Habari za Punde

Hotuba ya Bajeti ya Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi - 2


IDARA YA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA NA URATIBU WA SHUGHULI ZA WAZANZIBARI WANAOISHI NCHI ZA NJE


1.             Mheshimiwa Spika, Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa na Uratibu wa Shughuli za Wazanzibari wanaoishi Nchi za Nje imeendelea na utekelezaji wa majukumu ya kuimarisha Mtangamano wa Kikanda kwa kuratibu ushiriki wa sekta mbali mbali za Zanzibar katika mikutano hiyo na kuhakikisha kwamba Zanzibar inatumia fursa za kiuchumi zinazotokana na Jumuiya ya Afrika Mashariki, Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika na Jumuiya nyengine za Kikanda. Aidha, imeendelea kusimamia uimarishaji wa ushirikiano mwema na nchi marafiki na Taasisi za Kimataifa pamoja na kuratibu shughuli za Wazanzibari wanaoishi Nchi za Nje na kuwashajihisha Wazanzibari hao kushiriki katika kuiletea Zanzibar maendeleo.

2.             Mheshimiwa Spika, Ofisi ya Ushirikiano wa Kimataifa na Uratibu wa Wazanzibari wanaoishi Nchi za Nje, kwa mwaka wa fedha 2011/2012 iliidhinishiwa TZS 671 milioni kwa kazi za kawaida na hadi kufikia mwezi Machi 2012, Ofisi hii iliingiziwa TZS 554 milioni sawa na asilimia 82.6 ya makadirio ya matumizi ya kawaida na kutekeleza yafuatayo:-


a)       Iliratibu, ilishiriki na kufuatilia shughuli za Ushirikiano wa Jumuiya mbali mbali za Kikanda na kuwawezesha wataalamu wa Sekta mbali mbali kuhudhuria katika mikutano ya Kikanda na ya Kimataifa katika nchi za Kenya, Uganda, Burundi, Rwanda, India, Angola na Mauritius.
b)       Iliendelea kuimarisha juhudi za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kukuza uhusiano mwema na Nchi marafiki na Taasisi za Kimataifa. Idara ilikutana na Wawakilishi wa Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) na wameonesha nia ya kusaidia kuzijengea uwezo Kitengo cha Diaspora na Idara Maalum za SMZ.
c)       Idara kwa kushirikiana na Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki ilitayarisha semina juu ya fursa na faida zitokanazo na Soko la Pamoja la Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa wafanya biashara na Waheshimiwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi
d)       Iliratibu ushiriki wa Zanzibar katika vikao vya matayarisho ya mikutano ya Jumuiya mbali mbali za kikanda na Kimataifa kwa lengo la  kupata msimamo wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  katika Mikutano hiyo
e)       Ilitayarisha Mpango Mkakati wa Diaspora.
f)        Maafisa wa Kitengo cha Diaspora na wadau wengine wamefanya ziara katika nchi za Falme za Kiarabu (Oman na Dubai) kwa lengo la kukutana na Wazanzibari ili kuwashajihisha kushiriki katika kuchangia maendeleo ya Zanzibar.
g)       Iliitangaza dhana ya Diaspora kwa kutayarisha vipindi vilivyorushwa hewani na ZBC TV na Redio na watendaji walihudhuria mikutano ya Diaspora iliyofanyika Uganda na Afrika ya Kusini.

Jumuiya ya Afrika Mashariki


3.             Mheshimiwa Spika, mkutano wa 13 wa kawaida wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki ulifanyika tarehe 30 November, 2011 nchini Burundi. Mkutano huo uliichagua Jamhuri ya Kenya kuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Miongoni mwa mambo muhimu yaliyojadiliwa katika mkutano huo ni kupitisha Sera na Mkakati wa Viwanda wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Itifaki ya kuzuia na kupambana na rushwa, Itifaki ya ushirikiano wa ulinzi, Himaya moja ya Forodha ya Jumuiya ya Afrika Mashariki na maombi ya Jamhuri ya Sudan na Jamhuri ya Sudan Kusini kujiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki. Wakuu wa Nchi walikubaliana kuwa Jamhuri ya Sudan haiwezi kuwa mwanachama kutokana na kutotimiza vigezo vya kujiunga na Jumuiya hiyo. Kwa upande wa Jamhuri ya Sudan Kusini, Wakuu wa Nchi waliliagiza Baraza la Mawaziri kupitia vigezo na baadae wawasilishe maoni yao katika mkutano wa 10 wa dharura wa Wakuu hao. Wakati huo huo, Wakuu wa Nchi waliunga mkono hatua zinazochukuliwa na Serikali ya Kenya ndani ya Somalia ili kulinda amani, usalama na utulivu.

4.             Mheshimiwa Spika, mkutano wa dharura wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki ulifanyika tarehe 28 Aprili, 2012. Pamoja na mambo mengine, Mkutano huo ulimchagua Naibu Katibu Mkuu Mheshimiwa Jesca Eriyo kutoka Uganda na kumuongezea muda wa kuwa Naibu Katibu Mkuu Mheshimiwa Jean Claude Nsengiyumva kutoka Burundi. Aidha, mkutano huo ulipokea taarifa ya Baraza la Mawaziri katika hatua zilizofikiwa katika Himaya moja ya Forodha ya Jumuiya ya Afrika Mashariki na taarifa ya vigezo vya Jamhuri ya Sudan Kusini kujiunga na Jumuiya. Katika mkutano huo, Baraza la Mawaziri liliagizwa kuharakisha mchakato wa kuangalia vigezo iwapo Jamhuri ya Sudan Kusini inaweza kujiunga na Jumuiya. Hata hivyo, Wakuu wa Nchi walisikitishwa na mgogoro unaoendelea kati ya Jamhuri ya Sudan na Jamhuri ya Sudan Kusini.

5.             Mheshimiwa Spika, utekelezaji wa Soko la Pamoja la Jumuiya ya Afrika Mashariki bado unasuasua. Katika mkutano wa 15 wa Kisekta wa Baraza la Mawaziri uliofanyika Kampala mwezi Januari 2012, Nchi Wanachama walielezea wasiwasi wao wa kutoridhishwa na mwenendo wa ratiba ya kufungua maeneo yaliyokubalika pamoja na marekebisho ya Sheria za Nchi katika utekelezaji wa Soko la Pamoja. Katika kulipatia ufumbuzi suala hili, Baraza la Kisekta liliamua kuunda Kamati za Kitaifa za utekelezaji wa Soko la Pamoja kwa kila Nchi Mwanachama. Katika Kamati hiyo, Zanzibar inawakilishwa na Makatibu Wakuu watatu kutoka Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Wizara ya Biashara, Viwanda na Masoko na Wizara ya Kazi Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi na Ushirika.

6.             Mheshimiwa Spika, majadiliano ya Itifaki ya Umoja wa Sarafu yanaendelea katika ngazi za wataalamu. Vikao saba vimefanyika na jumla ya Ibara 59 za Itifaki hiyo zimejadiliwa. Mambo muhimu ambayo wataalamu wamekubaliana ni pamoja na Nchi mwanachama kujiunga na Umoja wa Sarafu pale tu itakapotimiza vigezo vya kufanya hivyo. Aidha, majadiliano ya Eneo Huru la Biashara la Utatu (COMESA, EAC na SADC) yataanza rasmi mwezi wa Agosti 2012. Kama nilivyoeleza katika hotuba yangu ya mwaka 2011/2012, Soko hili litakuwa ni kubwa lenye jumla ya nchi 26 na idadi ya watu isiyopungua 600 milioni. Jumuiya ya Afrika Mashariki imeamua kuingia katika majadiliano hayo kwa pamoja – Regional Economic Community (REC). Mambo yatakayojadiliwa ni Uasili wa Bidhaa, Uondoshaji wa Vikwazo vya Biashara na Ushirikiano wa Kiforodha.     

Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Bara la Afrika (SADC)


7.             Mheshimiwa Spika, mkutano wa 31 wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini Mwa Afrika ulifanyika tarehe 17 Agosti, 2011 nchini Angola. Mkutano huo ulimchagua Mheshimiwa Jos’e Eduardo do Santos Rais wa Jamhuri ya Angola kuwa mwenyekiti wa jumuiya hiyo. Pia mkutano huo ulimchagua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Ushirikiano wa Siasa, Ulinzi na Usalama. Mkutano huo ulipokea taarifa ya hali ya kisiasa, ulinzi na usalama katika eneo la Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Bara la Afrika. Kwa ujumla, wakuu hao waliridhika na hali hiyo, hata hivyo walisisitiza migogoro ya nchi za Lesotho, Madagascar na Zimbabwe iendelee kutatuliwa. Aidha, mkutano huo ulizungumzia kuhusu maendeleo ya Miundombinu ya Nishati na ikaagiza uharakishaji wa Mpango Mkuu wa Miundombinu katika Nchi za SADC.     

Jumuiya ya Nchi za Ukanda wa Bahari ya Hindi (IOR-ARC)


8.             Mheshimiwa Spika, mkutano wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Nchi za Ukanda wa Bahari ya Hindi (IOR-ARC) unaoshirikisha nchi 19 wanachama wa Jumuiya hiyo ulifanyika nchini India – Bungalore tarehe 15 Novemba 2011. Katika mkutano huo, India iliteuliwa kuwa mwenyekiti na Balozi K.V Bhagirath kutoka India kuwa Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo. Mkutano huo ulizungumzia mambo mbali mbali yakiwemo biashara, uwekezaji, uharamia, taaluma, mashirikiano katika nyanja za Sayansi na teknologia, utamaduni, utalii na kubadilishana utaalamu kwenye maeneo ambayo nchi hizi zina maslahi ya aina moja. Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa jumla zinaweza kufaidika sana na fursa nyingi zilizomo katika Jumuiya ya IOR – ARC hasa katika maeneo ya Utalii na uvuvi.

Wazanzibari Wanaoishi Nje ya Nchi (Diaspora)


9.             Mheshimiwa Spika, Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa na Uratibu wa Shughuli za Wazanzibari wanaoishi nchi za nje imetayarisha Mpango Mkakati wa miaka mitano ambao unatoa muongozo wa utekelezaji wa shughuli zitakazoimarisha na kuwashajihisha Diaspora. Utekelezaji wa mkakati huu, utapelekea upatikanaji wa michango na uekezaji katika sekta za kijamii na kiuchumi kutoka kwa Wazanzibari wanaoishi Nchi za Nje.

10.         Mheshimiwa Spika, katika juhudi za kuwatafuta na kuwashajihisha Wazanzibari wanaoishi Nchi za Nje, Idara imeendelea kuwa karibu na kuwasiliana na Jumuiya mbali mbali za Wazanzibari zikiwemo ZAWA – Uingereza, ZACADIA, ZANCAN za Canada na nyenginezo. Matokeo ya ukaribu na mawasiliano haya yamepelekea Wazanzibari wanaoishi Nchi za Nje kuitikia wito wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kuekeza katika sekta za kijamii, elimu na afya. Kwa mfano ujenzi wa madarasa matano katika skuli ya Unguja Ukuu.

11.         Mheshimiwa Spika, kwa mwaka wa fedha 2012/2013, Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa na Uratibu wa Shughuli za Wazanzibari Wanaoishi Nchi za Nje imekusudia kutekeleza malengo yafuatayo:-

a)       Kuendeleza na kuimarisha juhudi za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kukuza uhusiano mwema na nchi marafiki na Taasisi za Kimataifa.
b)       Kuwawezesha wataalamu wa Zanzibar kushiriki katika mikutano ya kikanda na ya kimataifa.
c)       Kutayarisha Sera ya Diaspora.
d)       Kuaanda mazingira bora yatakayowawezesha Wazanzibari wanaoishi nchi za nje kuweza kuekeza kwa urahisi ndani ya Zanzibar.
e)       Kuanzisha mfumo wa mawasiliano utakaowawezesha wanadiaspora kupeana taarifa mbali mbali.
f)        Kushirikiana kwa karibu na Idara inayoshughulikia Watanzania Waliopo Nje (Diaspora) ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
g)       Kuijengea uwezo Idara pamoja na watendaji wake.
h)       Kuongeza ufanisi kazini ikiwemo kuwapatia watendaji stahili zao.
i)         Kuelimisha masuala mtambuka yanayohusiana na jinsi ya kujikinga na maradhi yenye kuambukiza pamoja na UKIMWI kwa wafanyakazi.

12.         Mheshimiwa Spika, ili Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa na Uratibu wa Shughuli za Wazanzibari Wanaoishi Nchi za Nje iweze kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi, kwa mwaka wa fedha 2012/2013, naliomba Baraza lako Tukufu liidhinishe TZS 884.0 milioni kwa matumizi ya kazi za kawaida.

IDARA YA URATIBU WA TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA


13.         Mheshimiwa Spika, Idara ya Uratibu wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa ina jukumu la kufuatilia na kuratibu uendeshaji wa shughuli zote za Mamlaka ya utawala wa Serikali za Mikoa na Serikali za Mitaa. Aidha, inaratibu, kutoa maelekezo ya kitaalamu na kuzishauri Serikali hizo juu ya utendaji bora wa kazi zao za kila siku sambamba na kusimamia utekelezaji wa shughuli mbali mbali za maendeleo, uwajibikaji na uhusiano bora wa kisekta. Idara hii pia inajukumu la kusimamia utekelezaji wa Sera na Sheria katika mamlaka za Mikoa, Wilaya na Serikali za Mitaa.

14.         Mheshimiwa Spika, Idara ya Uratibu wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, kwa mwaka wa fedha 2011/2012 iliidhinishiwa TZS 200 milioni kwa kazi za kawaida na hadi kufikia mwezi Machi 2012, Idara hii iliingiziwa TZS 114.9 milioni sawa na asilimia 57.5 ya makadirio ya matumizi ya kawaida na kutekeleza yafuatayo:-

a)       Idara kwa kushirikiana na watendaji wa Idara ya Mazingira imefanya ziara katika maeneo ya Muambe, Kangagani na Micheweni kuangalia uharibifu na utunzaji wa Mazingira na kushauri njia bora ya kudhibiti uharibifu wa Mazingira.
b)       Mafunzo na mikutano ya kitaalamu ilifanyika katika Serikali za Mitaa na matokeo yake yameweza kuongeza mapato, udhibiti na usimamizi wa fedha. Mapato ya Serikali za Mitaa yamefikia wastani wa asilimia 102 ya lengo la mwaka.  
c)       Watendaji na Madiwani katika Serikali za Mitaa wameweza kufahamu mipaka ya kazi zao na wajibu wao kwa jamii.
d)       Semina za mafunzo zenye lengo la kuimarisha mahusiano ya kiutendaji kati ya wananchi, Madiwani na watendaji zimefanyika kwa ufanisi na kwa sasa Madiwani na Watendaji wanafanyakazi kwa mashirikiano.
e)       Idara kupitia Mabaraza ya Halmashauri na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu imekamilisha utayarishaji wa Sheria ndogo ndogo za Serikali za Mitaa. Sheria hizo ni pamoja na Kanuni za Madiwani, Kanuni za udhibiti wa wanyama na uzoaji taka.

15.         Mheshimiwa Spika, Serikali inaendelea na azma yake ya kuziendeleza huduma za Mijini kupitia Mradi wa Kuimarisha Huduma za Mjini (ZUSP). Katika kutekeleza hatua ya kwanza na ya pili, Mradi huu umeshatekeleza shughuli zifuatazo:-

a)       Kutafuta mshauri mwelekezi (Consultant) wa usimamizi wa kazi za ukarabati na ujenzi wa misingi ya maji ya mvua kwa ajili ya maandalizi ya kutafuta Mkandarasi wa ujenzi. Maeneo yatakayonufaika na mradi huu ni Ziwa la Sebleni, Ziwa la Mtumwajeni, Ziwa la Kwa-binti Amrani, Ziwa la Mwantenga, Kwamtipura, Kilima hewa, Karakana, Sogea, Mpendae, Jan’gombe (Botanical garden), Uwanja wa Demokrasia na Shauri Moyo.
b)       Serikali imewasilisha ripoti katika Benki ya Dunia kwa ajili ya kuthibitishwa ili hatua za kumtafuta Mjenzi  wa silabu193 za kuweka makontena ya kuwekea taka. Aidha, ripoti ya kutafuta kampuni ya kununua gari za kubebea taka na maji machafu pamoja na taa za barabarani tayari imewasilishwa Benki ya Dunia kwa kuthibitishwa.
c)       Serikali kupitia Mradi wa ZUSP imenunua baadhi ya vifaa na tayari vimeshafika Zanzibar na vengine vinatarajiwa kufika hivi karibu; vitu hivyo ni gari 5 za wakuu wa Idara za Manispaa, Vespa 10 za Manispaa, Vespa 15 na gari 6 za kubebea  taka  kwa ajili ya Mabaraza ya Miji Pemba, Honda 3, gari moja ya Idara ya Mipango Miji na gari moja ya Idara ya Uratibu wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa.
d)       Serikali imeshatayarisha hadudi rejea za kumtafuta mshauri wa kusimamia uwekaji wa taa za barabarani na zimeshawasilishwa Benki ya Dunia kwa kuthibitishwa. Maeneo yatakayonufaika kutokana na mpango huu ni Mwanakwerekwe hadi Amani, Amani hadi Mwembeladu, Magomeni hadi Kariakoo, Kikwajuni hadi Baraza la Wawakilishi la zamani, Barabara ya Mazizini lilipo jengo la Bodi ya Mapato ya Zanzibar, maeneo ya Kiponda, Shangani na Mkunazini.
e)       Serikali imeshatayarisha hadudi rejea za kumtafuta mjenzi wa utanuzi wa ukuta unaopita pembezoni mwa pwani ya Forodhani na zimeshawasilishwa Benki ya Dunia kwa kuthibitishwa.

16.         Mheshimiwa Spika, kwa mwaka wa fedha 2012/2013, Idara ya Uratibu wa  Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa imekusudia kutekeleza malengo yafuatayo:-

a)       Kuimarisha Uratibu  wa Serikali za Mikoa, Wilaya na Serikali za Mitaa Pamoja na kuimarisha ushirikiano na TAMISEMI Tanzania Bara
b)       Kusimamia utekelezaji wa Sera ya Serikali za Mitaa itakayowezesha ushirikishaji wa wananchi.
c)       Kuongeza ufanisi kazini ikiwemo kuwapatia wafanyakazi stahili zao, kununua vitendea kazi vya kisasa na samani.
d)       Kufanya uchambuzi wa ripoti za utekelezaji wa Taasisi za Serikali za Mitaa.
e)       Kuwajengea uwezo watumishi kwa kuwapatia mafunzo ya muda mrefu na mfupi kwa maafisa watano katika fani za mipango, utawala bora, utawala na rasilimali watu.

17.         Mheshimiwa Spika, pamoja na kupanga kutekeleza malengo niliyoyataja hapo juu, Idara ya Uratibu wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa itaratibu kwa karibu utekelezaji wa Mradi wa ZUSP. Shughuli zitakazotekelezwa kwa mwaka wa fedha 2012/2013 ni kama ifuatavyo:-

a)        Kufanya matengenezo ya ujenzi wa misingi ya maji ya mvua yenye urefu wa mita 3,339 katika maeneo ya Uwanja wa Mnazi Mmoja, Magogoni, Amani, Sebleni na Sogea.
b)        Ujenzi wa silabu 78 za kuwekea taka katika maeneo ya Mji Mkongwe na Ng’ambo.
c)        Matengenezo na uwekaji wa taa za barabarani katika maeneo ya mjini yakiwemo maeneo ya mji Mkongwe.
d)        Kutafuta taarifa muhimu na kufanya tathmini ya taarifa za vyanzo vya mapato, miundo ya utumishi, kanuni na sheria ziliopo kwa ajili ya kupendekeza na kutoa mikakati ya utekelezaji kwa lengo la kuinua uwezo wa utendaji wa Baraza la Manispaa (Institutional strengthening).
e)        Kufanya Ubunifu (structural design) na tathmini ya gharama za ujenzi wa utanuzi wa ukuta wa pwani ya Forodhani wenye urefu wa mita 340 kwa ajili ya matayarisho ya vitabu vya zabuni ya kumtafuta mkandarasi wa ujenzi.
f)          Kuibua miradi midogo midogo na kuifanyia tathmini na kutayarisha vitabu vya zabuni ya kutafuta mkandarasi na kuandaa mpango wa utekelezaji wa miradi hiyo kwa Mabaraza ya Miji ya Pemba. 

18.         Mheshimiwa Spika, ili Idara ya Uratibu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa iweze kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi, kwa mwaka wa fedha 2012/2013, naliomba Baraza lako Tukufu liidhinishe TZS 1,992.4 milioni. Kati ya hizo TZS 701.4 milioni kwa matumizi ya kazi za kawaida zikijumuisha TZS 255 milioni kwa ajili ya ruzuku za Halmashauri za Wilaya za Unguja. Aidha, ruzuku ya Baraza la Manispaa ni TZS 1,291 milioni.

MAMLAKA ZA SERIKALI ZA MIKOA


19.         Mheshimiwa Spika, Mamlaka za Serikali za Mikoa zina jukumu la kuratibu na kusimamia utekelezaji wa shughuli za Serikali katika maeneo hayo ikiwa ni pamoja na kutoa miongozo, kutafsiri sera, sheria pamoja na kuratibu amani na utulivu.

MKOA WA MJINI MAGHARIBI


20.         Mheshimiwa Spika, Mkoa wa Mjini Magharibi, kwa mwaka wa fedha 2011/2012 uliidhinishiwa TZS 744 milioni kwa matumizi ya kawaida na hadi kufikia mwezi Machi 2012, Mkoa huu uliingiziwa TZS 637 milioni sawa na asilimia 85.6 ya makadirio ya matumizi na kutekeleza yafuatayo:-

a)       Kupitia kamati za Ulinzi na Usalama za Mkoa, Wilaya na Shehia, Mkoa ulisimamia hali ya ulinzi na usalama kwa kufuatilia matukio mbali mbali yaliyoripotiwa, kutoa elimu kwa wananchi juu ya suala la ulinzi na usalama.
b)       Mkoa kwa kushirikiana na sekta mbali mbali umefanikisha kampeni za chanjo kwa watoto, zoezi la upigaji dawa majumbani, ugawaji wa vyandarua, uandikishaji wa watoto waliofikia umri wa kuanza skuli, ujenzi  wa madarasa mapya, kufanikisha mazingira mazuri ya mitihani ya Kitaifa, uhamasishaji wa kilimo cha mazao ya biashara na matunda. Aidha, umesimamia ugawaji wa misaada ya wazee wasiojiweza ambapo jumla ya wazee 2,071 wamepatiwa misaada hiyo. Kati ya hao 1,619 kutoka Wilaya ya Mjini na 452 kutoka Wilaya ya Magharibi. Mkoa umeshiriki kampeni za kupiga vita udhalilishaji wa wanawake na watoto. Jumla vijana 4,159 wameorodheshwa na Mkoa kwa lengo la kuwatafutia ajira, kati ya hao wanaume ni 2,328 na wanawake ni 1,831.
c)       Wafanyakazi 12 wamepatiwa elimu katika ngazi ya stashahada ya uzamili, stashahada na cheti kwa fani za utawala wa umma, utunzaji wa kumbukumbu, uhandisi wa magari na uhasibu.
d)       Jumla ya kamati 37 za maendeleo za Shehia zimepatiwa mafunzo ya uandaaji wa mipango na usimamizi wa fedha za miradi. Pia Masheha 72 wamepatiwa mafunzo ya utawala bora.
e)       Wafanyakazi 29 na Masheha 28 wamepatiwa mafunzo ya uelewa wa usawa wa jinsia. Wafanyakazi 36 na Shehia 27 wamepatiwa mafunzo ya UKIMWI na unyanyapaa. Aidha, ziara zimefanyika  kufuatilia uharibifu wa mazingira  pamoja na kufanya vikao kwa kushirikiana na wadau wengine wakiwemo Bazara la Manispaa na Halmashauri ya Wilaya ya Magharibi  kuzungumzia usafi wa mji na uzururaji wa wanyama.
f)        Mkoa umeratibu na kusimamia miradi mbali mbali inayoanzishwa na wananchi na kuona utekelezaji wake. Kiambatanisho Namba 7 kinatoa ufafanuzi wa miradi iliyotekelezwa.

21.         Mheshimiwa Spika, kwa mwaka wa fedha 2012/2013, Mkoa wa Mjini Magharibi umekusudia kutekeleza malengo yafuatayo:-

a)       Kuratibu na kusimamia utekelezaji wa malengo ya sekta mbali mbali.
b)       Kuratibu na kusimamia shughuli za ulinzi na usalama.
c)       Kutatua migogoro ya ardhi inayoukabili Mkoa kuanzia ngazi ya Shehia, Halmashauri, Baraza la Manispaa, Wilaya na Mkoa pamoja na kushirikiana na Wizara husika.
d) Kusimamia uimarishaji wa usafi wa mji, udhibiti wa wanyama wanaozurura na udhibiti wa uchimbaji holela wa mchanga. Shughuli hizi zitafanywa kwa kushirikiana na Baraza la Manispaa pamoja na Halmashauri ya Wilaya ya Magharibi.
e)       Kuanza matayarisho ya ujenzi wa jengo jipya la Ofisi za Mkoa lilopo Amani na kufanya matengenezo ya jengo la Ofisi za Mkoa Vuga.
f)        Kuanza matayarisho ya ujenzi wa jengo la Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Magharibi
g)       Kuratibu na kusimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya wananchi.
h)       Kuzijengea uwezo Kamati mbalimbali zinazosimamia maendeleo ya Shehia.
i)         Kuongeza ufanisi kazini ikiwemo kuwapatia wafanyakazi stahili zao, kununua vitendea kazi vya kisasa na samani.
j)         Kutoa elimu ya kujikinga na maambukizi mapya ya UKIMWI, utunzaji wa mazingira na usawa wa jinsia.

22.         Mheshimiwa Spika, ili Mkoa wa Mijini Magharibi uweze kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi, kwa mwaka wa fedha 2012/2013, naliomba Baraza lako Tukufu liidhinishe TZS 1,099 milioni kwa matumizi ya kazi za kawaida.

MKOA WA KASKAZINI UNGUJA


23.         Mheshimiwa Spika, Mkoa wa Kaskazini Unguja, kwa mwaka wa fedha 2011/2012 uliidhinishiwa TZS 774 milioni kwa kazi za kawaida na TZS 60 milioni kwa matumizi ya kazi za maendeleo na hadi kufikia mwezi Machi 2012, Mkoa huu uliingiziwa TZS 711.8 milioni sawa na asilimia 92 ya makadirio ya matumizi ya kawaida na TZS 60 milioni sawa na asilimia 100 ya kazi za maendeleo na kutekeleza yafuatayo:-

a)       Umesimamia shughuli za ulinzi na usalama kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama vilivyomo Mkoani.
b)       Mkoa umeendelea na ujenzi wa Ofisi ya Mkoa
c)       Mkoa umefanya utafiti juu ya sababu zinazopelekea vitendo vya ubakaji na unyanyasaji wa kijinsia. Ambapo utafiti umebainisha kuwa vijana kushiriki katika vikundi hatarishi na utumiaji wa madawa ya kulevya ni chanzo kikuu cha ubakaji na unyanyasaji kijinsia.
d)       Kwa kushirikiana na Ofisi za kilimo za Mkoa na Wilaya, Mkoa uliwashajihisha wananchi kulima kilimo cha juu na mabondeni kwa mazao ya chakula na biashara ili kuhakikisha uhakika wa chakula, kuongeza kipato na kupunguza umasikini. Hadi kufikia mwezi Machi, 2012 Mkoa umelima jumla ya ekari 22,229 sawa na asilimia 37.25 ya lengo, kati ya hizo ekari 6,429 za mpunga, kilimo cha juu ekari 15,800 na kilimo cha maweni ni ekari 21,351.
e)       Kwa upande wa mazao ya biashara, misitu na matunda, hadi kufikia mwezi Machi, 2012 Mkoa umeweza kuatika jumla ya miche 239,000 sawa na asilimia 77.59. Kati ya hiyo, mikarafuu 62,000, miche ya misitu ni jumla 99,000 na miche ya mazao ya matunda na biashara ni miche 78,000.
f)        Mkoa umeshajihisha viongozi na wananchi kujenga jumla ya madarasa 39 na kutoa elimu kwa Wazazi jinsi ya kuondoa tatizo la kutofaulu kwa wanafunzi.
g)       Mkoa umewashajihisha wananchi juu ya umuhimu wa usafi wa mazingira, chanjo za watoto, kujikinga na malaria. Pia usimamizi na ushajihishaji wa uvuvi, upatikanaji wa maji safi na salama, utawala bora ulifanyika kwa mafanikio makubwa.
h)       Mkoa ulisimamia matayarisho ya kuanza ujenzi wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini “A” Unguja kwa kununua kiwanja na kukisafisha.
i)         Mkoa ulikarabati nyumba ya Mkuu wa Mkoa kwa kuezeka paa jipya, ukarabati wa madirisha na miundombinu ya umeme.
j)         Jumla ya wafanyakazi 8 walijengewa uwezo kwa viwango tofauti katika fani za Kompyuta wafanyakazi wawili, Utawala (cheti) mfanyakazi mmoja, Utawala (Diploma) wafanyakazi watatu, Mipango (PG) mfanyakazi mmoja na Shahada ya kwanza mfanyakazi mmoja.
k)       Umetoa elimu ya kijikinga na maambukizi mapya ya UKIMWI na uelewa wa jinsia

24.         Mheshimiwa Spika, kwa mwaka wa fedha 2012/2013, Mkoa wa Kaskazini Unguja umekusudia kutekeleza malengo yafuatayo:-

a)       Kusimamia shughuli za Ulinzi na Usalama.
b)       Ukamilishaji wa ujenzi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na kuanza ujenzi wa Ofisi za Wakuu wa Wilaya
c)       Kuandaa Mpango kazi wa Mkoa
d)       Kuendeleza juhudi za kupunguza migogoro ya ardhi kwa kushirikiana na  wizara husika pamoja na wadau wengine zikiwemo Halmashauri za wilaya na jamii yenyewe.
e)       Kuratibu na kusimamia miradi ya maendeleo.
f)        Kuratibu na kusimamia malengo ya sekta mbali mbali.
g)       Kuongeza ufanisi kazini ikiwemo kuwapatia wafanyakazi stahili zao, kununua vitendea kazi vya kisasa na samani.
h)       Kuwajengea uwezo wafanyakazi 10 kwa kuwapeleka masomoni katika ngazi za cheti na Stashahada  katika fani za Mipango Vijijini na Utawala na  Uendeshaji  
i)         Kuratibu shughuli mtambuka ikiwemo Ukimwi na jinsia.

25.         Mheshimiwa Spika, ili Ofisi ya Mkoa wa Kaskazini Unguja iweze kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi, kwa mwaka wa fedha 2012/2013, naliomba Baraza lako Tukufu liidhinishe TZS 1,083 milioni kwa matumizi ya kazi za kawaida.

MKOA WA KUSINI UNGUJA


26.         Mheshimiwa Spika, Mkoa wa Kusini Unguja, kwa mwaka wa fedha 2011/2012 uliidhinishiwa TZS 761 milioni kwa kazi za kawaida na  TZS 20 milioni kwa matumizi ya kazi za maendeleo na hadi kufikia mwezi Machi 2012, Mkoa huu uliingiziwa TZS 642.3 milioni sawa na asilimia 84.4 ya makadirio ya matumizi ya kawaida na TZS 20 milioni sawa na asilimia 100 kwa kazi za maendeleo na kutekeleza yafuatayo:-

a)       Mkoa kwa kushirikiana na Kamati za ulinzi na usalama umeweka hali ya utulivu na amani kwa kuwashajihisha wananchi kuunda Kamati za Polisi shirikishi jamii ambapo Shehia zote 61 za Mkoa zimeshaunda Kamati hizo. Aidha, jumla ya vikao 36 vya ulinzi na usalama vilifanyika.
b)       Mkoa  kwa mashirikiano na Wilaya zake umeratibu na kusimamia utekelezaji wa sekta mbali mbali kama vile ujenzi wa ukumbi wa skuli ya Sekondari ya Makunduchi, ukamilishaji wa ujenzi wa nyumba ya walimu Charawe kwa kiwango cha uezekaji, umalizaji wa nyumba za madaktari, ukamilishaji wa majengo ya madarasa matano kwa skuli za Kidimni, Miwaleni,  Unguja Ukuu Msingi, Kiboje na Ndijani Mseweni kwa hatua ya utiwaji plasta pamoja na umaliziaji wa ujenzi wa skuli za Mwera Sekondari, Ubago, Mtende Sekondari na Jumbi.
c)       Mkoa umeratibu zoezi la Kampeni ya Kitaifa ya utoaji wa chanjo kwa watoto 17,340 chini ya umri wa miaka mitano, zoezi la utoaji wa vyandarua 56,888 na upigaji wa dawa ya malaria katika nyumba 20,252.
d)       Umewapatia Masheha 61 mafunzo ya utawala bora kwa kuendesha semina ili kuongeza uwajibikaji na utoaji wa huduma kwa jamii.
e)       Mkoa umeweza kukamilisha ujenzi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kwa kiwango cha utiaji wa rangi, shata na viyoo vya madirisha, feni, viyoyozi kwa baadhi ya vyumba pamoja na mageti ya nje.
f)        Umefanya matengenezo madogo madogo Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kusini kwa kutia rangi.
g)       Umeanza matayarisho ya ujenzi wa Ofisi mpya ya Mkuu wa Wilaya ya Kati ambapo hatua ya kupata hati miliki na kusafishwa eneo imekamilika.
h)       Wafanyakazi wanne wa Mkoa wanaendelea kupatiwa mafunzo katika ngazi ya cheti, Diploma na Shahada ya pili ndani ya nchi katika fani za usimamizi wa ofisi na Utawala.
i)         Mkoa kwa kushirikiana na Wilaya zake umewapatia wafanyakazi wake semina juu ya kujikinga na maambukizi mapya ya UKIMWI. Jumla ya wafanyakazi 113 wamepatiwa mafunzo hayo.
j)         Mkoa kwa kushirikiana na maafisa husika umehamasisha miradi mbali mbali ikiwemo ya kijamii na vikundi ili kuwa endelevu. Jumla ya miradi 25 ya Mkoa imefanyiwa ukaguzi ikiwemo miradi ya kilimo, ufugaji, vyama vya ushirika (SACCOS), wajasiriamali na wakulima wa mwani.

27.         Mheshimiwa Spika, kwa mwaka wa fedha 2012/2013, Mkoa wa Kusini Unguja umekusudia kutekeleza malengo yafuatayo:-

a)       Kuratibu na kusimamia shughuli za ulinzi na usalama.
b)       Kuratibu na kusimamia utekelezaji wa malengo ya sekta mbali mbali zilizomo ndani ya Mkoa  kama vile sekta ya elimu, kilimo, afya, utawala bora, maji safi na salama, uvuvi, miundombinu, ustawi wa jamii, ufugaji, vijana, wanawake na watoto na maendeleo ya kijamii na kiuchumi.
c)       Kuratibu na kusimamia miradi ya wananchi
d)       Kuanza ujenzi wa msingi wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kati.
e)       Kuendelea na ujenzi wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kusini kwa kutia vigae na samani za Ofisi.
f)        Kumaliza ujenzi wa Uzio wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja na kuweka vigae vya sakafu.
g)       Kuwapatia mafunzo wafanyakazi 6 ngazi ya Cheti, Stashahada, Shahada ya kwanza, Shahada ya pili na Stashahada ya uzamili katika fani za utunzaji wa kumbukumbu, utawala na uongozi.
h)       Kuongeza ufanisi kazini ikiwemo kuwapatia wafanyakazi stahili zao, kununua vitendea kazi vya kisasa na samani.
i)         Kuratibu na kusimamia utekelezaji wa shughuli mtambuka zikiwemo, UKIMWI, jinsia, madawa ya kulevya na ajira za watoto.

28.         Mheshimiwa Spika, ili Ofisi ya Mkoa wa Kusini Unguja iweze kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi, kwa mwaka wa fedha 2012/2013, naliomba Baraza lako Tukufu liidhinishe TZS 1,064 milioni kwa matumizi ya kazi za kawaida.

 

MKOA WA KUSINI PEMBA


29.         Mheshimiwa Spika, Mkoa wa Kusini Pemba, kwa mwaka wa fedha 2011/2012 uliidhinishiwa TZS 1,164 milioni kwa kazi za kawaida na hadi kufikia mwezi Machi 2012, Mkoa huu uliingiziwa TZS 886 milioni sawa na asilimia 76 ya makadirio ya matumizi ya kawaida na kutekeleza yafuatayo:-.

a)       Umeendelea kusimamia amani, umoja na mshikamano miongoni mwa wananchi pamoja na kudumisha utulivu, ulinzi na usalama wa raia na mali zao.
b)       Umeratibu utekelezaji wa shughuli za sekta mbali mbali ikiwemo sekta ya kilimo, elimu, afya, maji safi na salama, miundombinu, utawala bora, umeme, ustawi wa jamii, maendeleo ya vijana, wanawake na watoto, uvuvi, ufugaji, maendeleo ya kijamii na kiuchumi.
c)       Kuendelea na ujenzi wa jengo la Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na ujenzi wa uzio wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Mkoani.
d)       Jumla ya wafanyakazi 14 wa Mkoa na Wilaya zake wanaendelea na mafunzo katika ngazi za Cheti na Stashahada katika fani ya Uongozi wa Rasilimali Watu, Utawala na Biashara.
e)       Jumla ya wafanyakazi 77 wa Mkoa na Wilaya zake wamefanyiwa semina juu ya kupambana na UKIMWI na Madawa ya kulevya.

30.         Mheshimiwa Spika, kwa mwaka wa fedha 2012/2013, Mkoa wa Kusini Pemba imekusudia kutekeleza malengo yafuatayo:-

a)       Kuendelea kusimamia amani, umoja na mshikamano miongoni mwa wananchi pamoja na kudumisha utulivu, ulinzi na usalama wa raia na mali zao
b)       Kuratibu na kusimamia utekelezaji wa malengo ya sekta mbali mbali zilizomo ndani ya Mkoa  kama vile sekta ya elimu, kilimo, afya, utawala bora, maji safi na salama, uvuvi, miundombinu, ustawi wa jamii, ufugaji, vijana, wanawake na watoto na maendeleo ya kijamii na kiuchumi.
c)       Kujenga nyumba ya Mkuu wa Mkoa, kuanza matayarisho ya ujenzi wa jengo la Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Chake Chake na kununua jengo kwa ajili ya Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mkoani.
d)       Kuratibu shughuli za utekelezaji wa sekta mtambuka zikiwemo UKIMWI, jinsia, madawa ya kulevya na viashiria vya idadi ya watu.
e)       Kuongeza ufanisi kazini ikiwemo kuwapatia wafanyakazi stahili zao, kununua vitendea kazi vya kisasa na samani.
f)        Kuwajengea uwezo wafanyakazi 6 kwa kuwapatia taaluma katika ngazi tofauti, Cheti katika fani  ya  utunzaji wa kumbukumbu, Stashada ya  uhasibu, Manunuzi, Utawala na  Uongozi na Shahada ya  kwanza katika fani ya  Uandishi wa habari.

31.         Mheshimiwa Spika, ili Mkoa wa Kusini Pemba uweze kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi, kwa mwaka wa fedha 2012/2013, naliomba Baraza lako Tukufu liidhinishe TZS 1,741 milioni. Kati ya hizo TZS 1,169 milioni kwa matumizi ya kazi za kawaida na TZS 572 milioni kwa ajili ya ruzuku za Baraza la Mji la Mkoani na Chake Chake.

 

MKOA KASKAZINI PEMBA


32.         Mheshimiwa Spika, Mkoa wa Kaskazini Pemba, kwa mwaka wa fedha 2011/2012 uliidhinishiwa TZS 950 milioni kwa matumizi ya kawaida na hadi kufikia mwezi Machi 2012, Mkoa huu uliingiziwa TZS 793 milioni sawa na asilimia 83.5 ya makadirio ya matumizi ya kazi za kawaida na kutekeleza yafuatayo:-

a)       Umesimamia amani, umoja na mshikamano miongoni mwa wananchi pamoja na kudumisha utulivu, ulinzi na usalama wa raia na mali zao.
b)       Umeratibu na kusimamia kwa ufanisi utekelezaji wa sekta mbali mbali zinazoratibiwa na Mkoa ikiwemo, elimu, afya, maji safi, miundombinu, ufugaji, uvuvi, ustawi wa jamii na maendeleo ya kiuchumi.
c)       Umeweza kuratibu na kusimamia miradi mbali mbali ya maendeleo.
d)       Umewajengea uwezo wafanyakazi 5 katika fani za uhasibu, usimamizi wa biashara, rasilimali watu na sayansi ya jamii katika ngazi ya stashahada
e)       Umehamasisha jamii juu ya masuala ya UKIMWI na jinsia kwa wafanyakazi na Masheha. Aidha, Mkoa umehamasisha NGOs zinazojihusisha na utowaji wa elimu ya UKIMWI kuendelea kuishajihisha jamii kujikinga na maambukizi mapya na kupunguza unyanyapaa ndani ya jamii.
f)        Ofisi ya Mkuu wa Mkoa imefanyiwa matengenezo na ununuzi wa vitendea kazi vikiwemo Vespa moja na kompyuta mbili.

33.         Mheshimiwa Spika, kwa mwaka wa fedha 2012/2013, Mkoa wa Kaskazini Pemba imekusudia kutekeleza malengo yafuatayo:-

a)       Kuratibu na kusimamia shughuli za ulinzi na usalama katika Mkoa.
b)       Kuratibu na kusimamia utekelezaji wa Malengo ya Sekta mbali mbali zikiwemo ya elimu, afya, kilimo, maliasili na mifugo, maendeleo ya jamii na mazingira
c)       Kuratibu na kusimamia miradi mbali mbali ya maendeleo ya wananchi
d)       Kufanya matengenezo ya nyumba za Mkuu wa Mkoa na Wakuu wa Wilaya na Ofisi za Wilaya.
e)       Kuratibu ziara za viongozi wa Kitaifa na Kimataifa wanaotembelea katika Mkoa
f)        Kuendelea kuwapatia mafunzo wafanyakazi 11 wa Ofisi ya Mkoa na Wilaya zake katika ngazi ya Shahada ya kwanza, Stashahada na Cheti katika fani za Usimamizi wa biashara, utawala na uendeshaji, Teknohama, utunzaji wa kumbukumbu, rasilimali watu na uhasibu.
g)       Kuratibu na kuhamasisha jamii juu ya masuala mtambuka yakiwemo UKIMWI, jinsia na madawa ya kulevya.
h)       Kuongeza ufanisi kazini ikiwemo kuwapatia wafanyakazi stahili zao, kununua vitendea kazi vya kisasa na samani.

34.         Mheshimiwa Spika, ili Mkoa wa Kaskazini Pemba uweze kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi, kwa mwaka wa fedha 2012/2013, naliomba Baraza lako Tukufu liidhinishe TZS 1,384 milioni. Kati ya hizo TZS 1,109 milioni kwa matumizi ya kazi za kawaida na TZS 275 milioni kwa ajili ya ruzuku za Baraza la Mji la Wete.

MAMLAKA ZA SERIKALI ZA MITAA


35.         Mheshimiwa Spika, Mamlaka za Serikali za Mitaa zimenzishwa kwa Sheria namba 3 na 4 za mwaka 2004 ya Baraza la Wawakilishi kwa lengo la kutoa huduma kwa wananchi, Mamlaka hizi zinajumuisha Baraza la Manispaa, Mabaraza ya Miji pamoja na Halmashauri za Wilaya. Mbali na majukumu mengine ya msingi, Mamlaka hizi ziliweka kipaumbele katika kukusanya mapato kutoka katika vyanzo vyao. Takwimu za makadirio ya makusanyo ya mapato katika Serikali za Mitaa zinaonyesha matumaini makubwa. Wastani wa makusanyo umevuka lengo. Angalia Kiambatanisho Namba 15 kwa ufafanuzi zaidi.



BARAZA LA MANISPAA


36.         Mheshimiwa Spika, Baraza la Manispaa, kwa mwaka wa fedha 2011/2012 liliidhinishiwa TZS 1,041 milioni kwa ajili ya ruzuku na lililenga kukusanya TZS 1,094.9 kupitia vyanzo vyake vya mapato. Hadi kufikia mwezi Machi 2012, Baraza liliingiziwa TZS 887.7 milioni sawa na asilimia 85.3 kwa ajili ya ruzuku na limekusanya TZS 987 milioni sawa na asilimia 90.1 na kutekeleza yafuatayo:-

a)       Limekusanya na kuzoa taka wastani tani 25,920 sawa na asilimia 45 ya taka zote zinazozalishwa mjini
b)       Limesafisha barabara kuu za Mjini kwa kutumia vikundi vya mazingira. Barabara hizo ni pamoja na Mnazimmoja-Uwanja wa ndege, Kiembesamaki-Amani, Amani-Kwa Biziredi, Gulioni-Kilimani na barabara zote za ndani za mji Mkongwe.
c)       Limeziba paa kwa kutiwa zege Soko la Mwanakwerekwe katika sehemu zilizokuwa zinavuja. Aidha, limerejeshewa huduma ya maji safi kwa kuwekewa mashine moja ya maji katika soko la Mombasa ili kutoa huduma ya maji katika soko hilo. Pia, limeimarisha soko la Mikunguni kwa kuweka huduma za maji safi na matengenezo ya paa.
d)       Baraza limekamilisha michoro ya ujenzi wa Ofisi ya Mapato Darajani na kibali cha ujenzi kimeshapatikana kutoka Mji Mkongwe.
e)       Limekamilisha kazi za ujenzi wa msingi wenye urefu wa mita 160 pamoja na uwekaji wa taa katika eneo la kituo cha biashara Saateni.
f)        Limechangia miradi midogo midogo ya maendeleo ya wananchi katika Wadi zote  zilizomo ndani ya Manispaa ya Zanzibar kwa lengo la kupunguza kero za jamii kwa kuchangia vifaa vya upatikanaji wa maji safi, ujenzi wa madarasa ya Skuli na ujenzi wa vyoo
g)       Limefanya matengenezo madogo katika msingi wa maji machafu wa Mpendae na wa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui pamoja na matengenezo ya msingi wa Kwamtipura.
h)       Limewajengea uwezo wafanyakazi wake kwa kuwapatia mafunzo ya muda mfupi wafanyakazi sita katika fani ya ukaguzi wa hesabu za ndani, mabadiliko ya tabia nchi, usafi wa Mji pamoja na ukaguzi na usimamizi wa Masoko.
i)         Limeendelea na zoezi la ukamataji wa wanyama wanaozurura ovyo ndani ya Mji. Jumla ya wanyama 35 wamekamatwa na kutozwa faini na gharama za kugomboa zenye thamani ya TZS 2.3 milioni.

37.         Mheshimiwa Spika, kwa mwaka wa fedha 2012/2013, Baraza la Manispaa limekusudia kutekeleza malengo yafuatayo:-

a)       Kukusanya mapato yatakayofikia Jumla ya TZS 1,874 milioni kutoka katika vyanzo vyake vya mapato na TZS 1,291 ruzuku kutoka Serikali Kuu
b)       Kujenga na kuezeka paa, kutia rangi pamoja na kutengeneza kuta katika soko la Mwanakwerekwe
c)       Kufanya matengenezo ya misingi na kuimarisha huduma za maji safi katika soko la Darajani, Mombasa na Mikunguni.
d)       Kuendeleza ujenzi wa jengo la Ofisi ya mapato Darajani kwa kujenga ghorofa moja
e)       Kuendeleza ujenzi wa jengo la Ofisi ya Funguni
f)        Kujenga misingi ya maji ya mvua, uwekaji wa mabomba ya maji safi na umeme, ujenzi wa uzio pamoja na kituo kidogo cha polisi katika kituo cha biashara cha Manispaa kilichopo Saateni.
g)       Kufanya matengenezo ya maegesho ya magari Darajani.
h)       Uendelezaji wa bustani za ndani ya Manispaa ya Zanzibar (Bustani za Mjini)
i)         Kuchangia miradi midogo midogo ya Maendeleo ya Wadi 20 zilizomo ndani ya Manispaa ya Zanzibar.
j)         Kuimarisha na kuitunza michirizi ya maji machafu na mvua katika Manispaa ya Mji wa Zanzibar.
k)       Kuwajengea uwezo wa kitaaluma wafanyakazi wake saba katika fani za udereva, mafundi magari, maafisa usafirishaji na ukaguzi wa hesabu.
l)         Kutekeleza mkakati mpya wa uzoaji taka na uondoaji wa wanyama wanaozurura ovyo  ndani ya eneo la Manispaa ya Zanzibar na vitongoji vyake kwa kushajihisha vikundi vya mazingira katika Wadi zote 24 kwa kushirikiana na Madiwani na Masheha
m)     Kutafuta eneo jipya la kutupia taka lenye ukubwa wa zaidi ya hekta 15.
n)       Kuimarisha na kuendeleza huduma ya Taa za Barabarani Mjini na kulipia gharama za umeme.
o)       Kugharamia matumizi ya maji safi katika masoko na Ofisi zote za Baraza la Manispaa, bustani, pamoja na Karakana ya gari, Saateni   
p)       Kuhakikisha maslahi ya wafanyakazi yanapatikana kwa mujibu wa sheria na kwa wakati ili kuimarisha ufanisi kazini.

38.         Mheshimiwa Spika, ili Baraza la Manispaa liweze kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi, kwa mwaka wa fedha 2012/2013, naliomba Baraza lako Tukufu liidhinishe TZS 1,291 milioni kwa ajili ya ruzuku.

 

HALMASHAURI YA WILAYA YA MAGHARIBI


39.         Mheshimiwa Spika, Halmashauri ya Wilaya ya Magharibi, kwa mwaka wa fedha 2011/2012 ililenga kukusanya TZS 400 milioni kupitia vyanzo vyake vya mapato na hadi kufikia mwezi Machi 2012, ilikusanya TZS 570.1 milioni sawa na asilimia 143.0 na kutekeleza yafuatayo:-

a)       Imeendelea na ujenzi wa jengo la Ofisi ya Halmashauri Mombasa
b)       Halmashauri imejenga Silabu mbili za kuhifadhia taka katika maeneo ya Pangawe na Jumba la Benki - Mwanakwerekwe.
c)       Imekusanya na kuzoa taka wastani tani 24,958.
d)       Imenunua gari ya ukaguzi.
e)       Imeendelea na ujenzi wa jengo la Hospitali Mbuzini.
f)        Imenunua mashine ya kutengenezea Matofali  kwa ajili ya miradi ya wananchi.
g)       Imesaidia utekelezaji wa miradi 16 ya Maendeleo ya wananchi katika Wadi zao (Kiambatanisho Namba 8 kinatoa ufafanuzi zaidi).

40.         Mheshimiwa Spika, Halmashauri ya Wilaya ya Magharibi, kwa mwaka wa fedha 2012/2013, imekusudia kutekeleza malengo yafuatayo:-

a)       Kukusanya TZS 480.7 milioni kutoka katika vyanzo vyake vya mapato
b)       Kuendeleza mradi wa usafi wa mazingira
c)       Uendelezaji wa ujenzi wa Hospitali Mbuzini kwa kutia sakafu, dari, milango, madirisha na kupiga plasta.
d)       Kununua mashine ya kuchanganya mchanga na saruji kwa ajili ya utengenezaji wa matofali ya kujengea miradi ya maendeleo.
e)       Kusaidia miradi 16 ya wananchi kupitia Wadi zao

HALMASHAURI YA WILAYA KASKAZINI ‘A’


41.            Mheshimiwa Spika, Halmashauri ya Wilaya Kaskazini ‘A’ Unguja, kwa mwaka wa fedha 2011/2012, ililenga kukusanya TZS 189.7 milioni kutokana na vyanzo vyake vya mapato na hadi kufikia mwezi Machi 2012, Halmashauri imekusanya TZS 144.4 milioni sawa na asilimia 76.1. Kati ya hizo, TZS 59.7 milioni zilitumika kwa kazi za kawaida na TZS 78.9 milioni zilitumika kwa kazi za maendeleo na kutekeleza yafuatayo:-

a)       Imefanya matengenezo ya jengo la Makao Makuu ya Ofisi ya Halmashauri Mkokotoni kwa kuweka mlango wa chuma Ofisi ya Mhasibu na kupiga plasta.
b)       Imefanya matengenezo ya jengo la Skuli ya Msingi Chaani, Skuli ya Msingi Matemwe, Skuli ya Maandalizi Kikongeni.
c)       Imefanya ujenzi wa madarasa manne ya Skuli ya Msingi Kinyasini na Ofisi za walimu.
d)       Imefanya ujenzi wa msingi wa madarasa manne ya Skuli ya Kandwi na ujenzi wa Skuli ya Msingi Moga.
e)       Imefanya ujenzi wa visima viwili Tumbatu Gomani na imefanya ununuzi wa mipira ya maji kwa ajili ya Changani Mnarani.
f)        Imesaidia gharama za mafunzo kwa wafanyakazi watatu wanaosoma Chuo Cha Utawala wa Umma ngazi ya cheti katika fani za Uhasibu, Katibu Muhtasi na masjala.
g)       Halmashauri imeandaa michoro ya masoko ya Kinyasini, Mkwajuni, Bwekunduni, Mkokotoni na Soko la Vinyago Pwani Mchangani.
h)       Imesaidia usambazaji wa maji katika Wadi ya Muwange, uwekaji wa kifusi katika njia ndogo za Chaani Mtakuja, Kinyasini Ziwani na Bwekunduni. Aidha, imejenga maduka ya wafanyabiashara Pwani Mchangani.

42.         Mheshimiwa Spika, kwa mwaka wa fedha 2012/13, Halmashauri ya Wilaya ya Kaskazini ‘A’ imelenga kutekeleza malengo yafuatayo:-

a)       Kukusanya TZS 205.3 milioni kutoka katika vyanzo vyake vya mapato.
b)       Kuendeleza ujenzi wa Ofisi ya Halmashauri – Mkokotoni.
c)       Kuanza ujenzi kituo kidogo cha Halmashauri – Nungwi.
d)       Kusaidia ujenzi wa maktaba Skuli ya Sekondari – Jongowe.
e)       Kusaidia ukarabati na ujenzi wa vyoo Skuli za Msingi Kidagoni, Bwereu, Kandwi, Chaani Kubwa, Potoa na Kilima Juu.
f)        Kujenga kituo cha kuhifadhia Mitihani – Mkwajuni.
g)       Kujenga kiwanda cha kusagisha nafaka – Nungwi.
h)       Kujenga masoko ya Bwekunduni na ujenzi wa Soko la Kinyasini.
i)         Kuimarisha utendaji kwa kununua vifaa na kuwajengea uwezo wafanyakazi wa Halmashauri na kusaidia maendeleo ya elimu katika Wilaya Kaskazini ‘A’.
j)         Kujenga njia ndogo Tumbatu Gomani na Shindoni/Chutama.
k)       Kuendesha semina kwa wafanyakazi na Madiwani wa Halmashauri.
l)         Kununua gari na jenereta.
m)     Kununua samani na mashine za Ofisi.

43.            Mheshimiwa Spika, Halmashauri inakadiria kupata kiasi cha TZS 782 milioni, ikiwa ni ruzuku kupitia programu ya Market Infrastructure Value Additional Rural Financing (MIVARF) kwa ajili ya uboreshaji miundombinu ya masoko.

HALMASHAURI YA WILAYA YA KASKAZINI ‘B’ UNGUJA


44.         Mheshimiwa Spika, Halmashauri ya Wilaya ya Kaskazini ‘B’, kwa mwaka wa fedha 2011/2012, ililenga kukusanya TZS 214 milioni kutoka katika vyanzo vyake vya mapato na hadi kufikia mwezi Machi 2012, Halmashauri imeshakusanya TZS 184.9 milioni sawa na asilimia 86.4. Kati ya hizo, TZS 68.7 milioni zilitumika kwa kazi za maendeleo na TZS 116 milioni zilitumika kwa kazi za kawaida.

45.         Halmashauri imesaidia miradi ya maendeleo ya Wadi inayotekelezwa na wananchi yenye thamani ya TZS 65 milioni ikiwemo ujenzi wa Skuli, usambazaji wa maji safi, uchimbaji wa visima, ujenzi wa kituo cha afya na  ujenzi wa jengo la ukumbi wa mkutano na Ofisi za Halmashauri (Kiambatanisho Namba 9 kinaonesha orodha ya miradi iliyotelekelezwa).

46.            Mheshimiwa Spika, kwa mwaka wa fedha 2012/2013, Halmashauri ya Wilaya ya Kaskazini ‘B’ imelenga kutekeleza malengo yafuatayo:-

a)       Kukusanya kiasi cha TZS 275.6 milioni kutoka katika vyanzo vyake vya mapato
b)       Kusaidia maendeleo ya elimu katika Wilaya ya Kaskazini ‘B’ kwa kufanya mikutano na wadau wa elimu na kusaidia vifaa vya ujenzi wa Skuli za Donge Mtambile, Donge Kipange, Pangeni, Mbaleni, Donge Kitaruni, Donge Muwanda, Makoba, nyumba ya Walimu Kiwengwa pamoja na jengo la Maktaba Mahonda.
c)       Kusaidia ununuzi wa vifaa vya kusambazia maji safi na salama Mwembehemari, Donge Mbiji na Donge Chechele.
d)       Kusaidia ununuzi wa vifaa vya kusambazia umeme Zingwezingwe na Kinduni.
e)       Kusaidia ununuzi wa vifaa vya kuendeleza vituo vya afya Matetema na Bumbwini Kiongwe.
f)        Uendelezaji wa jengo jipya la Ukumbi wa mikutano wa Halmashauri uliopo Kinduni.
g)       Kusaidia vifaa vya ujenzi na ununuzi wa mbegu za mazao kwa vikundi vitatu vya ushirika vya Mahonda, Bumbwini Makoba na Matetema.
h)       Kusaidia ununuzi wa vifaa vya ujenzi wa masoko Donge Muwanda, Mahonda na Mtendeni Shehia ya Mangapwani.
i)         Uendelezaji barabara za ndani (feeder roads) kwa kutia kifusi barabara ya Mkadini.
j)         Kusaidia utunzaji wa mazingira kwa kupanda miti pembezoni mwa barabara kuu.
k)       Kujenga josho la wanyama Donge Muwanda.
l)         Ununuzi wa vespa na gari moja aina ya (Double cabin).
m)     Kuwajengea uwezo wafanyakazi watatu wa Halmashauri, wawili ngazi ya Shahada ya kwanza ya sheria na Utawala wa Umma na mmoja ngazi ya cheti katika fani ya Katibu muhtasi.

HALMASHAURI YA WILAYA YA KUSINI

 

47.            Mheshimiwa Spika, kwa mwaka wa fedha 2011/2012, Halmashauri ya Wilaya Kusini ililenga kukusanya TZS 94.6 millioni kutokana na vyanzo vyake vya mapato na hadi kufikia mwezi Machi 2012, ilikusanya TZS 110 milioni sawa na asilimia 116.3  na kutekeleza yafuatayo:-
                              
a)       Imesaidia miradi ya wananchi kwa kupeleka vifaa vya ujenzi vikiwemo saruji, milango na matofali katika Kituo cha Afya Bwejuu, Skuli ya Kiongoni, Skuli ya Muungoni, Ukamilishaji wa vyoo Skuli ya Paje na ujenzi wa wodi ya kituo cha Afya Mtende vyenye thamani ya TZS 27.8 milioni (Kiambatanisho Namba 10 kinatoa ufafanuzi zaidi).
b)       Imeratibu ukusanyaji wa taka katika Hoteli za kitalii ili kuzuwia utupaji taka ovyo pamoja na uchafuzi wa mazingira.
c)       Kuendelea kutayarisha mji wa kisasa wa Uswiswi kwa kuzingatia ujenzi unaofuata sheria na kanuni.
d)       Imenunua vifaa vya Ofisi ikiwa ni pamoja na gari moja, kompyuta na vifaa vya kuandikia.
e)       Halmashauri ya Wilaya ya Kusini Unguja ilishirikiana na Kamati za Mazingira za Shehia, imetoa vifaa vya kufanyia usafi kwa Shehia za Paje, Kizimkazi Mkunguni na Kajengwa vyenye thamani ya TZS 301,000.

48.            Mheshimiwa Spika, shughuli nyengine zilizotekelezwa ni kuwaelimisha wananchi kupitia mikutano ya hadhara katika Shehia zao ili waweze kufahamu kazi na wajibu wa Halmashauri ambapo jumla ya mikutano minane ilifanyika.

49.            Mheshimiwa Spika, kwa mwaka wa fedha 2012/2013, Halmashauri ya Wilaya ya Kusini imepanga kutekeleza malengo yafutayo:-

a)    Kukusanya TZS 139.3 milioni kutokana na vyanzo vyake vya mapato
b)    Kutekeleza miradi ya wananchi kwa Wadi tatu ambayo ni kukamilisha ujenzi wa kituo cha Afya Kajengwa, kununua mipira ya maji yenye thamani ya TZS 5 milioni Muungoni na kuendelea na ujenzi wa kituo cha Skuli ya Maandalizi ya Jambiani Kibigija
c)    Kuendelea na ujenzi wa Ofisi ya Halmashauri ya Wilaya Kusini
d)    Uendelezaji wa soko la Kitogani
e)    Matayarisho ya ujenzi wa soko jipya Paje.
f)      Ujenzi wa bustani na maegesho ya gari katika kijiji cha Makunduchi.
g)    Ujenzi wa kitalu cha miti katika kijiji cha Kitogani.
h)       Kuwaendeleza wafanyakazi kwa kuwapatia mafunzo ya muda mrefu wafanyakazi 3 katika ngazi za Cheti na Stashahada katika fani za Rasilimali Watu, Utunzaji Kumbukumbu na Uhasibu.

HALMASHAURI YA WILAYA YA KATI


50.            Mheshimiwa Spika, kwa mwaka wa fedha 2011/2012, Halmashauri ya Wilaya ya Kati ililenga kukusanya TZS 174.5 milioni kutokana na vyanzo vyake vya mapato na hadi kufikia mwezi Machi 2012, ilikusanya TZS 137.6 milioni asilimia 78.9 na kutekeleza yafuatayo:-

a)       Imesaidia ujenzi wa Jengo moja la Madrasa Shehia ya Mchangani.
b)       Imesaidia ujenzi wa Maduka Kipilipilini ambapo yamefikia hatua ya linta.
c)       Imesaidia mradi wa usambazaji maji safi na salama pamoja na utiaji wa kifusi Shehia ya Dunga Kiembeni.
d)       Imesaidia ujenzi wa Skuli ya Chekechea Mpapa, madarasa katika Skuli ya Msingi Unguja Ukuu Tindini.
e)       Imetandaza nyaya za umeme ndani ya kituo cha afya na nyumba ya daktari katika Shehia ya Tunguu.
f)        Imenunua kompyuta moja kwa Skuli ya Sekondari Unguja Ukuu.
g)       Ujenzi wa vyoo viwili katika Ofisi ya Halmashauri Dunga.

51.               Mheshimiwa Spika, Halmashauri ya Wilaya ya Kati kwa mwaka 2012/2013, inatarajia kutekeleza malengo yafuatayo:-

a)       Kukusanya jumla ya TZS 200 milioni kutoka katika vyanzo vyake vya mapato
b)       Kujenga Skuli ya Maandalizi ya Kibele.
c)       Kujenga Skuli ya msingi ya Mwera-Pongwe.
d)       Kuezeka jengo la soko la Mgenihaji.
e)       Kujenga Skuli ya Maandalizi Dunga.
f)        Kujenga Skuli ya Sekondari ya Uroa
g)       Kumaliza jengo la maduka ya Kipilipilini Chwaka
h)       Kujenga Ofisi ya Halmashauri ya Tunguu.
i)         Kuwaendeleza wafanyakazi kwa kuwapatia mafunzo ya muda mrefu wafanyakazi 3 katika ngazi za Stashahada na Shahada ya kwanza katika fani za Rasilimali Watu na Uhasibu.

BARAZA LA MJI MKOANI


52.            Mheshimiwa Spika, kwa mwaka wa fedha 2011/2012, Baraza la Mji Mkoani lililenga kukusanya TZS 19 milioni kutoka katika vyanzo vyake vya mapato na hadi kufikia mwezi Machi 2012, Baraza limekusanya TZS 31.2 milioni sawa na asilimia 164.2 ya makadirio ya makusanyo na kutekeleza yafuatayo:-

a)       Limejenga sehemu ya paa la soko la Samaki na matunda la Mbuyuni Mkoani kwa thamani ya TZS 4.5 milioni
b)       Limejenga Silabu nne za kuhifadhia taka Kinyasini, Makadara, Kanisani Ng’ombeni na Kipitacho.

53.            Mheshimiwa Spika, shughuli nyengine zilizotekelezwa na Baraza la Miji Mkoani ni kusaidia miradi miwili ya jamii. Miradi hiyo ni ujenzi wa mahodhi mawili ya kuhifadhia taka pembezoni mwa fukwe za Mbuyuni na kuweka saruji kwenye mabanda mawili ya Skuli ya Chekechea Ng’ombeni.

54.            Mheshimiwa Spika, kwa mwaka wa fedha 2012/2013, Baraza la Mji Mkoani linakusudia kutekeleza malengo yafuatayo:-

a)       Kukusanya jumla ya TZS 35 milioni kutoka katika vyanzo vyake vya mapato
b)       Uendelezaji wa ukarabati wa soko la matunda na samaki Mbuyuni Mkoani.
c)       Uwekaji wa kifusi eneo la Mapinduzi na Ng’ombeni.
d)       Kusaidia miradi ya jamii iliyomo katika eneo la Baraza.
e)       Kuongeza ufanisi kazini ikiwemo kuwapatia wafanyakazi stahili zao, kununua vitendea kazi vya kisasa na samani.
f)  Kuendeleza huduma za usafi katika eneo la Baraza la Mji wa Mkoani.
g)       Kuwajengea uwezo wafanyakazi watatu wa Halmashauri, wawili ngazi ya Stashahada katika fani uhasibu.

BARAZA LA MJI CHAKE CHAKE


55.            Mheshimiwa Spika, kwa mwaka wa fedha 2011/2012, Baraza la Mji Chake Chake lililenga kukusanya TZS 64 milioni kutoka katika vyanzo vyake vya mapato na hadi kufikia mwezi Machi 2012, Baraza limekusanya TZS 67.2 milioni  sawa na asilimia 105 ya makisio ya makusanyo na kutekeleza yafuatayo:-

a)       Baraza limeezeka Soko la Machomane na limefanya matengenezo ya Ofisi ya Baraza kwa kujenga ukuta sehemu ya nyuma.
b)       Limetoa misaada wa vifaa vya ujenzi kwa waliopata matatizo Madungu na Mtoni. Aidha, Baraza limeweka kifusi njia ya Machomane.
c)       Limejaza kifusi katika eneo la wafanya biashara wadogo wadogo soko la samaki Chake Chake pamoja na kujenga bomba la kupitishia maji (Culvat), kujenga msingi wa maji machafu katika Mtaa wa Tenga na Silabu mbili katika maeneo ya Mtoni na Kilimatinde.

56.            Mheshimiwa Spika, kwa mwaka wa fedha 2012/2013, Baraza la Mji Chake Chake linakusudia kutekeleza yafuatayo:-

a)       Kukusanya jumla ya TZS 83 milioni kutoka katika vyanzo vyake vya mapato
b)       Kuendeleza ujenzi wa Soko la Machomane
c)       Matengenezo ya Ofisi ya Baraza
d)       Kujenga msingi wa maji machafu Mkungumalofa
e)       Kujenga Skuli ya Maandalizi Machomane mpaka kufikia linta
f)        Kujenga daraja la Mtoni
g)       Matengenezo ya machinjio Kisiwani
h)       Kujenga Silabu tatu Bandataka, Mkungumalofa na Misufini.
i)         Utiaji wa kifusi, usafishaji na utengenezaji wa eneo la kuegesha gari katika eneo la soko la samaki Chake Chake.
j)         Kusaidia maafa ya kijamii.
k)       Kuongeza ufanisi kazini ikiwemo kuwapatia wafanyakazi stahili zao, kununua vitendea kazi vya kisasa na samani.
l)         Kuendeleza huduma za usafi katika eneo la Baraza la Mji Chake Chake.
m)     Kuratibu umaliziaji wa ujenzi wa msingi wa Msingini Mtoni unaosimamiwa na Idara ya Mazingira.
n)       Kuwajengea uwezo wafanyakazi wawili wa Baraza kwa kuwasomesha ngazi ya Stashahada ya Sheria na Uhasibu.

 

HALMASHAURI YA WILAYA MKOANI


57.            Mheshimiwa Spika, kwa mwaka wa fedha wa 2011/2012, Halmashauri ya Wilaya Mkoani ililenga kukusanya TZS 30 milioni kutoka katika vyanzo vyake vya mapato na hadi kufikia mwezi Machi 2012, Halmashauri ilikusanya TZS 44 milioni sawa na asilimia 146.7 ya makadirio ya makusanyo na kutekeleza yafuatayo:-

a)       Kusaidia ujenzi wa Soko la samaki na matunda Mkanyageni kwa kuezeka paa.
b)       Imesaidia ununuzi wa vifaa vya ujenzi wa Msikiti wa Michenzani, Madarasa Chumbageni, Skuli ya Sekondari Kengeja, Skuli ya Msingi Mahuduthi, Daraja la Mto Mkuu Kengeja, Madarasa ya Kengeja na Mwambe vyenye thamani ya TZS 4 milioni.
c)       Imesaidia gharama za mitihani ya majaribio ya wanafunzi wa Wilaya ya Mkoani.
d)       Imeweka kifusi barabara ya Likoni/Kengeja na Msikiti wa Maambani, Chambani.

58.            Mheshimiwa Spika, kwa mwaka wa fedha 2012/2013, Halmashauri ya Wilaya ya Mkoani  inakusudia kutekeleza yafuatayo:-

a)       Kukusanya mapato ya TZS 53.6 milioni kutoka katika vyanzo vyake vya mapato
b)       Kuendeleza ujenzi wa Soko la Samaki na Matunda Mkanyageni.
c)       Kujenga Ukuta Bandari ya Mbuyuni/Kengeja.
d)       Kusaidia shughuli za maendeleo ya wananchi katika Wadi za Kisiwa Panza, Chokocho, Kangani, Mtambile, Kiwani na Mkanyageni.
e)       Kuongeza ufanisi kazini ikiwemo kuwapatia wafanyakazi stahili zao, kununua vitendea kazi vya kisasa na samani.

HALMASHAURI YA WILAYA YA CHAKE CHAKE


59.            Mheshimiwa Spika, kwa mwaka wa fedha 2011/2012, Halmashauri ya Wilaya ya Chake Chake ilikusudia kukusanya TZS 35.2 milioni kutoka vyanzo vyake vya mapato na hadi kufikia mwezi Machi 2012, Halmashauri imekusanya TZS 36.8 milioni sawa na asilimia 104.5 ya makadirio ya matumizi na kutekeleza yafuatayo:-

a)       Imesaidia ujenzi wa kituo cha afya Kibokoni kwa kupeleka vifaa vya ujenzi.
b)       Imefanya matayarisho ya ujenzi wa jengo jipya la Halmashauri kwa kuchora ramani na kutangaza tenda ya ujenzi.
c)       Kusaidia ada za masomo ya wanafunzi 36 wa darasa la kumi katika Shehia ya Wesha na ukarabati wa njia ya Gombani/Ng’ambwa.

60.            Mheshimiwa Spika, kwa mwaka wa fedha 2012/2013, Halmashauri ya Wilaya ya Chake chake  inakusudia kutekeleza malengo yafuatayo:-

a)       Kukusanya TZS 36 milioni kutoka katika vyanzo vyake vya mapato
b)       Kuendeleza ujenzi wa jengo jipya la Halmashauri kwa kuweka msingi.
c)       Kutia rangi na kuweka milango mitatu katika ukumbi wa mikutano jengo la zamani la Ofisi.
d)       Kusaidia ununuzi wa vifaa vya ujenzi vituo vya afya Matale, Ndagoni na Kibokoni, Madrasa Ng’ambwa, Skuli za Kwale, Ziwani Sekondari, Shungi Sekondari, Mvumoni Msingi, Chanjamjawiri Msingi na Pujini Sekondari. 
e)       Kuongeza ufanisi kazini ikiwemo kuwapatia wafanyakazi stahili zao, kununua vitendea kazi vya kisasa na samani.
f)        Kuwajengea uwezo wafanyakazi wanne wa Halmashauri, wawili katika ngazi ya Stashahada ya uhasibu na wawili katika ngazi ya Cheti (uhasibu na rasilimali watu).

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.