6/recent/ticker-posts

Dk Shein Akutana ns Watendaji Wizara ya Kilimo na Maliasili

STATE HOUSE ZANZIBAR 
OFFICE OF THE PRESS SECRETARY
 PRESS RELEASE Zanzibar 21.5.2012 


 WIZARA ya Kilimo na Maliasili imeeleza kuwa Mapinduzi ya Kilimo yataendelezwa kwa lengo la kujijengea uwezo wa kuwa na uhakika wa chakula na kupunguza kwa kiasi kikubwa utegemezi wa chakula kutoka nje ya nchi. 

 Uongozi wa Wizara ya Kilimo na Maliasili ulieleza hayo leo katika mkutano wa kuangalia utekelezaji wa kazi za Wizara hiyo kwa kuangalia robo tatu ya utekelezaji wa Bajeti ya mwaka wa fedha 2011-2012 na kulinganisha na robo ya kwanza na ya pili pamoja na vipaumbele na malengo kwa mwaka wa fedha 2012-2013. 


 Mkutano huo uliofanyika Ikulu mjini Zanzibar ambapo Mwenyekiti wake ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein pia, ulihudhuriwa na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad pamoja na Katibu Mkuu Kiongozi na Katibu wa Baraza la Mapinduzi Abdulhamid Yahya Mzee. 

Uongozi huo, ulieleza kuwa ni vyema ikafahamika kuwa dunia hivi sasa imekabiliwa na hali ya upungufu mkubwa wa chakula na tishio la njaa ambapo sababu kuu za hali hiyo ni pamoja na upungufu mkubwa wa uzalishaji wa nafaka, mabadiliko ya tabia nchi.

 Jengine ni gharama kubwa za uzalishaji kutokana na kupanda kwa bei za mafuta na mahitaji makubwa ya nafaka yanayotokana na kuongezeka kwa matumizi mbadala ya nafaka hali ambayo imepelekea ushindani mkubwa katika masoko ya nafaka ya kimataifa na hivyo upandaji wa bei za vyakula kuongezeka. 

Kutokana na hali hiyo, Wizara hiyo ilieleza kuwa kwa kipindi cha muda mfupi na wa kati imekusudia kutekeleza Mpango wa Kuendeleza Kilimo cha Mpunga ulioridhiwa na Baraza la Mapinduzi kwa lengo la kupunguza utekegemezi wa mchele kutoka nje ya nchi. 

Akitoa taarifa ya Wizara hiyo, Kaimu Waziri wa Kilimo ambaye pia ni Waziri wa Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati Mhe. Ramadhan Abdalla Shaaban alisema kuwa Mpango huo umeanza kutekelezwa katika bajeti ya mwaka huu wa Fedha 2011/212. 

 Aidha, Waziri huyo alisema kuwa Wizara imelenga kuongeza uzalishaji wa mazao mengine muhimu ya chakula yakiwemo muhogo, ndizi, viazi vitamu na mbogamboga, mazao ambayo hivi sasa uzalishaji wake umekuwa ukiongezeka siku hadi siku. 

 Alieleza kuwa lengo la Wizara ni kukabiliana na changamoto za uzalishaji ikiwemo maradhi, wadudu pamoja na upungufu wa mbegu bora kwa baadhi ya mazao hayo. Wizara hiyo pia, ilieleza kuwa kutokana na umuhimu wa zao la karafuu kwa Zanzibar, Wizara imelenga kuendelea na jitihada zake za kuendeleza uzalishaji wa miche ya mikarafuu na kuisambaza kwa wakulima bila ya malipo pamoja na kufuatilia maendeleo ya zao hilo kwa karibu zaidi huku ikieleza juhudi zilizofanywa kwa kuwasaidia wakulima pembejeo za kilimo na kuwawezesha kuwa na mori na hamu ya kilimo. 

 Sambamba na hayo, Wizara hiyo imeeleza kuwa iwapo kilimo kitaendelezwa na kikawa cha ufanisi na tija zaidi mafanikio makubwa kwa wananchi katika kupunguza ukali wa maisha, kuondokana na umasikini na nchi kupiga hatua zaidi za ukuaji wa uchimi yatapatikana. Wizara hiyo pia, imkeeleza mafanikio yaliopatikana katika kuimarishaji wake wa Shamba Darasa, ambazo hutoa mafunzo ya kilimo kwa wakulima na kuijengea sifa Zanzibar na kuwa kivutia kwa wageni, wahisani na hata wakulima kutoka nje ya nchi. 

 Pamoja na hayo, Wizara imeeleza mashirikiano mazuri kati yake na Wizara ya Biashara, Viwanda na Masoko katika kuimarisha mazao ya viungo huku ikieleza tafiti mbali mbali zilizofanyika Unguja na Pemba sanjari na program kadhaa zinazokusudiwa kufanywa. 

 Nae Makamu wa Kwanza wa Rais Maalim Seif Sharif Hamad, alieleza kuwa Wizara ya Kilimo na Maliasili ina mengi na imepiga hatua kwa kupata mafanikio hivyo juhudi zinahitajika za kuwaeleza wananchi. Kwa upande wake Rais Dk. Shein ametoa pongezi kwa Wizara hiyo kutokana na mafanikio makubwa yaliopatikana na kuitaka kuyatangaza mafanikio hayo ili wananchi wayajue kwa kupitia vyombo vya habari vya ndani na nje ya Zanzibar. 

 Alieleza kuwa Wizara hiyo imepiga hatua katika mipango yake na malengo iliyojiwekea hivyo ni jambo la busara wananchi wakajua juhudi za Serikali ilizozichukua katika sekta ya kilimo kupitia Wizara hiyo. Wakati huo huo, Dk. Shein alikutana na uongozi wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, chini ya Waziri wake Mhe. Abdilahi Jihad Hassan na kueleza ambapo katika taarifa yao ya Mpango kazi, Robo ya Kwanza hadi ya Tatu

Wizara hiyo pamoja na mambo mengineyo ilieleza malengo yake ikiwa ni pamoja na kutoa elimu bora ya ufugaji na uvuvi. Aidha, Wizara hiyo ilieleza utekelezaji wake wa kutoa taaluma ya uvuvi bora na kuzuia uvuvi haramu ili kuimarisha mazingira ya bahari na fukwe sanjari na kuendeleza uvuvi wa kienyeji, ufugaji mazao ya bahari na uvuvi wa bahari Kuu. Aidha, Wizara hiyo ilieleza tatizo la uvamizi wa maeneo mbali mbali vijijini yakiwemo Madiko, Mashamba na vituo vya kufanyia kazi ambapo Wizara hiyo imeamua kuyatafutia hati miliki.Aidha, Wizara hiyo ilieleza maagizo ya Rais na yale ya Makamu wa Kwanza wa Rais. 

Nae Dk. Shein kwa upande wake alipongeza juhudi zinazochukuliwa na Wizara hiyo na kusisitiza haja ya kuziimarisha zaidi ili malengo yaliokusudiwa yaweze kufikiwa.

Post a Comment

0 Comments