Habari za Punde

Chipukizi waweka kambi kwa ajili ya mapokezi ya vijana wa UVCCM

 Mke wa Mbunge wa Jimbo la Kitope Mama Asha Suleiman Iddi akizungumza na Vijana wa Chipukizi walioweka Kambi kwa ajili ya sherehe za Mapokezi ya Vijana wa UVCCM  Tarehe 5 Januari 2014 ambao wanaendelea na matembezi ya kusherehekea miaka 50 ya mapinduzi ya Zanzibar katika Wilaya mbali mbali za Zanzibar.

Kulia ya Mama Asha ni Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Mjini Magharibi Nd. Othman Kibwana na Kushoto ya Mama Asha ni Mbunge wa Jimbo la Kitope ambae pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi.
 Mbunge wa Jimbo la Kitope Balozi Seif Ali Iddi akimkabidhi mchango wa vyakula mbali mbali Chipukizi Ismail Rajab Abdulla kwa ajili ya   Vijana wa Chipukizi walioweka kambi katika Kituo cha Maandalizi Miembeni Mjini Zanzibar.

Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na Vijana Chipukizi walioweka Kambi ya mazoezi kwa ajili ya mapokezi ya Vijana wa UVCCM wanatembea Wilaya mbali mbali za Zanzibar kuadhimisha sherehe za kutimia miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar hapo Kituo cha Maandalizi Miembeni.

Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.