Habari za Punde

UTEUZI WA NAIBU MABALOZI


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, amefanya uteuzi wa Naibu Mabalozi wawili.
Walioteuliwa ni Bw. Robert Kahendaguza (pichani juu) anayekuwa Naibu Balozi, Ubalozi wa Kudumu kwenye Ofisi za Umoja wa Mataifa, Geneva, Uswisi, na Bw. Msafiri Marwa (pichani chini) anayekuwa Naibu Balozi wa Tanzania London, Uingereza.

Kabla ya uteuzi huu, Bw. Kahendaguza alikuwa Kaimu Mkurugenzi, Idara ya Ushirikiano wa Kikanda, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Bw. Marwa alikuwa Ofisa Mambo ya Nje Mkuu.

Uteuzi huu unaanza tarehe 25 Mei, 2014.

IMETOLEWA NA:
KATIBU MKUU
WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA,
DAR ES SALAAM
JUNI 11, 2014

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.