Na Mwajuma Juma
\
TIMU ya Soka ya Benki ya Biashara ya Kenya (KCB Tanzania LTD) imewatambia wenyeji wao wa Benki ya Watu wa Zanzibar kwa kuwafunga mabao 3-2 katika mchezo wa Kirafiki uliochezwa juzi uwanja wa Ziwani Zanzibar.
Pambano hilo ambali lina lenga kuunganisha udugu kati ya mashirika mawili hayo ililichezwa majira ya jioni mbapo KCB tawi la Tawi la Dar Es Salaam ilifanya ziara ya kimichezo visiwani Zanzibar.
Katika mchezo huo KCB ndio waliotangulia kupata bao katika dakika ya 10 kupitia kwa mchezaji wake Rogers Mdowe, wakati bao la pili lilifungwa katika dakika ya 25 na Iddi Nyunga ambapo dakika mbili badae Erick Makundi akafunga bao la tatu.
Kuingia kwa mabao hayo kuliwafanya PBZ kuliendesha mchakamchaka lango la wapinzani wao na kufanikiwa kupata bao katika dakika ya 37 lililofungwa na Twahiri Issa na kuwafanya waende mapumziko kwa timu ya KCB kuongoza kwa mabao 3-1.
Kuanza kwa kipindi cha pili timu zote zilifanya mabadiliko na kuongeza kasi ya kushambuliana lakini kwa upande wa PBZ mabadiliko yao yaliweza kuzaa matunda kwa kupata bao la pili katika dakika ya 75 lililofungwa na Jaha Haji aliyepokea pasi ya Seif Suleiman na kuendelea kushambulia lakini hadi mchezo huo unamalizika KCB mabao matatu na PBZ mawili.
Wakizungumza mara baada ya mchezo huo Meneja Masoko wa Benki ya PBZ Seif Suleiman na nahodha wa timu ya KCB Tanzania LTD Raymond Bunyinyinga walisema kuwa mchezo huo ni moja ya kuendeleza mahusiano yao kirafiki kupitia michezo.
Walisema kuwa taasisi zao pamoja na kutoa huduma za kijamii lakini wamekuwa wakishiriki michezo kwa lengo ya kuziweka sawa afya zao na kuwa na uhusiano wa karibu kati yao wafanyabiashara na jamii kwa ujumla.
No comments:
Post a Comment