Na Mwantanga Ame
UONGOZI wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), umepanga kuyafanyia usafi makaazi ya nyumba Wazee Amani, Wilaya ya Mjini Unguja ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha miaka 48 ya kuanzishwa kwa jeshi hilo.
Hatua hiyo imetangazwa jana na Idara ya uhusiano Makao Makuu ya Brigedia ya Nyuki Zamzibar, katika taarifa yao iliyosambazwa kwa vyombo vya habari Mjini Zanzibar.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo kutokana na kuwapo kwa maadhimisho ya miaka 48 ya Jeshi hilo linakusudia kufanya usafi katika maeneo ya makaazi ya nyumba ya Wazee ya Amani.
Jeshi hilo pia limeeleza kuwa litaafanya usafi huo katika skuli ya msingi ya Mtoni, maeneo ya kambi ya Mtoni, na zahanati ya Kidimni.
Maeneo mengine ambayo yanatarajiwa kufanyika kwa usafi huo, taarifa hiyo imeeleza ni pamoja na barabara zinazoizunguka kambi hiyo hadi soko la Shimoni Mombasa Wilaya ya Magharibi Unguja.
Idara hiyo imefahamisha kuwa imeamua kuyafanyia usafi maeneo hayo ikiwa ni hatua ya muendelezo wa kuihudumia jamii kutokana na dhana halisi ya Jeshi hilo kuwa ni malai ya Wananchi wa Tanzania.
« mbali ya kupigana vitasanjari na ulinzi wa amani katika nchi mbali mbali tangu wakati huo JWTZ imekuwa ikishiriki kikamilifu katika majanga ya kitaifa kama mafuriko, kuzama Mv. Bukoba, Skagit, kuanguka kwa treni Dodoma, kuzima moto » Ilisema taarifa hiyo.
Idara hiyo imeeleza kuwa, Jeshi litaadhimisha sherehe hizo ifikapo Septemba 1, 2012 ikiwa ndio tarehe lilipoasisiwa mwaka 1964, na kazi hizo za usafi zitamaliza kufanyika leo.
No comments:
Post a Comment