Habari za Punde

Mwenyekiti wa Chama cha ADC Awashukuru Wananchi wa Jimbo la Kiembesamaki Kukikubali chama Chake cha ADC.

Mwenyekiti wa Chama cha ADC Mhe Said Miraj, akizungumza na Waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vilioko Zanzibar, akitowa shukrani kwa Wananchi wa Jimbo la Kiembesamaki kukipigia kura Chama chao na kukipa ushindi katika uchaguzi huo kuchukua nafasi ya tatu katika Vyama vilivyoshiriki Uchaguzi huo. baada ya kusimamisha mgombea Wao kutoka katika Jimbo hilo Mhe. Amani Ismail Rashid. 
Mwenyekiti wa Chama cha ADC Mhe.Said Miraj, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari  amesema Uchaguzi huu umewafundisha mambo mengi kuyafanya katika Chaguzi zijazo na kuongea nguvu ili kuweza kuongeza Wanachama katika jimbo hilo na mengineyo, na kusema wamepata mialiko sehemu mbalimbali kutangaza sera zao. 
 Mhe Said Miraj akisoma vipengele vya Rasimu ya Katiba Mpya, mbele ya Waandishi wa habari wakati wa mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Sealand Malindi Zanzibar,
Mhe. Said Miraj akionesha Rasimu ya Pili Katiba, wakati akijibu suala kuhusu Chama chake kina Msimamo gani kuhusu mfumo wa Serekali, na kusema suala hilo ni la Wananchi wenyewe ndio watakaoamua mfumo wa serekali gani wanaitaka, Na kusema kuna Wananchi wanataka Serekali ya Mkataba ukiwaliza hawana jibu wengine serekali tatu pia hawajuwi hizo serekali tatu .wao wanasubiri maamuzi ya Wananchi katika kura ya maoni. 
                                               Mwenyekiti akisisitiza jambo katika mkutano huo.
Waandishi wakifuatilia mkutano wa Mwenyekiti wa akizungumza na waandishi kuhusiana na mafanikio ya Chama chao katika kipindi hichi tangu kusajiliwa na kuweza kushiriki Chaguzi Tatu na kupata tatu Bora katika Vyama vinavyoshitriki uchaguzi huo, 


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.