Habari za Punde

Pinda ataka vyombo vya dola vipewe nafasi

Na Kunze Mswanyama, DODOMA 

SERIKALI imeviagiza vyombo vya ulinzi na usalama kufuatilia utekwaji nyara, vipigo na mauaji matukio ambayo umetokea maeneo mbali mbali ya nchi katika siku za hivi karibuni. 

 Waziri Mkuu Mizengo Pinda alieleza hayo jana Bungeni mjini Dodoma, alipokuwa akijibu suali papo kwa papo aliloulizwa na mkuu wa kambi ya Upinzani Freeman Mbowe. 

Katika suali lake, Mbowe aliitaka serikali kutoa tamko juu ya hisia za kuwepo kwa mauaji, utekwaji na vipigo vyenye lengo la kuleta mauaji kwa viongozi wa kisiasa na hata wananchi wa kada mbalimbali huku vyombo vya usalama vikituhumiwa kufanya matukio hayo. 


 Mbowe alisema matukio mbali mbali yanayojitokeza yameonekana kuwa na utata jambo linalowafanya wananchi kupoteza imani na serikali yao kuwa haijali mauaji au mateso wanayoyapata bila hatia. 

 Pinda alisema serikali imeviagiza vyombo hivyo kufanyakazi yake na kuhakikisha inawatia nguvu wahusika wa vitendo hivyo na kwamba hakuna chombo cha dola ambacho kinaweza kushiriki katika kufanya matendo hayo. 

 Mbowe pia alimuuliza Pinda kuhusiana na tetesi zilizoko mitaani zinazovuhusisha vyombo vya dola kumteka, kumpiga na hatimaye kumjeruhi kabla ya kumtekeleza Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari Dk.Stephen Ulimboka wiki iliyopita. 

 Waziri Mkuu aliwataka wananchi kutulia na kuiachia serikali ifanyekazi zake kwa umakini bila ya msukumo kutoka kwa wanasiasa hali itakayotoa majibu ya kudumu juu ya matukio hayo yasiyokubalika kwenye jamii ya kistarabu. 

 Hata hivyo Pinda aliktaaa kukubali kauli ya Mbowe kuwa sifa ya Tanzania kimataifa imechafuka kutokana na matukio hayo ikiwemo pia yamauaji. Alisema jina la Tanzania haijachafuka kabisa kwa kiasi anachosema Mbowe huku pia akimtaka kuacha kuzungumzia suala la kupigwa kwa Ulimboka pasipokuwa na ushahidi kuwa serikali imehusika na kipigo hicho na vya raia wengine.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.