Habari za Punde

Rais wa Zanzibar Dk. Shein Amteuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Viwango Zanzibar.


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohamed Shein amemteuwa Profesa Ali Seif Mshimba kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Viwango la Zanzibar(Zanzibar Bureau of Standards) katika Wizara ya Biashara Viwanda na Masoko Zanzibar.

Kwa mujibu wa Taarifa iliotolewa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Dkt. Abdulhamid Yahya Mzee imeeleza kuwa Rais amefanya uteuzi huo kwa uwezo aliopewa chini ya kifungu 8(2)(a) cha Sheria ya Viwango namba 1 ya mwaka 2011.

Uteuzi huo umeanza jana.

IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR
3/1/2013

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.