Na Fatuma Kitima, DAR ES SALAAM
KUTOKANA na ongezeko la mfumko wa bei nchini gharama za uzalishaji zimeongezeka hali inayosababisha baadhi ya mikopo katika benki kutolipwa kwa wakati.
Taarifa hiyo imetolewa jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei alisema kuwa kupanda kwa gharama za uzalishaji kumepelekea wafanyabiashara na watu wengine waliokopa kuchelewa kurejesha mikopo hiyo.
Dk. Kimei alisema kuwa mfumko huo wa bei nchini umekuwa tatizo hadi kuchangia bei za vyakula kuuzwa bei za juu.
Alisema kuwa Benki ya CRDB imekuwa ikiwawezesha wakulima nchini kwa asilimia 60 ili kuweza kuendesha shughuli zao za kilimo.
Aidha alisema licha ya kupanda kwa riba, ujazo mdogo katika soko la mabenki na kupanda kwa dhamana za serikali, lakini benki ya CRDB bado hawakuongeza riba kwa wateja wake.
Dk.Kimei alisema katika mwaka wa 2012 mapato ya riba yameongezeka asilimia 35, gharama za riba asilimia 78, mapato halisi ya riba asilimia 26, mapato fedha za kigeni asilimia 33,mapato mengine asilimia 36, tengo la mikopo isiyolipika asilimia 51, jumla ya gharama za uendeshaji asilima 21,faida kabla ya kodi asilima 34,pamoja na namba ya wafanyakazi ni asilimia 20.
Benki hiyo ilifanya maboresho katika huduma za kibenki kupitia matumizi ya mitandao ya sim za mikononi (simbanking) inayoweza kutoa huduma.
Hata hivyo alisema benki hiyo inampango wa kuongeza ATM 50 nchini katika mikoa mbalimbali pindi watapopata kibali ili kupunguza gharama kwa wateja wake kwenda masafa marefu kupata huduma hiyo.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Dhow Financial ltd Prof.Mohamed Warsame Benki hiyo inatoa mikopo mingi kwa wakulima na mwaka huu wataanza tena kukopesha.
Prof. Warsame alisema kuwa muelekeo wa huduma za benki zinaendelea vizuri na miaka 5 ijayo wanategemea hisa zitapanda bei ,kwasasa ni 130 zimepungua ikiwa kipindi kilichopita ni zaidi ya 200.
No comments:
Post a Comment