Habari za Punde

Dk Shein Afungua Semina ya Kuimarisha Uhusiano Baina ya Wanasiasa na Watendaji wa Serikali za Mitaa Zanzibar

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,pia Mwenyekiti wa Semina ya kuimarisha Uhusiano baina ya Wanasiasa na watendaji katika Serikali za Mitaa Zanzibar,wakati  semina hiyo ikiendelea katika ukumbi wa Karume Hall Zanzibar Beach Resort,nje ya Mji wa Unguja,(kulia) Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi,na (kushoto) Katibu Mkuu Kiongozi Dk.Abdulhamid Yahya Mzee.
 Baadhi ya   Masheha na Madiwani wakiwa katika Semina ya Uongozi ya Viongozi wa Serikali za mitaa Zanzibar,wakimsikiliza Mwenyekiti wa Semina hiyo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza
la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,alipokuwa akiendesha  michango mbali mbali iliyotolewa kabla ya kuifunga leo katika ukumbi wa Zanziar Beach Resort,nje kidogo ya Mji wa Unguja.
 Mwanasheria wa  Mahakama ya Ardhi Zanzibar,Khamis Faraji Abdalla,akiwasilisha mada ya  wajibu wa Serikalki za Mitaa katika kusimamia taratibu na Sheria za Ardhi ,katika semina ya  kuimarisha Uhusiano baina ya Wanasiasa na watendaji katika Serikali za Mitaa Zanzibar, iliyomalizika leo katika ukumbi wa wa Zanzibar Beach Resort, nje kidogo ya Mji wa Unguja.
 Baadhi ya Madiwani na Masheha,wakimkaribisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, pia Mwenyekiti wa Semina ya kuimarisha Uhusiano baina ya
Wanasiasa na watendaji katika Serikali za Mitaa Zanzibar,wakati semina hiyo ikiendelea baada ya mapunziko ya kipindi cha kwanza, kabla ya kuifunga semina hiyo, katika ukumbi wa Zanzibar Beach Resort,nje kidogo ya Mji wa Unguja.
 Sheha wa Shehia ya Ubago Unguja Wilaya ya Kati Unguja,Bibi Asha Abeid Suba,akichangia mada iliyozungumzia maji, wakati wa Semina ya Uongozi ya Viongozi wa Serikali za mitaa,iliyowashirikisha Madiwani na Masheha katika ukumbi wa Zanziar Beach Resort,nje kidogo ya Mji wa Unguja iliyomalizika leo.
Diwani wa Jimbo la Amani  Abdalla Ali Choum, alipokuwa akichagia mada ya mazingira,wakati wa Semina ya kuimarisha Uhusiano baina ya Wanasiasa na watendaji katika Serikali za Mitaa Zanzibar,iliyomalizika leo katika ukumbi wa Zanzibar Beach Resort,nje kidogo ya Mji wa Unguja[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.