Habari za Punde

Balozi Seif Akabidhi Fedha za Mkopo kutoka Mfuko wa Uwezeshaji Wananchi ulioanzishwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, akizungumza na Wanavikundi vya Ushirika wakati wa hafla ya kuwakabidhi Fedha za Mkopo kwa Ajili ya Vikundi hivyo, hafla hiyo imefanyika Wizara ya Uwezeshaji Wan anchi Kiuchumi Mwanakwerekwe Zanzibar. 
Mwakilishi wa Kikundi cha wajasiri amali wa usafirishaji abiria kwa njia ya Bahari cha Rehema za Mungu cha Kisiwa cha Tumbatu  Wilaya ya Kaskazini “ A “ akipokea hundi ya shilingi Milioni 2,400,000/- kutoka kwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi zilizotolewa na Mfuko wa Uwezeshaji wa Wananchi Kiuchumi Zanzibar.
Mwakilishi wa Kikundi cha Wajasiriamali cha Uvivu Si Mtaji cha Tunguu Wilaya ya Kati akipokea hundi ya shilingi Milioni 2,000,000/- kutoka kwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi zilizotolewa na Mfuko wa Uwezeshaji wa Wananchi Kiuchumi Zanzibar.
Baadhi ya Viongozi wa Vikundi 12 vya wajasiri amali wa Kisiwa cha Unguja wakifuatilia hafla ya utowaji Mikopo kwa vikundi vyao kutoka mfuko wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi iliyofanyika Makao Makuu ya Wizara ya Uwezeshaji, Ustawi wa Jamii, Vijana Wanawake na Watoto Mwanakwerekwe.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif kati kati waliokaa vitini akiwa katika Picha ya pamoja na baadhi ya Viongozi wa Vikundi  12 vya ujasiri amali wa kisiwa cha Unguja waliopata Hundi ya mkopo wa kuendeleza Miradi yao.
Kulia ya Balozi Seif ni Waziri wa Uwezeshaji, Ustawi wa Jamii, Vijana, Wanawake na Watoto Mh. Zainab Omar Mohammed na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mh. Abdulla Mwinyi.Kushoto yake Balozi ni Mwenyekiti wa Kamati ya kuchangisha Fedha za Mfuko wa uwezeshaji wananchi kiuchumi Mh. Haroun Ali Suleiman na Mwenyekiti wa Kamati ya Baraza la Wawakilishi inayosimamia Wanawake na Watoto Mh. Mgeni Hassan Juma.(Picha na Hassan Issa  OMPR)


1 comment:

  1. rushwa za wazi kutaka kura mwaka ujao , hampati kitu hata mtupe mamilioni , tunaangalia uadilifu na ukweli wa viongozi mara hii , msipoteze bure pesa zenu

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.