Na Bakari Mussa, Pemba
MJUMBE wa kamati kuu ya CCM na waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Prof. Makame Mnyaa Mbarawa amesema kuwa chama hicho kimedhamiria kutekeleza Ilani yake ya uchaguzi kivitendo.
Alisema kutekelezwa kwa ilani hiyo kutawathibitishia wananchi kuwa CCM iliahidi mambo ambayo yanatekelezeka ambayo yataleta manufaa kwa wananchi wote.
Prof. Mbarawa alisema chama cha Mapinduzi, hakito wabagua wananchi kwa mujibu wa itikadi zao za kisiasa kwa vile wananchi wanachohitaji ni maendeleo na sio maneno ya hadaa.
Mjumbe huyo, alieleza hayo huko Chokocho, wakati alipokuwa akizungumza na wanaCCM na wananchi wengine katika mkutano wa hadhara wa kutathimini maendeleo yaliopatikana katika jimbo hilo.
Alifahamisha kuwa CCM, tokea kushinda katika uchaguzi wa Mwaka 2010, imefanya mambo mengi katika jimbo la Mkanyageni Pemba, katika kuwaletea maendeleo wananchi wa jimbo hilo bila ya kujali itikadi zao
za kisiasa.
Alisema maendeleo hayo ambayo yameletwa katika jimbo hilo ni miongoni mwa utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya iliyonadiwa kwa wananchi hao katika uchaguzi mkuu uliopita kwani hata kama CCM, haikupata jimbo lakini imeshinda na inaongoza serilali.
“Viongozi mliopewa kura na wananchi waonyesheni kile mlichowaahidi wakati wa kuomba kura na sio kuwadanganya kwa maneno matupu maana, wameshachokana kwa sasa wanahitaji kuona maendeleo”, alisema Prof.
Mbarawa.
Alieleza viongozi wa CCM, wako tayari kushirikiana na wananchi katika suala la maendeleo wakati wowote kwani inaelewa maendeleo hayana Chama na ndio maana kuma miradi kadhaa ilioanzishwa na CCM, ndani ya Jimbo hilo kuwashirikisha wananchi ili waone miradi hiyo inwagusa.
Mnyaa alifahamisha kuwa kwa kipindi cha mwaka mmoja tokea CCM, iingie madarakani ndani ya awamu hii ya saba, miradi mbali mbali imeanzisha ndani ya Jimbo hilo la Mkanyageni yenye thamani ya zaidi ya shilingi
70 milioni ikiwemo ya elimu, afya , madrassa za kur-ani.
Katika mkutano huo Mjumbe huyo wa Kamati kuu ya CCM, alikabidhi bati kwa waalimu wa Madrasa tatu, skuli ya msingi ya Shidi sambamba na kukabidhi kadi CCM kwa wanachama waliovihama vyama vya upinzani wapatao 50.
No comments:
Post a Comment