Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akitoa shukrani kwa viongozi na watendaji wa CUF walioitikia mwaliko wa futari ya pamoja aliyoiandaa kwa ajili ya viongozi hao huko nyumbani kwake Mbweni, nje kidogo ya mji wa Zanzibar. Kulia (aliyesimama) ni Mkurugenzi wa habari na haki za binadamu wa CUF Bw. Salim Bimani.
Baadhi ya viongozi na watendaji wa CUF wakijumuika katika futari ya pamoja iliyoandaliwa na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar ambaye ni Katibu Mkuu wa chama hicho Maalim Seif Sharif Hamad, huko nyumbani kwake Mbweni.
Baadhi ya viongozi na watendaji wa CUF wakijumuika katika futari ya pamoja iliyoandaliwa na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar ambaye ni Katibu Mkuu wa chama hicho Maalim Seif Sharif Hamad, huko nyumbani kwake Mbweni. (Picha na Salmin Said, OMKR).
Na Hassan Hamad, OMKR
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad amewashukuru viongozi na watendaji wa Chama Cha Wananchi CUF kwa kuitikia mwaliko na kujumuika nae katika futari ya pamoja aliyoiandaa kwa ajili ya viongozi hao.
Akitoa shukrani baada ya futari hiyo iliyofanyika nyumbani kwake Mbweni, Maalim Seif alisema hali hiyo inaonesha upendo na mshikamano miongoni mwa viongozi na wanachama wa chama hicho.
Amewatakia kila la kheri viongozi na watendaji hao katika mwendelezo wa mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani, na kuwataka waongeze mshikamano na upendo miongoni mwao katika kutafuta radhi za Mwenyezi Mungu.
Viongozi na watendaji kadhaa wamejumuika katika futari hiyo wakiwemo Makamu Mwenyekiti wa CUF Bw. Machano Khamis Ali, Mkurugenzi wa habari na haki za binadamu Bw. Salim Bimani na Mwakilishi wa Jimbo la Ole Mhe. Hamad Massoud Hamad.
No comments:
Post a Comment