Timu ya Netiboli ya Makamo wa Pili yaoneshwa Barabara na Wizara ya Mawasiliano Zanzibar

MICHUANO ya Kombe la Mapinduzi ya Wizara za SMZ kwa mchezo wa netiboli yameanza juzi kwa mwenyeji wa mashindano hayo timu ya Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais kuanza kwa kichapo.

Timu hiyo ambayo ilishuka katika uwanja wa Gymkhanah ilipokea kipigo cha mabao 13-9 dhidi ya wizara ya Miundombinu na Mawasiliano.

Katika mchezo huo ambao mgeni rasmi alikuwa ni Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Bihindi Hamad Khamis ulikuwa na msisimko mkali licha ya kuchezwa na watu wazima, ambapo kutokana na utuuzima wao walilazimika kucheza kwa dakika 40.

Miundombinu ambayo ilianza kuongoza katika kota ya kwanza  kwa kuimaliza wakiwa na mabao sita huku wapinzani wao wakiwa na mabao matano ambapo kota ya pili ambayo ndio ya mwisho ilimalizika kwa Miundombinu kuvuna mabao saba na kuunda idadi ya mabao 13 huku OMKP ikiongeza mabao manne na kuwa na idadi ya mabao tisa.

Post a Comment

Previous Post Next Post