Mabingwa watetezi wa
kombe la Mapinduzi, KCC ya Uganda imeyaaga mashindano hayo baada ya kutolewa kwa
penalti 5 kwa 4 na makamo bingwa wa ligi ya zanzibar timu ya Polisi Zanzibar.
Mchezo huo wa robo
fainali ya pili uliochezwa majira ya saa 9 alasiri na kuhudhuriwa na kamishna
wa Polisi Zanzibar, Hamdani Makame, vijana wa polisi ambao walionekana kucheza
mchezo huo kwa kujilinda zaidi katika muda mwingi wa mchezo huo na kuwafanya
KCC kuutawala mchezo huo.
Mbali na kamishna huyo
pia mchezo huo ulishuhudiwa na Rais wa shirikisho la soka la Tanzania
aliyeambatana na kocha mkuu wa Taifa Stars, Polisi ililazimika kuwa makini muda
wote kutokana na washambuliaji Willium Wadri na Saka Mpima kulisakama lango la
Polisi na kokosa nafasi nyingi za kufunga.
Hali hiyo iliendelea
hadi kukamilika kwa mchezo huo na ndipo mikwaju ya penalti ikachukua nafasi
yake ambapo timu ya Polisi walioanza kupiga penalti hizo na kupata 3 kati ya 5
sawa na KCC ndipo zilipoongezwa penalti moja moja na Polisi kukwamisha wavuni
2 na KCC 1.
Waliofunga kwa upande
wa mabingwa hao walioutwaa mwaka jana baada ya kuifunga simba 2 – 0 ni Tom
Masiko, Ronnie Kiseka, Mpiima Saka na Kasule Owen wakati Ntege Ivan na Wadri
Willium penalti zao ziliishia mikononi mwa golikipa wa polisi Nassir Suleiman
kabla ya Namwanya Simon penalti yake kugonga nguzo na kutoka nje.
Kwa upande wa Polisi ni
waliofunga ni Daniel Justine, Mohamed Seif, Abdalla Mwalim, Mohamed Salim na Ali
Khalid huku penalti za Juma Ali na Suleimani Makungu zikiota mbawa na kutoka
nje.
Kwa matokeo hayo Polisi
itacheza na Simba katika mchezo wa nusu fainali utakaochezwa siku ya jumamosi
katika uwanja wa Amaan.
0 Comments