Na Mwinyi Sadallah
Waziri asiye na Wizara Maalum wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Mansoor Yussuf Himid, amependekeza kuwepo na Muungano wa mkataba kati ya Tanzania bara na Zanzibar.
Mansoor alitoa matamshi hayo wakati akichangia hoja kwenye semina ya mjadala wa mchakato wa ukusanyaji maaoni ya uundwaji wa Katiba mpya ya Jamhuri ya Muugano Tanzania uliofanyika katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Chukwani Zanzibar.
Alisema ipo haja ya kuwa na Muungano wa mkataba ili kuondokana na malalamiko mengi ambayo yanalalamikiwa katika Muungano wa sasa.
Katika maelezo yake, Mansoor alisema bado ataendelea kuwa muumini wa mfumo wa serikali mbili chini ya mkataba na si kama ilivyo sasa ili kuipa fursa zaidi Zanzibar kujijenga na kujitegemea kiuchumi.
Alisema si dhambi Zanzibar na Tanganyika chini ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zote zikawa na viti viwili katika Umoja wa Mataifa (UN).
Alieleza kuwa kuna baadhi ya viongozi kwa malengo yao binafsi wanajaribu kuwajengea hofu wenzao na kuwazuia kutoa maoni yao kwa upana kama raia huru kwa mujibu wa Katiba ya nchi.
Aliongeza kuwa hajawahi hata mara moja kukataa Muungano, ila mara zote amekuwa akihimiza mabadiliko ya kimfumo katika Muungano huo na kwamba anaamini kuwa kufanya hivyo si uadui wala usaliti.
“Hata NEC ya CCM ilipoanzisha mchakato wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa kulienezwa hofu kila mahali, nashukuru tumefanikiwa kuunda GNU, sasa imesimama na kusonga mbele, kila mmoja anaona fahari, faida na tija ya jambo hilo,” alisema.
Hata hivyo, kauli ya Mansoour ya kutaka Muungano wa mkataba na suala zima la kila upande kuwa na kiti UN, inamaanisha kwamba Zanzibar inapaswa kuwa huru.
Alisema awali suala la kuundwa kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa lilipoibuliwa na Rais Jakaya Kikwete, kulikuwa na mtazamo hasi kwa baadhi ya wanasiasa waliokuwa wakiamini kuwa kuundwa kwa GNU kungetoa mwanya wa kuwarejesha watawala waliopinduliwa Januari 12,mwaka 1964 na kulipizana visasi.
“Hata wenzetu wa CUF kabla ya GNU, walikuwa wakipinga kila kitu kizuri cha SMZ, baada ya kushirikishwa serikalini hata yale waliyokuwa wakiyapinga wakati ule, sasa wanayaunga mkono, kuyasimamia na kuyashangilia,” alisema Waziri Mansoor.
Akizungumzia umuhimu wa dhana ya Muungano alisema hapendi uvunjike na kwamba mara zote amekuwa akitaka hoja na haja ya Muungano huo kufanyiwa marekebisho ya msingi na kuwa chini ya mkataba.
Waziri huyo wa SMZ ambaye pia ni Mwakilishi wa Jimbo la Kiembesamaki kwa tiketi ya CCM, aliongeza kuwa ikiwa maoni yake yatachukuliwa na chama chake kuwa ametenda dhambi, atakuwa tayari kukabiliana na adhabu yoyote atakayopewa.
“Niko tayari kuadhibiwa kwa kutoa maoni ninayoyaamini kama ni ya kujenga, nafikiri nimetumia haki yangu ya Kikatiba na kiraia, nataka Zanzibar iwe na nyenzo zake za kiuchumi kwa maendeleo ya watu wake, sijali na wala sitawasikiliza wanaoeneza maneno ya uzushi,” aliongeza Waziri Mansoor.
Alisema kila Mzanzibari anayo haki ya kutoa maoni yake bila mtu mwingine kuzuia utashi wake huku akisisitiza kuwa hiyo ndiyo demokrasia anayoijua yeye ndani ya chama chake.
Hata hivyo, aliipongeza CCM kuwa ina mwelekeo, viongozi wake wana uwezo wa kuvumiliana na kupima mabadiliko ya nyakati.
“Ninakiheshimu sana chama changu, ninakipenda, ndicho kilichonilea, bado ni imara sana, kuna watu wanataka kukichafua, kufika kwetu hapa ni kutokana na utashi wa viongozi wake kuwa na dira na uvumilivu,” alisema.
Jamani, mwenye kufahamu naomba maelezo zaidi juu ya Muunngano wa Mkataba. Kwa kweli sifahamu hapa panakusudiwa nini. Kwani huu Muungano wa sasa hivi hauna Mkataba? Muungano huu wa sasa hivi na huo wa Mkataba utakuwa unatofauti gani? Anaejua anijuvye!
ReplyDeleteMuungano wa sasa hv ni muungano wa katiba.nchi zinatumia katiba moja.ila muungano wa mkataba kila nchi iwe na katiba yake.pili zile nchi zilizoungana nazo ziwe na majina yao na kujitegemea ktk masuala km ya kiti cha UN nk.sio km ss hv hatuoni nchi ya tanganyika imeenda wapi.wizara zao wamezipa jina la tanzania.jambo ambalo sio sahihi.lazima zikuwepo wizara na katiba za tanganyika.baada ya hapo kuna mambo yataamuliwa yawe ya mashirikiano ili kuendeleza umoja na muunagno pamoja na udgu ulokuwepo
ReplyDeleteAhsante sana Kaka/Dada kwa maelezo yako. Kwani ni nini Katiba? Katiba sio Mkataba? Hivi sasa ZNZ hatuna Katiba yetu? Hivyo kwani tunachogombania ni majina na viti katika Umoja wa Mataifa? Sidhani kama Waznz tunajua wapi tunaelekea na nini tunajitakia. Hao wanaotuchukua huko ni tayari ma-trillionaires na wanachotaka ni ulwa tu, bali sisi tunataka kunyanyua hali zetu. Hali zetu hazitonyanyuka kwa kuwa Bw. Mansoor ni Balozi wa Zanzibar katika Umoja wa Mataifa. Sidhani kama Mansoor anapigania wachini na wanyonge! He has everything na sasa anataka ukubwa zaidi tu. Ni kweli Bara inatunyima opportunities za kujiendeleza, lakini we need to know exactly what we want na sio matakwa ya wawili ambao tayari wanacho kila kitu na "kila pahala ni pao"!
ReplyDeleteBara is a vast opportunity for us to do biz with. We don't screw the chance to work with them amicably because we will repent. Ni lazima hili jambo lichukuliwe kimaarifa na kwa uwerevu mkubwa na sio kwa jazba ya wawili ambao hawana haja ya kunyanyua hali ya maisha yao kama sisi wachini.
Kuwageuza Bara kama ni wakoloni na kuwafananisha na wakoloni waliopita sidhani kama tunataka kujenga uwelewano mzuri nao baada ya huo uhuru wetu. Ugomvi wetu uwe na hawa jamaa wa Kisiwandui na sio Bara. Bara wanasikiliza sisi wenyewe tunasema nini. Tukisema yule ni Mpemba na asipewe basi ndio hivyo itakuwa!
Hayati Shk Ameir Tajo alisema kwanza tusome. Leo tumesoma, lakini bado we are not very inclusive. Bado tunamuona huyu ni Mpemba na yule ni Muunguja. Huu usalama wa hivi sasa ni kwasababu watu wanapitishiwa vijiko vya asali midomoni mwao. Once vijiko vikiwa vikavu tutarejea kule kule. Sababu au kero zilizoleta Mapinduzi Zanzibar bado hazijashughulikiwa na kwa sasa zinazidi kukuwa.
We have more to lose in this divorce then them! Tufikirie vipi ndugu zetu wakizanzibari walivyojiamirisha katika kila corner ya Bara. Huyo tunaemwita mkoloni akitupa uhuru wetu itabidi sote tuhamie kwenye nchi yetu huru. After all, kwenu ushakuwa huru ya nini tena unang'ang'ania kukaa kwa mkoloni?
Mwisho, nafahamisha tena kuwa mimi binafsi ninaunga mkono ZNZ iachiwe ipumue, lakini siungi mkono haya maneno ya ovyo yanayotolewa na baadhi yetu kwa faida yao. Hii ni issue ambayo inataka watu wazima wakae kitako na sio few trillionaires wajifanye ndio wasemaji wa wanyonge wa Zanzibar - wanyonge ambao maisha yao kila siku yanadidimia na yanazama pale Chumbe!
Ulioandika dada/kaka yote ni chapwa,wewe kwenu bara eeh?usilete vitisho uliyoyasema yote ni mtizamo wako usio na ukweli ndani,hivyo wewe unataka tutawaliwe kwa kwa sababbu ya mbatata na vitunguu,kama ni hivyo,basi vitunguu na mbatata tutanunua tunapotaka,ikiwa msumbiji,kenya au kwengineko bara wanatuibia tena kimachomacho mchana,na kweli bara ni wakoloni wetu,walituibia na wanaendelea kutuibia,zanzibar inachangia asilimia kubwa katika muungano,kuliko bara hilo unalijua,walikuwa wanatupa asilimia 5 ya mgawio,wakaamua 11 a hiyo kumi na moja hawatupi,bajeti iliyopita hawajatukamilishia,hiyi niasilimia ndogo ya matatizo tuu mambo na mambo,sikiliza wazanzibari sio watu wa matatizo asili,wabara ndi wenye matatizo,ndio maana hata hao wabara hushushia makontena yao zanzibar kwa kukwepa corruption iliyokithiri bara,huo muungano muungano gani wa nchi moja ukalipa ushuru mara mbili,leo sio kwa wazanzibar au wabara,ukivuka kutoka znz to dar unalipishwa ushuru tena na si ushuru watu wanakula wao,hakuna usawa serikali ya ina kila aina ya ufisadi,kuanzia mkapa mpaka mwinyi,lowassa ukija katiak suala la wanyonge wa zanzibari kuzama chumbe,hayo yote yamesababishwa na bara,meli zote zilizozama zilikosa kukaguliwa kianzio cha safari dar es sallam matokeo yake watu kuingizwa bila hesabu pale dar,kwa nini wahusika pale dar wasijiuzulu kama waziri nakadhalika,juzi mmekimbilia kuomba bahari,maana yake mnajipanga mapema,muungano ukivunjika mtuibie bahari,basi mfahamu hilo hatulikubali,katiba ya znz tuliyoipisha mwaka jana zanzibar ni nchi na mipaka ya bahari yake kama mmeona afuta ndio mnakimbilia umoja wa mataifa kubadilisha mipaka hilo hatulikubali,leo hii mnaanza kungombana na jirani zenu malawi kwa ziwa nyasa,lile si lenu ni la nyasaland.tumeshaamka hatutaki tena na nchi kamili tunataka,huo ujanja wa nyani tumeushitukia,mlitufitinisha tukauwana wenyewe kwa wenyewe miaka,kama ni umoj wa afrika,haya yamekwisha sudan juzi imekatwa kipande,znz asilimia 99 waislamu,huko bara kanisa limeshika kila kitu hakuna usawa,kwanza waeke usawa katika dini mbili za tanganyika halafu ndio ndio tuwe na muungano huo unaoutaka wewe,waislamu wa bara wamedhulumiwa haki zao,maskuli yote kikiristo,mahospitali asilimia 90 ya mb=ambo ya tanzania yanaendeshwa na ukatoliki,kuanzia,na mikataba ya nyerere na wakoloni wa kiingereza yaliipa ukristo uongozi wa nchi,kuanzia kcmc,shue za tec na kadhalika,kodi za wanyonge masikini,zinachangia katika matrilioni ya mabajeti ya kuongoza shule za kanisa na hospitali zake hiisio fairkila mwaka wakristo kukatiwa waislamu wakarambiswa,hizo memorandum zilizoekwa na nyerere na wakoloni,watu washaamka itabidi mzifute,waislamu nao wanataka maendeleo wakatiwe chao,kwenye elemu usiseme ndio wameshika wao wanaamua wao,sasa nasema hivi sisi wazanzibar tuachieni tupumue na mkatba,mungano ubalikie,udugu wa jamii upo palepale hauondoki,wewe kama mbongonyoso usitie wasiwasi isipokua sheria msumeno.
ReplyDeleteAhsante kwa majibu yako maxuri,wazanzibari tushikamane wabongonyoso kama hawa,wasituchonganishe,Mansur yussuf Himmid,Amani Karume Oyee,mcheza kwao hutunzwa,jini likujualo halikuli likakwishwa
ReplyDelete