Na Mauwa Mussa
Zanzibar. Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Rais wa Zanzibar, Dk Mwinyihaji Makame Mwadini, amesema watumishi wa idara maalumu za SMZ wanaoingia kazini usiku, hawalipwi posho.
Alisema hatua hiyo inatokana na ukweli kwamba huo ndiyo utaratibu wa majukumu yao.
Aliyasema hayo jana alipokuwa akijibu swali la Mwalikishi wa Wawi, Saleh Nassor Juma, katika kikao cha Baraza la Wakilishi kinachoendelea mjini Zanzibar.
Mwakilishi huyo alitaka kujua sababu za wafanyakazi wa vikosi vinavyofanya kazi usiku, kutolipwa posho.
Waziri huyo alisema posho kwa ajili ya watumishi wanaoingia kazini usiku hazikuainishwa katika posho zilizotajwa katika katika Tume ya Utumishi ya Zanzibar.
Alisema hata hivyo hatua hiyo haina maana kwamba Serikali inataka kuwadhalilisha au kuwakatisha tama
Chanzo - Mwananchi
kufanya kazi usiku na mchana ni tofauti ndugu makame wa makame , hio phD yako inatia wasiwasi uliipata vipi ikiwa unashindwa kujua tofauti hii. Mbona wabunge na wawaklishi ambao kazi yao ni kuhudhuria vikao wanalipwa posho ya vikalio? wakati wao hii ndio kazi yao kimantiki.
ReplyDelete