Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe. Pandu Ameir Kificho akiongoza Kikao cha asubuhi cha maswali na majibu yalioulizwa na Wajumbe wa Baraza leo asubuhi.
Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wakiwa katika Kikao cha asubuhi cha Maswali na Majibu leo
Waziri wa Nchi Ofisi Rais Ikulu Dkt. Mwinyihaji Makame akijibu maswali ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi yaliowasilishwa katika Kikao hicho kuhusiana na Wafanyabiashara wa Jua Kali na Wanaouza Samaki nje ya Soko la Marikiti Darajani.
Waziri wa Biashara Viwanda na Masoko Mhe.Nassor Mazrui akijibu maswali ya Wajumbe wa Baraza kuhusiana na Wakulima wa Mwani Zanzibar hatma ya bei ya Zao hilo katika soko la Zanzibar bei yake iko shilingi 300/= na wengine hununua shilingi 400/=
Wajumbe wakifuatilia majibu yaMaswali yao.
Mhe. Ali Mzee Ali, Mhe. Mansoor Yussuf Himid na Mhe. Mbarouk Mtando, wikitoka katika Ukumbi wa Baraza baada ya kuahirishwa kwa ajili ya matayarisho ya Kikao cha Kuwasilisha Bajeti ya Serekali leo jioni.
Mwakilishi wa Jimbo la Rahaleo Nassor Salim Jazira, akisisitiza jambo na Mwakilishi wa Bububu Husein Ibrahim Makungu BHAA,wakiwa nje ya ukumbi wa mkutano baada ya kuahirishwa leo asubuhi.
Mwakilishi wa Mji Mkongwe Ismail Jussa akibadilishana mawazo na Wajumbe wa Baraza wakiwa nje ya Ukumbi wa Mkutano leo asubuhi.
Katiba ya Z'bar nayo ibadilishwe wasije wakatuuliwa wazee wetu maofisini.
ReplyDeleteSpika nae anahitaji kukaa na wajukuu zake tena!
Safari hii tafadhali msituchoche na mazungumzo ya Muungano, tunataka kusikia mnazungumzia shida zetu. Tumewashitukia mnatumia mada ya muungano kuficha uoza wenu. Hebu tokeni hapo barazani na muende Skuli ya Hailesalasi wakati wanafunzi wanarudi nyumbani mwao. Mkitoka Haile nendeni Benbella. Mkitoka hapo nendeni Skuli za Kwerekwe. Hizi ni skuli chache tu za mjini ambamo mtaona kundi kubwa la wanafunzi ambao ni wajenga nchi wa baadae. Sasa tunataka mtueleze mnamipango gani ya baadaye ya vijana hawa? Nionavyo mimi hakuna maandalizi yeyote ya maana. Hili ni bomu kama mipango bora haipo. Nyinyi ndio wa kuzima bomu hili. Haya yanatosha kukuwekeni busy. Mambo ya muungano kwao bungeni. Acheni kelele za mlango. Zungumzeni matatizo yetu ya kila siku.
ReplyDelete