Habari za Punde

Tendwa Aishauri CUF kutii Amri ya Mahakama

Na Kunze Mswanyama

MSAJILI wa vyama vya siasa nchini, John Tendwa, ameungana na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jaji Frederick Werema kwa kusema kuwa,chama cha wananchi (CUF),kimevunja katiba kwa kuidharau mahakama iliyotoa hati ya kutoendeshwa kwa mkutano uliohitimishwa kwa kumtimua Mbunge wa Wawi, Rashid Hamad Mohamed.

Pia,Tendwa alibainisha kuwa yeye hajkapokea barua yoyote toka cuf ikimtaarifu kuhusu kuvuliwa uanachama kwa Rashid Hamad,mbunge wa Wawi,Chakechake.Na kuwa,hata wakipeleka bungeni,bado bunge litasubiri apate yeye kwanza barua hiyo.


Akizungumza jijini Dar es salaam,Tendwa alisema kuwa kutokana na cuf kujiunga na Chama cha Mapinduzi na kuunda serikali ya umoja wa kitaifa (SUK),hataweza kukifuta kwani kinaendesha serikali kwa upande wa
Zanzibar.

Tendwa alisema kuwa,haungi mkono tamko lililotolewa na mwanasheria mkuu kuwa hakifai kuwa chama cha siasa nchini kwani kuna vigezo vingi vinavyofanya chama kuondolewa sifa hiyo.

Alibainisha kuwa,sifa mojawapo ni pamoja na kuvunja katiba ambayo wao wameivunja, kisheria hawatakiwi kuwa chama cha kisiasa hapa nchini pia kama chama kitaendeshwa upande mmoja tu wa nchi,kitakuwa kimekosa sifa za kuwa chama cha siasa.

Tendwa alibainisha sifa nyingine kuwa ni pamoja na kufanya vikao halali,kutumia lugha za uchochezi hayo ni kati ya mambo yanayokifanya chama husika kupoteza sifa.

Akizungumzia amri iliyotolewa na Mahakama kuu ya Tanzania juu ya kutofanyika kwa mkutano uliomfukuza Hamad na wenzake,Tendwa alikiasa CUF kuacha kuidharau mahakama kwani ipo kikatiba na kwamba warudi chini wazungumze kuliko kuendelea kurumbana na kuitolea maneno ya kebehi mahakama kuu.

“Kama kuna mazungumzo ndani ya chama cha siasa ni tiba bora kwani hupunguza migogoro ambayo inaweza kupunguza demokrasia.Mhili mmoja uliwishatoa amri, ni vyema ifuatwe.Ukifanya kitu kinyume na mahakama ni batili hivyo CUF walipaswa kuheshimu maamuzi ya mahakama”,alisema Tendwa.

Aidha,Msajili alivitaka vyama kutumia muda mwingi kujijenga kuliko kukaa na kufukuzana ,hivi sasa wanachama wa CUF wanajiondoa uanachama kutokana na maamuzi ya watu wachache,jambo linalomsikitisha zaidi.

Msajili pia alivitaka vyama hasa CUF,kuacha kufanya vurugu kwa kutumia vikundi vya ulinzi vya chama pindi makada wa chama hicho wanapokwenda kutoa misaada au kuhutubia kwenye mikutano mbalimbali ya matawi ya chama hicho.Tukio la kupigwa kwa wafuasi wa Hamad Rashid tawi la CUF Manzese hivi karibuni,limehusihwa na kauli hiyo ya Tendwa.

Katika hatua nyingine,Msajili amevitaka vyama vyote vilivyoshiriki uchaguzi mdogo wa jimbo la Igunga,vinapaswa kurejeshwa kwa mrejesho wa hesabu za fedha walizotumia kipindi cha uchaguzi huo mdogo uliomweka madarakani, Dk.Peter Kafumu kutoka CCM.

Alibainisha kuwa, vyama vyote vilivyoshiriki uchaguzi mkuu wa 2010,vijiandae kutembelewa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za serikali kwani tayari amekwioshapata hesabu za vyama vyote 18 vilivyopata usajili wa kudumu.

Msajili wa vyama vya siasa hapa nchini,kisheria ndiye mlezi wa vyama vyote vilivyopata usajili wa kudumu ambapo huvihitaji vyama hivyo kufuata sheria na taratibu za kuendesha vyama hivyo.

Hivi karibuni katika siasa za Tanzania,vyama vya NCCR-Mageuzi na CUF,viliwatimua makada wao ambao pia ni wabunge ambapo CUF kilimtimu mbali Rashid na NCCR kilimtimua David Kafulila mbunge wa Kigoma Kusini kutokana na kukiuka baadhi ya misingi iliyopo kwenye katiba za vyama vyao.

2 comments:

  1. jikateni huko nyie Wa Tanganyika mambo ya ndani ya Zanzibar hayawahusu so shut fack up u peoples mind your own business.

    ReplyDelete
  2. Kazi, kweli kweli!..haya si maoni bali ni maji taka! Mimi nlitarajia hicho kiingereza kisaidie kujibu hoja za Mwanasheria mkuu na Msajili wa vyama vya siasa ktk hilo sakata la CUF badala yake unakitumia kutukana watu?...Mungu akusaisie!

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.