Mh. Mgeni rasmi, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
baraza la Mapinduzi
Dr. Ali Mohammed Shein
Nd. Mwenyekiti wa ZATUC
Nd. Zahran Muhammed Nassor
Nd. Waziri wa Kazi, Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi na
Ushirika
Nd. Haroun Ali Suleiman
Mkurugenzi wa Jumuiya ya
Waajiri ZANEMA
Nd. Salahi Salim Salahi
Mwakilishi wa ILO Zanzibar
Bibi. Fatma Mohammed Rashid
Viongozi wa vyama vya
wafanyakazi
Viongozi mbali mbali wa
Serikali
Viongozi wa taasisi binafsi
Nd. Wafanyakazi
Nd. Wananchi
Mabibi na mabwana
Asalaam alaykum
IFUATAYO NI RISALA YA
WAFANYAKAZI WA ZANZIBAR KUPITIA SHIRIKISHO LA VYAMA VYA WAFANYAKAZI ZANZIBAR
KATIKA KUADHIMISHA SIKU YA WAFANYAKAZI DUNIANI TAREHE 01- 05 – 2012
Mhe. Mgeni Rasmi, ndugu viongozi na ndugu wafanyakazi
Kwanza kabisa nichukue fursa hii kumshukuru M/ Mungu mwingi
wa rehema kwa kutujaalia kufika hapa tukiwa wazima wa afya zetu na usalama wa
nchi yetu
Pili, tunapenda kukushukuru wewe Mh. Rais kwa
kukubali kwako kuwa Mgeni Rasmi katika siku hii adhimu inayoadhimishwa kila
mwaka na Wafanyakazi Duniani
Tatu, tunawashukuru wageni wetu waalikwa, viongozi
wafanyakazi na wananchi wote kwa kuhudhuria kwenu kwa wingi katika hadhara hii
Mhe. Mgeni Rasmi, ndugu viongozi na ndugu wafanyakazi
Siku ya wafanyakazi duniani (Mai Dei) ni miongoni mwa
kumbukumbu muhimu duniani kote ambayo haitasahaulika kwani inaashiria historia
iliyotokea siku ya tarehe 1 Mei, 1889 ambapo wafanyakazi huko CHICAGO Marekani
waliandamana kwa amani kwa madhumuni ya kupinga madhila waliyokuwa wakifanyiwa
katika sehemu zao za kazi na kudai haki zao, maslahi yao na hali bora za
usalama katika sehemu za kazi zao,
Baadhi ya madhila ambayo waliyapinga wafanyakazi hao
ni
· Kufanyishwa kazi kwa masaa mengi bila
mapumziko wala malipo ya ziada
· Kulipwa mishahara duni isiyokidhi hali zao
za maisha
· Kafanyakazi katika mazingira yasiyo na
usalama kiafya nay a hatari
· Kubaguliwa katika sehemu zao za kazi hasa
ubaguzi wa rangi
· Kudhalilishwa katika sehemu za kazi
Lakini badala ya kusikilizwa na waajiri na Serikali ya
wakati huo huko Marekani, mabavu yalitumika na kuwatawanya kwa mitutu ya
bunduki na kwa masikitiko makubwa maelfu ya wafanyakazi wasio na hatia waliuwawa.
Pamoja na kwamba ni miaka 123 imepita tangu tukio hilo
litokee wafanyakazi wote Duniani wanaendelea kuliadhimisha kila ifikapo tarehe
kama ya leo
Vile vile tukio hilo limekuwa kichocheo kinachopelekea
wafanyakazi kote Duniani kuendelea kudai haki, maslahi zaidi na mazingira bora
ya kazi zao na kuhakikisha wanatambuliwa kuwa ni wadau muhimu katika maendeleo
ya nchi na jamii zao. Hasa kwa vile bado baadhi ya nchi duniani hali haiko
tofauti sana na ile ya wafanyakazi wa Chicago ya Mwaka 1889
Siku hii pia hutumika kuhimiza ajira zenye staha katika nchi zote duniani, yaani zenye maslahi
bora na heshima kwa lengo la kuondowa migogoro, migongano na kutoaminiana baina
ya Wafanyakazi, Waajiri na Serikali zao.
Ajira zenye Staha ni tamko la kimataifa la shirika la
kazi duniani linaloelekeza nchi zote duniani kuhakikisha mambo yafuatayo
1. Fursa za kuajiriwa au kujiajiri kwa wananchi zinaimarishwa
2. Haki
za msingi za wafanyakazi zinalindwa
katika nchi
3. Majadiliano
ya pamoja na ufungwaji wa mikataba kwa wafanyakazi na ushirikishwaji katika mambo ya ajira kwenye ngazi
zote.
4. Hifadhi
ya jamii kwa wafanyakazi
na familia zao zinakuwepo
Mhe.
Mgeni Rasmi, ndugu viongozi na ndugu wafanyakazi
Miongoni mwa haki za msingi za wafanyakazi duniani
ambazo kwa bahati nchi yetu imeridhia ni inastahiki kuzilinda ni kama zifuatazo
1. Haki wa kujiunga pamoja na kufanya shughuli
za vyama vya wafanyakazi bila kuingiliwa
2. Haki ya kujadiliana na muwajiri juu ya
masula na mazingira ya kazi na kufungiana mikataba ya hali bora za kazi
3. Haki ya kutofanyisha kazi za shuruti na
kazi za utotoni
4. Haki za utokubaguliwa au kudhalilishwa
katika sehemu ya kazi yako
5. Haki ya kulidwa kwa watoto na vijana na
kazi za hatari
6. Hati ya kupata mafao sawa kwa kazi
zinazofanana
Mhe.
Mgeni Rasmi, ndugu viongozi na ndugu wafanyakazi
Wafanyakazi wa Zanzibar tunamshukuru M/Mungu kwa
kupata fursa ya kushirikiana nawe katika maadhimisho haya adhimu, kama
ulivyoshuhudia tumeandamana kwa amani ilikuonyesha furaha yetu kwako na hisia
zetu kwa Serikali yako na waajiri. Fursa
hii vile vile inatupa hamu ya kuelezea wazi wazi mafanikio yaliyofikiwa na Serikali unayoiongoza chini ya muundo wa
Umoja wa Kitaifa unayoiongoza katika kipindi kifupi cha kuwa madarakani,
Miongoni mwa mafanikio hayo ni
1. Kuendeleza hali ya amani na utulivu hapa
nchini kitendo kilichowafanya wafanyakazi na wananchi kuendelea na kazi zao
bila wasiwasi wowote.
2. Kutoa fursa kwa vyama vya wafanyakazi
kutekeleza shughuli zao bila kuingiliwa au kubughudhiwa na mtu au chombo
chochote humu nchini.
3. Jitihada zako za kushirikiana na vyama vya
wafanyakazi katika kutatua kero zao na kutoa huduma bora kwa wananchi
4. Juhudi unazozifanya katika kuimarisha
Maslahi ya wafanyakazi wake. mfano
· Kuunda wizara maalum inayoshughulikia
maslahi ya wafanyakazi
· Kurejesha utaratibu wa kupandisha ngazi
watumishi
· Kurejesha utaratibu wa nyongeza za mwaka
· Kuzingatia taaluma katika kupanga mishahara
ya wafanyakazi
· Kuzipa vipaumbele taaluma adimu
· Kupambana na tatizo la wafanyakazi hewa na
malipo hewa
5. Kuimarishwa kwa kitengo cha kutatua
migogoro
6. Kuundwa
kwa kamati ya kitaifa ya afya na usalama katika sehenu za kazi
7. Bodi ya ushauri wa mambo ya kazi sasa inakutana
kwa mujibu wa sheria.
8. Kukutana kwa bodi ya ushauri wa kima cha
chini cha mshahara na kupitia mishahara ya sekta binafsi.
9. Kuwashirikisha wafanyakazi katika michakato
ya kitaifa
10. Kuanzisha mchakato wa kutungwa kwa sera ya
hifadhi ya jamii
Mhe. Mgeni Rasmi, ndugu viongozi na ndugu wafanyakazi
Pamoja na hatua tulizoziainisha na tulizokuwa
hatukupata muda wa kuzieleza bado wafanyakazi wale wa Serikalini, sekta binafsi
na sekta isiyo rasmi kwa Mwaka mmoja uliyopita haukuwa mzuri sana, hali hii ilisababishwa
na mambo mengi yalijitokeza katika kipindi hicho yakiwemo yafuatayo
1. Kuendelea kuwepo kwa matatizo makubwa
katika utaratibu wa nyongeza za mishahara ulifanywa na serikali mwaka jana.
mfano
· Vyama vya wafanyakazi kutoshirikishwa
kabisa katika mapendekezo ya nyongeza za mishahara ya serikali kama sheria ya
ajira inavyoeleza.
· Serikali kushindwa kutoa malimbikizo ya
mishahara kwa wale waliochelewa kufanyiwa marekebisho kama utaratibu
unavyotakiwa
· Serikali haikuwa makini katika
utekelezaji nyongeza za mishahara kiasi kwamba lilileta usumbufu kwa baadhi ya wafanyakazi.
2. Kuchelewa kutekelezwa kwa masuala ya
kisheria juu ya masuala ya maslahi ya wafanyakazi
a) Uundwaji wa kanuni za sheria za kazi.
b) Uundwaji wa Idara ya fidia
c) Mahakama ya kazi ya Zanzibar kukosa jengo
na kanuni
3. Kutokuwajibika kwa baadhi ya watendaji
katika kusimamia sheria za kazi
·
Kutokusimamia
ipasavyo ufungaji wa Mikataba ya kazi sehemu za kazi hasa katika sekta binafsi jambo
linalopelekea wafanyakazi kukosa haki zao.
·
Kutokuwasilishwa
kwa Mikataba ya Kimataifa katika Baraza La Wawakilishi la Zanzibar
·
Bodi
ya ushauri wa mishahara kutokutumiwa katika kupendekeza mishahara Serikalini kama
sheria inavyolekeza.
4. Upungufu wa vitendea katika baadhi ya
sehemu za ambavyo vilidumaza uwezo wa utendaji wa kazi katika sehemu zao za
kazi.
5. Kutokuwepo kwa chombo cha Kitaifa cha
majadiliano katika masuala ya kazi
6. Ushirikishwaji mdogo wa wafanyakazi katika
masuala yanayowahusu kwa mujibu wa sheria (Kamati za uongozi).
7.
Madeni
ya serikali juu ya haki za wafanyakazi kama vile likizo, overtime na fidia.
8.
Baadhi
ya waajiri kutokutoa ushirikiano wa
kutosha juu ya utekelezaji wa tamko la kupandishwa kima cha chini cha
mshahara wa sekta binafsi
9. Baadhi ya viongozi wa Serikali na taasisi
za binafsi kuwa na mtazamo hasi juu ya kuwepo na kufanyakazi kwa vyama katika
sehemu zao za kazi na Kitaifa.
10.
Wafanyakazi
wa mashirika ya umma kuchelewa kufanyiwa marekebisho ya mishahara yao kila
ambapo wafanyakazi wengine wa serikali wanaporekebishiwa mishahara
Mhe. Mgeni Rasmi, ndugu viongozi na ndugu wafanyakazi
Wafanyakazi wa Zanzibar wanaendelea kukosa usingizi
juu ya hali inavyoendelea nchini mwetu kwa maoni mwa mambo yanayo wapa taabu
sana ambayo viongozi wa serikali iliyopo madarakani ni lazima wayashughulikie
ni
1. Wasi wasi wa wafanyakazi kuhusu kuendelea kupanuka
kwa pengo baina ya watumishi wa kawaida na wale wa ngazi za juu (wateuliwa wa
Rais)
2. Mazingira ya kazi kiafya na usalama
yanahitaji kuboreshwa
3. Wasi wasi wa wafanyakazi juu ya miswada ya
sheria inayopelekwa katika Baraza la Wawakilishi bila kuzingatia mahitaji na
haki za msingi ya wafanyakazi
4. Tatizo la ukosefu wa ajira miongoni mwa
vijana linatishia usalama wa nchi wakati wo wote kuanzia sasa.
5. Masula ya msingi ya kazi kama vile hifadhi
ya jamii na fidia kwa wafanyakazi kutokuwepo chini ya wizara ya kazi jambo
linalosababisha ushiriki wa vyama vya wafanyakazi kuwa mdogo.
6. Kujitokeza kwa vikundi vinavyo hatarisha
amani kwa kukashifu wananchi wenzao na viongozi kwa visingizio vya dini
7. Hali za baadhi ya viongozi kutokuzielewa
sheria za kazi na kufikia hadi kuwabughudhi wanachama wa vyama vya wafanyakazi
Mhe. Mgeni Rasmi, ndugu viongozi na ndugu wafanyakazi
Wafanyakazi tunamatarajio makubwa kwamba viongozi mliomadarakani
mtajitahidi kufuata sheria, kutandika miongozo mizuri ya utawala bora na
kutimiza ahadi zenu mlizozitoa wakati wa uchaguzi wa 2010 zikiwezo
Ø Kushirikana na vyama vya wafanyakazi katika
kuimarisha mashali ya wafanyakazi
Ø Kutatua kero zinazowakabili wafanyakazi
humu nchini ikiwemo mishahara midogo
Ø Kukuza fursa za ajira kwa vijana wetu
Ø Kuwashirikisha wafanyakazi katika mambo
yanayowahusu kwa mujibu wa sheria.
Ø Kutekeleza sheria za kazi kama zilivyo
pitishwa
Ø Kutekeleza sera ya ajira ya Zanzibar kwa
lengo la kukuza ajira, ufanisi pamoja na kuimarisha sekta ya viwanda.
Ø Kutekeleza mpango wa utekelezaji wa kuondoa
ajira za watoto Zanzibar
Haya yote tunayakumbusha ili yawe vipaumbele serikali
na waajiri kwa malengo yafuatayo
1. Kuimarisha maisha ya wafanyakazi, familia
zao na jamii kwa ujumla.
2. Kuwepo kwa ajira zenye staha (desent work)
na huduma bora kwa umma (quality public sevices delivery)
3. Kuwepo kwa utekelezaji makini wa sheria za
kazi na mikataba ya kimataifa.
4. Kuwepo kwa mashirikiano bora kwa wadau wote
katika kuleta tija, ufanisi na maendeleo ya nchi kijamii na kiuchumi
Mhe. Mgeni Rasmi, ndugu viongozi na ndugu wafanyakazi
Kauli mbiu ya mwaka huu ya maadhimisho ya Mei Mosi
hapa Zanzibar ni
MFUMKO WA BEI KODI KUBWA NI
MISHAHARA DUNI, NI PIGO KWA WAFANYAKAZI
Wafanyakazi wa Zanzibar wameamua kuchagua ujumbe huu
kwa kuzingatia kuwa masuala hayo matatu ni miongoni mwa matatizo makubwa ya
wafanyakazi wa yanayowakabili kwa sasa.
Pamoja na jitihada zinazofanywa na viongozi wa juu,
wizara na Serikali kwa ujumla kuhakikisha mfumko wa bei upungue hapa nchini
bado wafanyabishara na watoa huduma hawaonekani kusikia au kujali hatua hizo za
serikali na wanaendelea na kuuza bidha au kutoa huduma kwa bei za juu
Kupitia ujumbe huu tunaiomba serikali yetu kuchukua
juhudi, hatua za dharura na kuandaa mipango madhubuti kupambana na watu kamahao
wanaojitakia manufaa na utajiri migongoni mwa wananchi ambao maisha yao ni ya
masghaka
.
Aidha, wafanyakazi wa Zanzibar ni miongoni mwa walipa
kodi wakuu na wa uhakika vile vile ndio kundi pekee lenye uhakika wa kulipa
aina zote kodi bila kukwepa. Isisahaulike kuwa wafanyakazi pia ndilo kundi
linalolipa kodi mara nyingi, yaani moja kwa moja na kupitia huduma na bidhaa
Cha kusikitisha ni kwamba kila ukicha kodi zinapanda
na nyingine zinaanzishwa, hivyo anaeumia zaidi ni mfanyakazi na familia yake
Kwa kupitia ujumbe huu tuaiomba serikali kupitia upya
taratibu za kodi anazomgusa mfanyakazi na kuzipunguza ili kumpunguzia mzigo
ambao tayari umemlemea
Suala la mishahara midogo na mafao mengine ni kilio kikubwa
kwa wafanyakazi wa Zanzibar la kusikitisha zaidi ni kwamba pamoja na serikali kufanya
jitihada ya kuongeza mishahara suala hili linakwazwa na kupanda kwa gharama za
maisha
Kwa upande mwengine Serikali kwa kushirikiana na wadau
wake kukubaliana kuongeza kiwango cha mishahara cha sekta binafsi lakini bado
kuna baadhi ya waajiri wanapinga kutoa mishahara hiyo kwa visingizio mbali
mbali na wengine ni jeuri tu
Hivyo basi kutitia ujumbe huu tunaiomba serikali
ilisimamie suala hili kinyume chake linaweza kuleta mtafaruku katika sekta ya
ajira na uhatarisha amani iliopo
Wafanyakazi wa Zanzibar ni wavumilivu sana lakini
uvumilivu unamipaka nasi hatumbeni tufike kuko ndio maaana tunakumbushana hapa
hadharani
Mhe. Mgeni Rasmi, ndugu
viongozi na ndugu wafanyakazi
Kwa kumalizia tungalipenda kutoa nasaha zetu au w itokwa
wafanyakazi wenzetu mliohudhuria hapa na wafanyakazi wote wa Zanzibar kupitia kwenu:-
1. Kuelewa nafasi yetu katika maendeleo ya
nchi yetu kwa kufanya kazi kwa bidii katika kujenga uchumi wetu ilituweze
kuhalalisha madai yetu mbele ya waajiri na serikali kwani penye tija maslahi
huongezeka au HAKI NA WAJIBU NI WATOTO
PACHA.
·Tunawaomba
wafanyakazi kuutumia muda wa kazi kwa kuzajisha mali au kutoa huduma
zilizobora kwa wananchi
·Kufika na kuondoka kazini kwa wakati
·Kujiepusha na uzembe, udokozi, rushwa
,upendeleo na ubaguzi
2. Kuendeleza amani na utulivu katika sehemu
zetu za kazi na nchi yetu na kufanya kazi kwa bidii, maarifa, nidhamu na
ubunifu katika kuongeza tija na kuimarisha huduma bora kwa wananchi
3. Tunatoa ushauri kwa viongozi wa kisiasa,
vikundi vya kiraia , vikundi vya kidini, wafanyakazi wote na wananchi wote wa
Zanzibar kuchukua kila tahadhari ili kuepukana na vurugu, mfarakano, utengano,
ubaguzi, ugomvi, fitna na choyo katika kutekeleza majukumu yao na kushiriki
katika michakato mbali mbali ya kitaifa yanayojitokeza hapa nchini, mfano ni wa
mchakato wa mabadiliko ya katiba. Kwani ushahidi unaonyesha kwamba kuna baadhi
ya taasisi kama hizo tayari wameichukuwa hoja ya katiba kuwagawa wananchi
4. Tunawaomba wafanyakazi na wananchi wote wa
Zanzibar kuchukua kila tahadhari ili kuepukana na maambukizo ya Ukimwi,
kutokaribia Madawa ya kulevya, uharibifu wa mazingira, kuchukia rushwa, ufisadi
na wizi wa mali za umma, mambo ambayo huzorotesha maendeleo ya nchi yoyote.
5. Tunawatahadharisha viongozi tuliowachaguwa
na kuteuliwa kwamba wamepewa jukumu la kutuongoza na si kututawala hivyo
ushirikishwaji wa wafanyakazi na wananchi ni kitu cha lazima. Kwani ushahidi
unaonyesha kwamba kuna baadhi ya viongozi waliochaguliwa na hasa waliteuliwa
kuongoza taasisi za serikali na mashirika wanatumia nafasihizo vibaya kwa
kutokuzingatia haki za wafanyakazi
6. Tunawashauri wafanyakazi wote kujiunga na
kuviunga mkono vyama vya wafanyakazi kama njia ya kuimarisha umoja wetu na
mshikamano wetu na kupata nguvu za kuwasilisha madai yetu mbele ya waajiri na
Serikali. Hatuna wasiwasi kuwa Serikali yetu ni sikivu na iko tayari kutekeleza
maombi yetu.
Sisi wafanyakazi wa Zanzibar tunakuhakikishia Mh. Rais
na Serikali unayoiongoza na wananchi kuwa tumekuwa na tuko tayari kushirikiana
nanyi katika juhudi za kukuza na kuimarisha uchumi wetu kwa faida yetu sote
Mhe. Mgeni Rasmi, ndugu viongozi na ndugu wafanyakazi
Mwisho kabisa tungelipenda kuchukuwa fursa hii kwa mara
nyengine tena kukupongeza sana kwa kufika kwako katika maadhimisho yetu haya na
kwa msaada mkubwa na nasaha unazoendelea kutupa wakati wote na hasa katika
kipindi cha maadhimisho kama haya.
Wafanyakazi wa Zanzibar tunakuahidi kukuunga mkono
katika jitihada zako na Serikali za kuwaletea maendeleo Wazanzibari na
watanzania na tuko bega kwa bega katika kujenga umoja, amani na uchumi wa
taifa.Tunakutakia kila la kheri na tunakuombea kwa M/Mungu akupe afya ili
ukitumikie kipindi chako cha uongozi salama, akupe umri mrefu wenye neema na
familia yako. Tunakuahidi kuendelea kutumia ushauri na busara zako unazotupa na
utakazotupa kwani mchango wako kwa vyama vya wafanyakazi vya Zanzibar wauwezi kuepukika.
Vile vile shukurani zetu dhati kwa Mh. Waziri wetu wa
Kazi, Uwezeshaji wananchi kiuchumi na Ushirika, nd. Haroun Ali Suleiman pamoja na
watendaji wake wote wanaoongozwa na Bibi: Asha Ali Abdulla kwa mashirikiano yao
mema na jumuiya yetu,
Aidha pongezi na shukrani za pekee kwa mh. Waziri wa
utumishi wa umma na utawala bora Mh. Haji Omar Kheir kwa ushirikiano usiokifani
na ZATUC, kusema kweli mh. Kama mawaziri wengine wangaliiga mfano wa mh. Haji
tusingalikuwa hapa katika maendeleo ya nchi. Anajali ushauri wetu ,
anashirikiana nasi katika raha na shida, hana mafuta ya ukubwa . Tumpongezeni
sana na wasaidizi wake wakiongozwa na Bw. Joseph Meza
Shukurani kwa viongozi wote wa serikali, Jumuiya ya
waajiri, Shirika la kazi duniani kwa mashirikiano yao kwetu
Asanteni kwa kunisikiliza
SOLIDARITY FOR EVER
No comments:
Post a Comment