Habari za Punde

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AHITIMISHA SHEREHE ZA MAADHIMISHO YA WIKI YA MAJI KITAIFA WILAYANI MPWAMPWA MKOA WA DODOMA LEO

 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Rehema Nchimbi, wakati wa sherehe za maadhimisho ya Wiki ya maji zilizofanyika Kitaifa Wilaya ya Mpwapwa Mkoani Dodoma leo, Machi 19, 2014.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiweka jiwe la msingi kuashiria kuzindua rasmi Kisima cha Bomba la maji sikiliza wakati wa sherehe za maadhimisho ya Wiki ya maji zilizofanyika Kitaifa Wilaya ya Mpwapwa Mkoani Dodoma leo, Machi 19, 2014. Kushoto kwa Makamu ni Waziri wa Maji , Profesa Jumanne Maghembe,(kushoto) ni Mama Asha Bilal
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Meneja wa Mradi wa Maji wa Wilaya ya Mpwapwa, Shadrack Matemba (wa pili kulia) wakati alipotembelea moja ya chanzo cha maji wakati wa sherehe za maadhimisho ya Wiki ya maji zilizofanyika Kitaifa Wilaya ya Mpwapwa Mkoani Dodoma leo, Machi 19, 2014. Kulia kwa Makamu ni Mama Asha Bilal na Waziri wa Maji , Profesa Jumanne Maghembe
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifurahia ngoma ya asili ya kabila la Wagogo wakati alipokuwa akiwasili katika sherehe za maadhimisho ya Wiki ya Maji zilizofanyika Kitaifa Wilaya ya Mpwapwa Mkoani Dodoma leo
  Baadhi ya wananchi wa Wilayani Mpwapwa wakimsikiliza Makamu wa Rais wakati akiwahutubia.(Picha na OMR)


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.