Habari za Punde

Mambo ya Haluwa ya Zenj.

 Mambo ya Zenj ya haluwa hivi ndivyo inavyosongwa haluwa hadi ukaiona ilivya wakati unaila na kuona utamu wake na uzuri wake na pia ubora wa haluwa katika mitaa ya Zanzibar. Haluwa sio kitu kigeni kwa Wananchi wa Zanzibar na Vitongoji vyake.

Haluwa hutumika katika maharusi, maulidi na kuhitimisha hitma hutumia haluwa na Vijana wa Wakati ulewa ujana wetu tulikuwa tukishindana kukata haluwa katika maharusi na hitma misikitini

Nakumbuka siku moja jamaa mmoja alipigwa kombe la haluwa kwa staili ya wahudumu walivyokuwa wakigawa na kuona huyu anakata haluwa kubwa alipikwa kombe la mkono. na kuambulia mafuta badala ya haluwa hiyo ilikuwa katika msikiti wa kwahani enzi hizo kama sikosei mmzee mmoja alikuwa vuti wa kuwatowa kapa vijana wanaotaka kukomoa kukata haluwa. Mzee Muki alikuwa fundi wa kuwatowa watu kaba katika kukata haluwa kubwa kwa mbinu ya kulipinduwa kombe la haluwa, hata mimi ilinikuta lakini sikuwa katika makundi hayo ya vijana wakomoaji, ilikuwa bahati mbaya

1 comment:

  1. Dah!! imenifurahisha sana hii story mimi nakumbuka pale msikiti Mabati na msikiti Makuti pale Kiswandui nishaona live jamaa anaambulia mafuta enzi hizoo!!!

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.