Habari za Punde

Awamu ya Kwanza ya Mradi wa Ujenzi wa Maegesho ya Ndege na Njia ya kuondokea imekamilika




5 comments:

  1. Astafirulah Muandishi au Mpiga picha ... Kwanza naacha Mdomo wazi ikiwa Mabehewa hayo matupu yasiokua na madirisha wala Vioo ndio Unasema Sehemu ya Kuegeshea Ndege imekamilika ndio kukamilika huko. Hebu jaribuni ku-google na Muangalie Viwanja vya Ndege vya Nchi nyengine kama hamujawahi kutoka Njer ya Tanzania . Hivo munaweza kujua kwamba Uwanja huo hata haujawaza kumaliza.. Na hela imeshaliwa mara 2 , isitoshe Balozi Sefu Ali Iddi kama Msimamaizi wa mambo ya Serikali Amewakabidhi Wachina Wengine kula hela ya Walipa kodi.. Kwani ni Wazanzibari ndio watakao lipa madeni hayo na sio viongozi..

    ReplyDelete
  2. Mdau hapo juu labda nikueleweshe kwamba kilichokamilika ni njia na maegesho ya ndege tu sio jengo. Hii ni miradi miwili tofauti. Mradi wa njia na maegesho ulikuwa chini ya Kampuni kutoka Ufaransa na hauhusiani na mradi wa jengo la uwanja ambalo linajengwa na kampuni kutoka China na haujakamilika bado kama inavyoonekana kwenye picha.

    ReplyDelete
  3. @ Zanzi News
    Kwanza nakupa pongezi zakuweza kusoma maoni yetu na kutupa Majibu. Sio Waandishi wengi wenye tabia yakuangalia comment za wasomaji. Nimefarijika sana na uatendaji huu unaouonyesha ndugu yangu Othman...
    Pili Nyinyi kama Waandishi wa habari au watu wa Blog. Mungechukua hatua yakutoa makosa Serikali pale inavyofanya makosa ambayo mara nyingi hua ni makosa ya Kurudia.

    Tunajua muna ugumu huo kwasababu yakutishwa tishwa kufungiwa mitandao yenu pale munapozungumza ukweli. Lakini nduguyangu Otmani Msema kweli ni mpenzi wa Mungu. Na mwisdho hao jamaa wakiona munasema ukweli na critised za SMZ ndipo watakapofanya vizuri..

    Uwanja huu itakuaje uwegeshaji Wapewe campony nyengine na Uwanja company nyengine? Kule Denmark, Norwa, Uk na hata Netherland wanaPEWA NAFASI ZA kUJENGA vIWANJA HUWA NI COMPANY NZURI NA ZENYE RECORDI nZURI ZAKUTUJENGEA HAPO nYUMBANI.. nASHANGAA KUIONA sERIKALI IMECHUKUA mKANDARASI NA KUUKABIDHI KWA KAMPUNI ZISIZO NA SIFA NA LEO UWANJA UMESHAFIKA MIAKA 3 HAUJAMALIZA.

    nA mEDIA ZOTE KAMA NYINYI MUNAREPOTI HABARI ZA KASUKU TU, HAZINA MAELEZO KAMILI NA KUULIZA MASUALI NDANI YAKE AU KUPATA INTERVIEW NA rAISI AU WAZIRI MUHUSIKA JUU KA DHIA HII. iNGEKUA MUNAFANYA HIVO BASI NAAMINI zANZIBAR CORRUPTION INGEPUNGUA SANA.

    ReplyDelete
  4. @ Anonymous 1

    Hata mimi naungana na Maoni yako kwamba Waandishi wa habari wa Tanzania hasa Zanzibar hawawezi kuikosoa Serikali au kiongozi wa SMZ. Hii nikutokana na Woga walionao yaani wasije kufungiwa au wasije kufukuzwa kazi hata sijui.

    Weekeness hii ndio imeifanya SMZ na Viongozi wengi wa Tanzania Bara na Visiwani wawe Wajeuri kila mara na waweze kuwanunua Waaandishi wa habari kwakuwakingia vifua. Kwakuchangia katika picha hii sioni mantiki yoyote ya Muandishi kusema kwamba namnukuu nduguyetu .".. Awamu ya Kwanza ya Mradi wa Ujenzi wa Maegesho ya Ndege na Njia ya kuondokea imekamilika" mwisho wa kumnukuu.

    Kwasababu kwa mtu mwenye kupendakazi yake hawezi kusema Awamu hiyo ya Ujenzi imemalizika wakati sehemu iliomalizika imefunikwa na hio iliokua haijamalizika.. Yaani hapa nimekusudia hata kama Sehemu ya Kurukia ndege imemalizika lakini visibility yakuonekana uzuri wake imefujwa na yale Mabehewa matupu ambayo muandishi amesema ni Maegesho ya Ndege..

    Hapo nilitegemea ndugu Muandishi aseme hivo kama angalau ingekua yale mabehewa yameshatiwa Vioo na Watu wameanza kupandia na kushukia pale kwenye mabehewa... Lakini naona Muandishji huyu hata kama ni kipenzi chetu uandishi wake ni wampisha vyangu tu kama walivowaandishi wengine wa Tanganyika na hapo Zanzibar... Yale kwa yale maju yafuti na nyayo..

    Muandishi na mimi nimesoma habari na niko Kwenye Redio za Norway nategemea hapo ungesema .. Uwanja ambao umepewa wakandarasi 2 tofauti umefikia katika hali hii ambayo njia ya kurukia ndege inaonekana kuwa bora japokua haina taa za uwanjani. Lakini yale Mabehewa yakuegeshea ndege bado imekua ni mitihani mpaka sasa hiyo company .....(hapo unaitaja jina lake) haijamaliza ujenzi wa mabehewa hayo ambayo SMZ- SUK inayoongozwa na CCm imekua ikiwaahidi Wazanzibari kwamba uwanja utamalizika mwaka huu. Hapo ungeandika hatua gani uliochukua kama Muandishi tunaekuamini kupata habari zaidi za uwanja huo?

    Mfano taa za uwanjani za chini , taa za juu ambazo hizo zinaweza kutumia Solar Power n.k

    Hongera Anonymous 1 kwa hoja zako.

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.