UJENZI wa
Bandari kubwa na yenye hadhi ‘hurb port’, uko kwenye hatua ya uchambuzi lakini
kikwazo kikubwa cha ujenzi huo ni gharama.
Naibu waziri wa
wizara ya Miundombinu na Mawasiliano Issa Haji Ussi alieleza hayo jana katika
ukumbi wa Baraza la Wawakilishi alipokuwa akijibu suali la Mwakilishi wa Muyuni
Jaku Hashima Ayoub.
Naibu huyo
alisema serikali ina azma ya kujenga bandari mpya na ya kisasa ambapo katika
utekelezaji wake tayari uchambuzi yakinifu umeshafanywa.
Alisema kutokana
na kikwazo cha gharama, serikali imeona ni vyema kuangalia tena na kujiridhisha
juu ya gharama iliyopendekezwa na makandarasi waliofanyakazi hiyo ya uchambuzi
yakinifu.
Naibu huyo
alisema kutokana na faida ya kimaumbile na kijiografia na ujenzi wa bandari
hiyo ukikamilika bandari zote
zilizojirani na Zanzibar haiwezi kuwa tishio kibiashara.
Alisema bandari
hiyo itakuwa ndiyo ‘hurts’ kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati.
No comments:
Post a Comment