Habari za Punde

Dk Shein akutana na Balozi wa Uingereza nchini

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Balozi wa Uingereza Nchini Tanzania Diane Corner,alipofika Ikulu Mjini Zanzibar kusalimiana na Rais leo
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akizungumza na Balozi wa Uingereza Nchini Tanzania Diane Corner,alipofika Ikulu Mjini Zanzibar kusalimiana na Rais leo.[Picha na Ramadhan Othman Ikulu.]

Na Rajab Mkasaba, Ikulu
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein amefanya mazungumzo na Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Mhe. Diane Corner na kumueleza jinsi Zanzibar ilivyoweka mikakati yake katika kuimarisha sekta za maendeleo hasa sekta ya kilimo.
Mazungumzo hayo yalifanyika Ikulu mjini Zanzibar ambapo, Dk. Shein alimueleza Baliozi huyo kuwa kwa vile Serikali ina mpango mkubwa wa kukifanya kilimo hapa Zanzibar kiwe cha kisasa na chenye tija na hatimae kiweze kuwa na mchango mkubwa katika kuinua hali ya wananchi na uchumi kwa jumla.
Dk. Shein alisema kuwa Serikali inampango mkubwa wa kuendeleza kilimo cha mpunga ambacho ndio chakula kikuu kwa wananchi wa Zanzibar hatua ambayo itapunguza uigizaji wa bidhaa kutoka nje kwa asilimia hamsini ifikapo mwaka 2015 ambapo hivi sasa tani 80000 zimekuwa zikiagizwa kutoka nje.
Alisema kuwa katika kufikia azma hiyo Serikali imeshafanya mazungumzo na Washirika wa Maendeleo ikiwemo pamoja na Serikali ya China, Korea, Marekani na Vietnam amabapo tayari wameshaonesha azma ya kuuunga mkono juhudi hizo za Serikali hasa katika kilimo cha mpunga wa kumwagilia maji.
Katika kuleta mageuzi makubwa ya kilimo nchini Dk. Shein alimueleza Balozi huyo kuwa Serikali imo katika mikakati maalum ya kukiimarisha kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Kizimbani kilichoanzishwa kwenye miaka mingi iliyopita ambacho ni miongoni mwa vituo vys mesnxo kstiks uksnds wa Afrika Mashariki.
Dk. Shein alieleza umuhimu wa Chuo hicho katika kuwapatia wakulima wa Zanzibar mbegu bora ikiwemo mbegu ya mpunga ya NERICA.
Aidha katika maelezo hayo, Dk. Shein alimueleza Balozi huyo lengo la Serikali la kutekeleza dhana ya Usalama wa Chakula kwa kujenga maghala ya kuhifadhia chakula sehemu mbali mbali kwa Unguja na Pemba kama ni hatua ya kuwa na chakula wakati wa ukame na majanga mengine yapotokea.
Kwa upande wa sekta ya uvuvi na ufugaji Dk. Shein alimueleza Balozi huyo kuwa Serikali imelenga kuendeleza uvuvi wa kisasa pamoja na kuimarisha uvuvi wa bahari kuu.
Katika kuendeleza dhana hiyo, Dk. Shein alisema kuwa Serikali inaendelea kuwapatia mafunzo mbali mbali wavuvi na wafugaji ndani na nje ya nchi.
Alisema kuwa Serikali ilishawapeleka wavuvi 50 nchini China kwa ajili ya kujifunza njia bora na za kisasa za kuendeleza shughuli hizo ambapo pia, kwa hivi Serikali ina mpango wa kukodi meli mbili na kuzitumia katika kuendeleza uvuvi wa bahari kuu pamoja na kutoa mafunzo kwa wavuvi.
Pamoja na hayo, Dk. Shein alimueleza Balozi huyo kuwa baada ya kufanya mazungumzo na Washirika wa Maendeleo na wadau wengine, tayari wameijitokeza baadhi yao walioonesha nia kubwa ya juka kuekeza katika sekta hiyo..
Kwa upande wa sekta ya aviwanda, Dk. Shein alimueleza Balozi huyo kuwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imo katika kufufua na kuimarisha viwanda nchini.
Alieleza kuwa katika miaka ya nyuma Zanzibar ilipiga hatua kubwa katika kuimarisha na kuendeleza viwanda vidogovidogo ambavyo ambavyo vilitoa mchango mkubwa katika soko la ajira.
Alisisitiza kuwa suala la ajira hivi sasa limekuwa ni changamoto kubwa ulimwenguni kote hivyo Serikali imo katika mipango ya kufufua viwanda ili viweze kutoa mchango unaostahiki katika kukuza ajira nchini na kufaidika vizuri na rasilimali zilizopo nchini.
Pamoja na hayo, Dk. Shein hakuchelea kumueleza Baliozi huyo jinsi Serikali anayoiongoza inavyosimamia amani na utulivu nchini huku akisisitiza kuwa mashirikiano mazuri yamekuwepo katika kuendleza nchi na kuwaletea maendeleo wananchi kama wanavyotarajia chini ya Serikali yao ya Mapinduzi ya Zanzibar yenye muundo wa Umoja wa Kitaifa.
Nae, Balozi wa Uiengereza Mhe. Diane Corner alipongeza juhudi za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar katika kuhakikisha inawaletea maendeleo wananchi wake huku akiahidi kuwa nchi yake itaendeleza uhusiano na ushirikiano uliopo.
Alieleza kuwa nchi yake inavutiwa na hatua za kimaendeleo zilizofikiwa Zanzibar na kuahidi kuendelea kuziunga mkono.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.