Mtazamo
wa Jamii ya Kizanzibari juu ya Utalii
Semina ya “Dhana ya Utalii kwa wote”.
Iliyoandaliwa na Kamisheni ya Utalii Zanzibar, Hoteli ya Bwawani
18 Juni, 2012
Mtayarishaji na muwasilishaji Mada: Dkt. Issa H. Ziddy, Chuo Kikuu (SUZA
• Kusafiri kutoka sehemu moja hadi nyengine kwa lengo la
kujifurahisha, kujifunza na kupata maarifa ya mambo mapya: المعجم
العربي الأساسي
Kusafiri katika nchi kwa ajili ya matembezi, kusoma,
kutafiti na kugundua mambo: http://islamqa.info/ar/ref/87846
Malengo ya Utalii
• Kujifurahisha: Kujiliwaza kwa kutembelea mandhari za kipekee na za
kuvutia
• Kijamii: kutembelea wapenzi, ndugu na jamaa
• Kielimu: mafunzo, na kubadilishana uzowefu
• Kiutamaduni: maonesho, michezo, sanaa, matamasha, sherehe za
kijadi, kimila, kuzuru majengo na sehemu za historia.
• Kidini: kuzuru miji mitakatifu, majumba, sehemu tafauti za ibada.
Historia ya Utalii Zanzibar
![]() |
Utalii enzi hizo |
• Zanzibar imevutia watalii wengi mno hata kabla ya
kuzaliwa Nabii Issa. (W. H. Ingrams, Zanzibar its History and its people + جهينة
الأخبار في تاريخ زنجبار )
• Sababu kuu: Eneo ilipo, hewa mwanana, mandhari na
fukwe nzuri, tamaduni anuwai (Idrisi, Ibnu Khalduun, Abu Zayd Hassan, AlBiruni,
Ibn Batuta, Abulfeda, Captain James Lancanster
1592, Mr. Burton nk)
Watalii walitoka Afrika, Arabuni, Asia, Bara Hindi,
Ulaya na Marekani (A guide to Zanzibar
Historia
• kuanguka kwa bei ya zao la karafuu katika soko la
dunia kwenye miaka ya 1970 na 80, kuliporomosha ukuaji uchumi Zanzibar
• utalii ukahuishwa na kuwa njia mbadala ya kukuza
uchumi wa Zanzibar.
![]() |
Maeneo ya Marikiti Darajani mwaka 1917 |
• Idadi ya watalii iliongezeka sambamba na kuongezeka
idadi ya mahoteli, nyumba za kulala wageni, vivutio vya utalii na ajira
Maoni
ya baadhi ya Wazanzibari
• Mvutano baina ya mahitaji ya utalii na mporomoko wa
maadili na dini
• Serikali inajali zaidi mazingira yatayokuza utalii,
wakati jamii zinatoa aula kwenye maadili
na dini
• Matokeo yake ni suitafahamu baina ya pande mbili hizo
na kutoshiriki katika shughuli za kitalii au hata kuupiga vita.
Mtazamo wa Uislamu kuhusu
Utalii
• Je utalii unaruhusiwa katika dini ya Kiislamu?
• Kama jawabu ni ndio; Je ni utalii wa aina gani
unaoruhusiwa?
• Je kuna mipaka na vigezo vyovyote vya utalii katika
Uislamu?
• Je kuna nchi za Kiislamu zinazokuza uchumi wake kwa
shughuli za utalii?
Hukmu ya Utalii katika Uislamu
• Utalii unaofuata misingi na miongozo inayokubaliwa na
Uislamu ni halali (مندوبة) (Dkt. Hussein Hussein Shihata – Azhar University)
• Aya ya 9 ya Sura ya Ar-ruum na Aya ya 13 ya Sura ya
Al-hujraat
• “madua’at” , “Tabliigh” na wafanya
biashara, Mahujaji ni mfano
Faida za Utalii unaokubalika
katika Uislamu
• Ni nyenzo inayosaidia malezi ya kiroho na kiimani.
(Al’imraan: 191)
• Ni nyenzo ya kujuana na kutambuana. (Al-hujraat: 13)
• Ni nyenzo ya utekelezaji wa baadhi ya ibada
• Husaidia “Tabliigh”. - hupata kipato, Taaluma
• Utalii wa biashara ndio ulioeneza Uislamu ZNZ
• Husaidia kukuza nafsi na kupumzisha mwili
Mipaka ya Utalii katika Uislamu
• Uwe unalinda akili, nafsi, familia/jamii, mali,
mazingira na ibada – Wasio waislamu hawakatazwi kutalii ktk jamii za Kiislamu
• Uwe ktk nyanja za uhalali ktk kauli, amali na tabia
(Fatwa nambari (332 / 26) na (224 / 26)
ya "اللجنة الدائمة" )
• Uwe unahifadhi maadili, mila, utamaduni, mwenendo na
vipaumbele vya halali vya jamii
• Uwe unachangia uchumi na maendeleo ktk jamii
• Usipelekee kufanya dhambi na israfu
kuondosha dhana
kuwa hapana tija ya utalii bila ya kuwapo ulevi, uasharati, kamari nk
Nchi za Waislamu na Utalii ...
• OIC inahamasisha uatalii na inalitambuwa Shirika la
Utalii Duniani (WTO)
• Benki ya Kiislamu ya (IDB) inafadhili Utalii
• Licha ya kutangaza kufuata sera za Kiislamu, Malaysia
imekuwa ni nchi ya 14 duniani kwa kupokea watalii wengi wa kimataifa mwaka 2005
kwa mujibu wa ripoti ya WTO. Katika Commonwealth ni nchi ya tatu
• Faida za watalii wanaotoka nchi za Kiislamu
• Malaysia na Maldives zimevutia watalii wa dunia kwa
kauli mbiu ya Tourist Friendly na Muslim Friendly
• Uturuki na Malaysia zimeshinda msimu wa Utalii wa
mwaka 2001-2002
• Tukio la kigaidi la Septemba 11, 2011 limepelekea
kuwapo kwa (Religious/Islamic Tourism)
• Umuhimu wa kujitambulisha waziwazi katika dunia kuhusu
sera za utalii zinozofuatwa
• Saudia inakuza uchumi wake kwa utalii pia
Tathmini ya Utalii wa Zanzibar
• Je malengo yake yanaendana na haja ya jamii?
• Je kuna uwiano baina ya uchumi na maadili ya
wanajamii?
• Je waanajamii wazanzibari wanashirikishwa?
• Je muamala wa utalii unaendana na maadili ya jamii?
• Je Utalii wa ZNZ ni kwa ajili ya uchumi na pesa tu au
pia kutunza maadili na utamaduni?
Maoni ya mwisho
![]() |
Dk Ziddy Akiwafundisha Watalii kuvaa mavazi ya kiasili ya Mzanzibari |
• Juhudi zifanywe ili kuondosha dhana kwamba kazi za Utalii ni za kihuni.
• Kutilia mkazo utalii unaoonesha silka na hali halisi
ya ZNZ na sio kuharibu historia
• Kutilia mkazo vivutio vya utalii vinavyochunga maadili
ya jamii ya Zanzibar kama nguo, lugha, uvuvi, kilimo, taaluma vyuo vya kielimu
nk
• Kuwa na watembezaji watalii wanaoijua Zanzibar na
historia na wenye maadili mema
Maoni…
![]() |
Dk Zidy akiwa na Watalii waliovaa vizuri mavazi yetu ya kiasili |
• kuandaa vipeperushi vingi vinavyoonesha maadili ya
Mzanzibari na kuwaomba wageni kwa lugha ya kidiplomasia waheshimu maadili hayo
• Kutangaza utalii katika nchi za Kiislamu na kuzifanya
huduma ziwe rafiki kwa watalii wa nchi hizo na nyenginezo.
• Kuwaandalia watu wa ndani sehemu na kuwashajihisha
kutalii.
Ahsanteni kwa Kunisikiliza.
No comments:
Post a Comment