Habari za Punde

Mama Asha akabidhi zawadi kwa ajili ya mashindano ya kusherehekea miaka 50 ya Mapinduzi

 Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman Iddi akimkabidhi Zawadi ya Bao miongoni mwa Mabao 12 Katibu wa mchezo wa Bao Wilaya ya Chake chake  Nd. Faki Salum Khamis aliyojitolea kuhamasisha mchezo huo ili wajiandae vyema katika mashindano ya bao kusherehekea miaka 50 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ya mwaka 1964.

Kulia ya Mama Asha ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Michezo Zanzibar {BTMZ } Sharifa Khamis, Makamu Mwenyekiti wa UWT Zanzibar Mama Asha Bakari Makame na Afisa Mdhamini Wizara inayosimamia Michezo Pemba Ali Omar.

Katibu wa Mchezo wa Karata Wilaya Chake chake Bwana Amour Khamis Haji akipokea msaada wa Karata kutoka kwa Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman Iddi  tayari kujiandaa na vugu vugu la michezo ya kusherehekea nusu karne ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Mama Asha pia alikabidhi mabusati manane kwa vilabu hivyo vya michezo ya ndani kisiwani Pemba hafla iliyofanyika katika uwanja wa michezo wa Gombani Kisiwani Pemba.

Picha na Hassan Issa wa  - OMPR – ZNZ.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.