Habari za Punde

Mama Asha Atembelea Soba House

 Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Asha Balozi Seif Ali Iddi, akitembelea maonesho ya Vijana wa Soba House , ambazo hutumia muda wao kwa kazi za Amali wakiwa katika Vituo hivyo  
 Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Balozi akitembelea maonesho ya vifaa vya Vijana wa Soba House katika moja ya nyumba za Vijana hao Mpendae Zanzibar. 
 MKE wa Makamo wa Pili wa Rais Mama Asha Balozi Seif  Iddi kulia,akimkabidhi Vyarahani,nyuz kushonea,Mchele.Sabuni na Sukari,Kiongozi wa Vijana walioacha kutumia dawa ya kulevya na kujifunza tabia njema Fatuma Sukwa,makabidhiano hayo yamefanyika katika moja ya nyumba hizo Detroit Sobar House Mpendae jana,(Picha na Abdallah Masangu).
 Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Balozi Seif, akimkabidhi Vifaa Kiongozi wa Nyumba za Soba House Suleiman Mauliy.
 Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Balozi Seif, akitowa nasaha zake kwa Vijana wanaoishi katika nyumba hizo za Soba House, kuacha matumizi ya Dawa  wanapomaliza muda wao wa kupata ushauri wakiwa katika makazi hayo na kuendelea na tabia nzuri walizo jifunza.   
 Kiongozi wa  Vijana Wanaoishi katika nyumba za Soba House akitowa historia ya  nyumba hizo wakati wa sherehe za kukabidhiwa misaada mbali kwa ajili ya vituo hivyo kujiendeleza kwa kazi xza mikono wanazofanya vijana hao wakiwa katika vituo hivyo.
 Vijana wa Soba House wakimsikiliza Mke wa Makamu wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Balozi Seif, akitowa nasaha zake.
Wake wa Viongozi  Wabunge na Wawakilishi wakiwa katika hafla hiyo ya kukabidhi zawadi kwa vijana hao wakiwa katika viwnja hivyo .

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.