha Mwenyekiti huyo alisema, mchezaji mwengine aliefungiwa michezo mitatu na kutakiwa kulipa faini ya shilingi 50,000 ni Amour Zahoro Omar wa timu ya Shidi Warriors ya daraja la pili, baada ya kutolewa nje kwa kadi neyekundu na kisha kuvua viatu na kumtishia kumpiga mwamuzi.
No comments:
Post a Comment