Na Waandishi Wetu
BALOZI wa Marekani nchini Tanzania,
Alfonso Lenhardt, amesema kuwa nchi yake imesikitishwa na machafuko ya siku
mbili yaliyosababisha uvunjifu wa amani hapa Zanzibar.
Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari, Balozi Lenhardt alisema fujo
zilizotokea ni za kusikitisha na kutaka hatua za haraka zichukuliwe katika
kurejesha amani visiwani Zanzibar.
Balozi huyo alitaka viongozi wa kisiasa kushiriki kikamilifu katika
kuirejesha amani, ambapo alisema machafuko ya siku mbili yameharibu sifa nzuri
ya amani iliyopo Zanzibar,
hasa baada ya kumalizika kwa uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010.
Balozi Lenhardt alisema amani ni suala muhimu sana
kwa visiwa vya Zanzibar
kwani kwa kiasi kikubwa uchumi wa visiwa hivyo umekuwa ukitegemea sekta ya
utalii ambayo huimarika zaidi panapotawala amani na utulivu.
Katika hatua nyengine Baraza la
Waislamu Tanzania (BAKWATA), limelaani vurugu na machafuko yaliyotokea Zanzibar, ambayo
yamesababisha kuchomwa makanisa.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es
Salaam, msemaji wa vijana wa Baraza hilo Said Mwaipopo, alisema kuwa waislamu si
watu wa vurugu na kwamba watu wamefanya kwa kutumia kusingizio cha dini.
Alifahamisha kuwa hakuna sehemu yoyote katika kitabu kituku cha qur-ani
ambacho kinahamasisha vurugu dhidi ya dini nyengine na kwamba vurugu hizo
zimefanywa na watu kwa kisingizio cha dini kupitia jumuiya ya UAMSHO.
Akizungumzia madai ya kikundi cha UAMSHO juu ya kupinga Muungano,
Mwaipopo alisema kama kunahitajika kutoa maoni
juu ya Muungano isubiriwe tume iliyoundwa kwani ndiyo yenye kazi ya kukusanya
maoni juu ya katiba mpya.
“Kama kuna lolote wanalolipinga dhidi ya Muungano, wawakataze wajumbe kuingia
kwenye tume hiyo pia wabunge wasishiriki, lakini hakuna maoni yatakayopokelewa
kwa kufanya vurugu na kuharibu mali
za wasiohusika”, alisema.
Nacho Chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA), kimevitaka vyombo
vya ulinzi na usalama kuhakikisha vinarejesha hali ya amani na utulivu pamoja
na kufanya uchunguzi wa kina dhidi ya waliohusika na matukio ya vurugu.
Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA
Zanzibar, Hamad Yussuf alisema vyombo vya ulinzi na usalama kuchukua jitihada za kudhibiti fujo
zinazofanywa na vijana ambao wana lengo la kutaka kuvunja amani na utulivu
uliopo.
Aidha aliwataka wananchi kushirikiana na vyombo hivyo ili wale wote
waliohusika na ufanyaji fujo huo uliosababisha haarsa kubwa wanakamatwa na
kufikishwa katika vyombo vya sheria.
Hamad, alisema Muungano hauwezi kupingwa kwa vurugu na kuwataka
wananchi wajipange kwa hoja zitakazoweza kuandikwa katiba ambayo itaondoshwa
mizwengwe iliyopo katika Muungano.
Alivitaka vyama vya siasa kuacha kuandaa makundi ya vijana ambao mwisho
wake wanakosa kuwapatia kazi, hali inayowafanya hukosa shughuli za kufanya na
hatimaye kuwa na vikundi vya kihalifu.
Chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) Zanzibar kimepokea kwa masikitiko makubwa
taarifa za kutokea kwa fujo zilizopelekea uchomwaji moto gari, nyumba za ibada
na nyumba za wananchi.
Nacho Chama cha CUF, kimesema kuwa machafuko
yaliyotokea yamesababishwa na wachochezi wasiopenda kuona serikali ya Umoja wa
Kitaifa inanawiri visiwani Zanzibar.
Akitoa taarifa ya Chama hicho Mkurugenzi wa Haki za Binaadamu, Habari,
Uenenzi na Mawasiliano ya Umma, Salum Bimani alisema CUF haiwezi kukaa kimya
kuona hali tete ya kuchezewa kwa amani ikitokea.
“Chama cha CUF, kinatoa wito kwa wananchi wote kuwa watulivu,
wavumilivu, na kuitumia fursa ya kutoa mawazo yao
bila ya jazba, pamoja na kutowanyima wengine nafasi ya kuwasilisha mitazamo yao”, alisema Bimani
katika taarifa hiyo.
Alibainisha kuwa vitendo vya watu wachache kuchoma makanisa na kuharibu
mali za watu ni vya uvunjifu wa sheria na kinyume na utamaduni wa Kizanzibari
na kutaka uchunguzi wa kina ufanyike na waliohusika wachukuliwe hatua za
kisheria, bila uonevu wala upendeleo.
Kama, kweli CUF ni waungwana wanatakiwa watuombe radhi kwa kitendo walichokifanya.
ReplyDeleteManeno ya Naibu katibu mkuu wa CCM Z'bar Vuai Ali Vuai ni ushahidi tosha kwamba CUF wanahusika na vurugu zilizotokea.
Abubakar Khamis Bakar akiwa waziri wa sheria na katiba ameewaacha UWAMSHO kufanya kazi kinyume na malengo ya kuanzishwa kwake.
Hivi kweli yule mzee ndio hakujua kwamba UWAMSHO ilianzishwa ili kutoa mihadhara ya dini ya kiislamu na siyo siasa za majukwaa au kuwahoji watu kama wanataka muungao au laa?
Kwa kweli CUF wameshikwa 'pabaya' tena hii mara ya pili, wakati ule waziri wao akasababisha vifo vya watu takriban 2000 kwa uzembe wa kusimamia vyombo vya usafiri na akakataa kujiuzulu.
Sasa tuone watafanya nini: wataifuta UWAMSHO na Abubakar kujiuzulu au watafanya yaleyale?
Kwa kweli CUF tumetokanayo mbali lakini naona sasa washatuchosha na lau kama si historia ya siasa chafu za CCM-Z'bar(1995-2005) za 'over reaction' kwa kumsingizia kila mtu kua ni CUF na kuwapiga 'pande' jamaa wa 'kisiwani' naamini wengi wangerudi CCM!