Habari za Punde

Mbunge wa Jimbola Kikwajuni azindua Nembo ya Chama cha Michezo cha Watu wenye Ulemavu Zanzibar

                            Nembo ya Chama cha Michezo cha Watu Wenye Ulemavu Zanzibar.
Mwenyekiti wa Chama cha Michezo cha Watu Wenye Ulemavu Zanzibar Hassan Silima, akitowa maelezo kwa Mbunge wa Kikwajuni Hamad Masauni, kabla ya Uzinduzi wa Nembo hiyo uliofanyika katika viwanja vya Amani nje.  
Mbunge wa Kikwajuni Mhe.Hamad Yussuf Masauni, akishangilia baada ya kuzinduwa Nembo ya Chama hicho cha Michezo katika viwanja vya Amaan nje, akiwa na Viongozi wa Chama hicho.
       Mhe. Masauni akifuatilia michezo ya Watu Wenye Ulemavu wakati wa uzinduzi wa Nembo yao.
Wanamichezo wa Chama cha Michezo cha Watu Wenye Ulemavu Zanzibar wakifanya mazoezi ya viungo kabla ya kuonesha uwezo wao katika mchezo wa kuinua vitu vizito.
Mwanachama wa SADZ, Ali Abdalla akionesha umahiri wake katika mchezo wa kuinua vitu vizito akiinua chuma chenye uzito wa Kilo 30.
Mwanamichezo Amina Simba akiinua kitu kizito cha kilo 20, ikiwa ni sherehe za uzinduzi wa Nembo yao.
Viongozi wa Chama cha Watu Wenye Ulemavu wakifuatlia uzinduzi wa Nembo ya Chama cha cha Michezo Zanzibar.
                         Mrisho Pandu akiinua uzito wa kilo 50 wakati wa hafla ya uzinduzi huo.
Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni Mhe.Hamad Yussuf Masauni, akizungumza katika mkutano huo wa Uzinduzi wa Nembo Chama cha Michezo ya Walemavu Zanzibar katika viwanja vya Amaan nje, na kutowa Nasaha zake kwa Wanachama wa chama hicho kudumisha michezo na kufikia kiwango cha Kimataifa katika nyanda ya michezo mbalimbali inayoshirikisha Watu Wenye Ulemavu Zanzibar na kuwahasisha na wengine kujiunga katika mazoezi hayo. 
Mwenyekiti wa Chama cha Michezoya Watu Wenye Ulemavu Zanzibar Hassan Silima, akitowa maelezo ya Chama chao wakati wa uzinduzi wake uliofanyika viwanja vya Amaan nje.  
Makamu Mwenyekiti wa Baraza la MichezoZanzibar BMZ, Khamis Abdalla,akizungumza katika uzinduzi huo na kutowa ahadi ya kuiboresha Nembo hiyo katika kiwango cha Digital kuweza kutumia katika matumizi yao mbalimbali kutambulikana kitaifa na Kimataifa kupitia Nembo hiyo.  
Mwanachama wa SADZ, akisoma risala ya Chama chao baada ya uzinduzi wa Nembo hiyo

 Katibu wa Chama cha Michezo kwa Watu Wenye Ulemavu Zanzibar Hada Khatibu. akisoma Utenzi katika hafla hiyo ya Uzinduzi wa Nembo ya Chama chao uliofanyika katika viwanja vya Amaan nje  





1 comment:

  1. Nembo iko sawa lakini naona imeandikwa Kiswaenglish. Tafsiri iliyo sawa ni : Sports Association for people with physical disabilities.

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.