Na
Abdi Shamnah – WHUUM
Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na
Michezo, Said Ali Mbarouk, amefanya uteuzi wa wajumbe 15, watakaounda Baraza la
Kiswahili Zanzibar, kwa kipindi cha miaka mine ijayo ( 2012 – 2016).
Waziri Mbarouk, amefanya uteuzi huo kwa mujibu
wa kifungu cha sheria no. 4 cha Sheria ya Baraza la Kiswahili Zanzibar, Act
No.4 ya 2004.
Katika Baraza hilo, kuna sura za wajumbe
watatu wa zamani walioteuliwa kuendelea
na kazi hizo kutoka Baraza lililopita. Wajumbe hao ni pamoja na Said Khalfan Amour
(NGO’s), Feisal Abdalla Said (ukaguzi Elimu Pemba) pamoja na Suleiman Maulid
Hega kutoka BAKITA jijini Dar es Salaam.
Wajumbe wapya walioteuliwa katika Baraza
hilo ni pamoja na Ameir Kitwana Karibu kutoka Mkoa wa Kusini Unguja, Mbweni
Mussa Ame (Kaskazini Unguja), Sharfan Twaha Mussa (Mkoa wa Mjini Magharibi),
Mwanakheir Mohammed Haji (Mjini Magharibi) na Rehema Ameir juma kutoka Mkoa wa
Kusini Pemba.
Aidha wajumbe wengine (wapya) ni pamoja na
Hamad Khamis Juma (Mkoa wa Kaskazini Pemba), Haji Makame Ussi (Ofisi ya rais),
Mmanga Mjengo Mjawiri (SUZA), Asha Mhene Hamad (SUZA), Kijakazi Omar Makame
(SUZA) na Makame Abdalla Seti (ZBC).
Hivyo wajumbe hao wataungana na Mwenyekiti wa Baraza hilo , Amour Abdalla
Khamis, ambae kwa mujibu wa sheria atamaliza muda wake mwaka ujao baada ya
kuliongoza Baraza hilo kwa kipindi cha miaka mitano.
No comments:
Post a Comment