Habari za Punde

Fadhila za Siku ya Arafah na Eid yake

بسم الله الرحمن الرحيم

Hatuna budi kumshukuru Allah(S.W) kwa kufika katika masiku 10 Bora katika mwezi wa Dhul Hijjah ambayo yeye mwenyewe ameyaapia masiku 10 hayo katika Suratul Fajr(1-2).Na Kumtakia rehema na amani Mtume wetu Sayyidna Muhammad(S.A.W) na Maswahaba zake na kila aliyefuata njia ya uongofu.
Siku ya Arafah Ni Siku Ya Tisa Dhul-Hijjah
a). Madhambi ya miaka miwili hufutiwa atakayefunga:
Siku hii tukufu ni siku iliyokamilika dini yetu. Thawabu za kufunga siku hii ni kufutiwa madhambi ya miaka miwili.

عن ابي قتادة رضي الله عنه أن النبي صلي الله عليه وسلم قال: (( صيام يوم عرفة أحتسب على الله ان يكفر السنة التي قبله والسنة التي بعده )) أخرجه مسلم

Imetoka kwa Abu Qataadah (Radhiya Allahu ‘anhu) ambaye amesema Mtume(S.A.W) kasema kuhusu Swawm ya Arafah kuwa ((inafuta madhambi ya mwaka uliopita na wa baada yake)) {Muslim}
b) Siku ambayo huachiliwa watu wengi huru na moto.

عن عائشة رضي الله عنها أن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال : ((ما من يوم ان يعتق الله فيه عبدا من النار من يوم عرفة)) رواه مسلم

Imetoka kwa Mama wa Waumini,Aaishaah(Radhiya Allahu anha) kwamba Mtume(S.A.W) amesema: ((Hakuna siku Allah(S.W) Anayowaacha huru waja na moto kama siku ya Arafah)) {Muslim}

c). Du’aa  bora kabisa ni Du’aa katika siku ya Arafah
Vile vile inapasa kumtaja sana Allah(S.W) siku hii kama alivyosema Mtume(S.A.W) kuwa:

((خير الدعاء دعاء يوم عرفه ˛ وخير ما قلت أنا و النبيون من قبلي: لا إله إلا الله وحده لا شريك له ˛ له الملك وله الحمد وهو على كل شيئ قدير)) روى الترمذى((Du’aa bora kabisa ni du’aa katika siku ya Arafah, na yaliyo bora kabisa niliyosema mimi na Mitume kabla yangu ni:’’Laa ILaaha IIIa Allah Wah-dahu Laa Shariyka Lahu,Lahul-Mulku Wa-Lahul-hamdu Wa Huwa Alaa Kulli Shay-in Qadiyr)){Tirmidhiy}
TANBIH 1: Siku ya Arafah ni siku ambayo Mahujaji wanasimama katika viwanja vya Arafaat huko Makkah nasi hatuna budi kuungana nao kwa kufunga siku hiyo kama alivyosisitiza Mtume(S.A.W) na kutuonesha fadhila zake.
Siku ya Kuchinja Ni Siku Kuu ya Iyd

Kasema Mtume (S.A.W) ثم يوم الق ))                                                                                       ( إن 
أعظم الأيام عندالله يوم النحر ˛
(( Siku iliyo tukufu kabisa kwa Allah ni siku ya kuchinja, kisha siku ya kutulia)) yaani siku ya kukaa Mina {Abu Daud}
Siku za Tashriyq
Ni siku ya 11,12 na 13 ya Dhul Hijjah yaani baada ya siku ya Iyd.Na siku hizi tatu zimeitwa siku za Tashriyq kwasababu watu walikuwa wakikatakata nyama na kuzianika juani.Siku za kuanika(nyama) juani.Na pia siku hizi hujulikana kwa ‘siku za Minaa’.
a). Katika siku hizi inampasa Muislamu popote alipo azidishe kumkumbuka Allah(S.W) kwa kuleta takbiratul Iyd kama Anavyosema:
(( واذكروا الله في أيام معدودات ))
(( Na Mtajeni Allah(S.W) katika zile siku zinazohisabiwa)) {Al Baqarah 203}


b). Haifai kufunga katika siku hizi.
Haifai kufunga katika siku hizi hata kama mtu alikuwa na mazowea ya kufunga Sunnah za Jumatatu na Alkhamiys au Ayyaamul Baydh kutokana na makatazo kama haya:
عن ابي هريرة أن رسول الله صلى الله عليه وسلم بعث عبدالله بن حذافة يطوف فى منى: (( لا تصوموا هذه الأيام˛ فإنها أيام أكل وشرب ˛ وذكر الله عزوجل )).
Imetoka kwa Abu Hurayrah kwamba Mtume(S.A.W) alimtuma ‘Abdullah bin Hudhaafah azunguke Mina na atangaze “Msifunge siku hizi,kwani hizi ni siku za kula na kunywa na kumkumbuka Allah Mwenye Nguvu Mtukufu “ {At-Twabariy:4:211}
Tunamuomba Allah (Subnaanahu wa Ta’aala) Atupe umri na Afya na uwezo wa kuweza kufanya mengi ya kumridhisha katika siku hizi tukufu na siku zote nyingine ili tujipatie thawabu nyingi na Atujaalie tuwe katika wale wanaosikiliza kauli na daima wakafuata zile zilizo njema.Aamiyn
TANBIH 2: a) In Shaa Allah Mahujaji wote huko Makkah watasimama kwenye viwanja vya Arafah siku ya Ijumaa sawa na tarehe 03-10-2014M – 09Dhul-Hijjah 1435H na sisi kwa Yule Mwenyezi Mungu akimjaalia na siha nzuri na wasaa mzuri basi na tuwekeni nia ya kufunga siku hiyo kwani utukufu wake ni mkubwa kama tulivyoelezewa hapo juu.Allah(S.W) atuwezeshe In Shaa Allah.
b) Kwa Kawaida ilivyo baada ya kisimamo cha Arafah siku inayofuata ina kuwa ni siku ya sikukuu kama ilivyoelezwa katika vitabu vya hadithi na kufunga siku hiyo itakuwa ni haramu kama ilivyoelezwa hapo juu.Kwahivyo siku ya sikukuu itakuwa ni siku ya Jumaamosi sawa na tarehe 04-10-2014M – 10Dhul Hijjah 1435H.
ZINDUKA: Kwa siku ya sikukuu hii inaitwa “IDDYL HAJJ’’(IDDYL ADH-HA/IDDYL NAHRI) kwasababu iddi hii imeambatana na tukio zima la Ibadah ya Hijjah ambayo inatekelezwa huko Makkah,Saudia Arabia.


"اللهم ارنا الحق حقا وارزقنا اتباعه وارنا الباطل باطلا وارزقنا اجتنابه "
“YAA ALLAH TUONESHE HAKI NA UTURUZUKU KUIFATA NA UTUONESHE BATILI NA UTURUZUKU KUIACHA”.
“YAA ALLAH WAKUBALIE MAHUJAJI WETU WOTE IBADA YAO YA HIJJAH IWE MAQBULI PAMOJA NA AMALI ZOTE WAKATAZOFANYA WAKIWA KATIKA SEHEMU TUKUFU YA MAKKA NA MADINAH” IN SHAA ALLAH AMEENY

Sambaza ujumbe huu na wewe Allah atakulipa ujira mzima wa kutoa elimu.


Jamal Murtadha Hassan El Turky
Mwalimu wa Madrasatul Minshamy Islamiyah
Baghani-Zanzibar
0773861777

2 comments:

  1. Shukran.
    JAZAKALLAH KHEIR. M/MUNGU akubariki kwa kutupa darsa.

    ReplyDelete
  2. Naomba tafsiri ya neni
    أحتسب على الله katika hadithi ya mtume Rehma za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na Amani. Ahsante

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.