Na Khamisuu Abdallah
KIKAO cha Baraza la Wawakilishi cha mwezi Machi kimehamishia mwezi
Januari mwaka huu, na kwamba kikao hicho kitaanza Januari 22 mwaka huu, huko
Chukwani nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, huko ofisini kwake katibu wa
Baraza hilo, Nd. Yahya Khamis Hamad,
alisema kikao hicho awali kinakuwa mwezi Machi na kuangukia Aprili, ambapo mwaka huu kitaanza mapema kutoka na
bunge la katiba.
Katibu huyo alifahamisha kuwa bunge la katiba linatarajiwa kukaa mwezi
Fabuari ambapo litachukua muda wa kati ya siku zisizopungua 70 na kuweza
kufikia Mei, jambo ambalo litakuwa vigumu kufanya kikao cha Baraza katika mwezi
huo.
Alisema kutokana na wajumbe wa baraza hilo kuwa ni wabunge wa Bunge la
katika hivyo ni vyema kikao cha Baraza kikatangulia, ambapo baada ya kumaliza
kikao hicho wajumbe hao wageukie kwenye bunge la katiba.
"Tunatarajia bunge hilo litaanza mwezi wa pili na kukaa siku
zisipongua 70 na inaweza kufika Mei halijamaliza itakuwa ni vigumu sisi kufanya
kikao katika mwezi huo kama iliyokawaida", alifafanua katibu huyo.
Alisema Mkutano huo utakaoanza Januari 22 utakuwa ukijadili kamati za
kudumu kwa mwaka mzima ambapo unatarajiwa kumalizika Febuari 10 mwaka huu.
"Wakati Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya
Mrisho Kikwete alipokabidhiwa rasimu ya pili ya katiba na Jaji Joseph Warioba
hivi karibuni alisema atalitangaza bunge ili lianze kazi yake”, alisema.
Akizungumzia suala la Wajumbe wa Baraza kukwepa na kutoroka vikao
alisema bado suala hilo halijafanyiwa kazi na wanategemea vikao vinayokuja
kulipelekea Barazani na kufanyiwa kazi na kupitishwa rasmi ili kuondoa tatizo
hilo.
No comments:
Post a Comment