Miundombinu bingwa wa Netiboli kombe la Mapinduzi

Na Mwajuma Juma
 
MABANATI wa timu ya Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano ya netiboli wameibuka kuwa mabingwa wa michuano ya kombe la Mapinduzi la mchezo  huo kwa wizara za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na taasisi zake.
 
Miundombinu ilifanikiwa kufikia hatua hiyo baada ya mchezo wake juzi kuifunga Wizara ya Kilimo na Maliasili mabao 26-22 katika mchezo ambao ulichezwa kwenye uwanja wa Gymkanah mjini Unguja.
 
Katika michuano hiyo ambayo inachezwa kwa mtindo wa ligi ambapo timu hiyo imeweza kushinda mechi zake zote mbili na kuwafanya waweze kumaliza wakiwa na pointi nne.
 
Jumla ya timu tatu zilikuwa zikishiriki michuano hiyo ambapo Miundombinu mchezo wake wa kwanza waliwafunga Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais mabao 13-9.
 
Kutokana na matokeo hayo timu hiyo inatwaa ubingwa huo huku timu za Kilimo na Ofisi ya Makamo wa pili zitashuka dimbani Novemba 21 kutafuta mshindi wa pili na watatu.

Post a Comment

Previous Post Next Post