Habari za Punde

Katiba pendekezwa yaanza kugawiwa Pemba

 
BAADHI ya maboksi yenye katiba iliyopendekezwa ambayo Wilaya ya Chake Chake imepatiwa katiba 14925, ambazo zinataka kugaiwa kwa wananchi waliomo ndani ya wilaya hiyo.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)

 
MKUU wa Wilaya Ya Chake Chake Pemba, Mhe:Hanuna Ibrahim Massoud, akizungumza na wananchi na Wakuu wa taasisi mbali mbali za Serikali nje ya ofisi yake, kabla ya kuwakabidhi katiba iliyopendekezwa kwa wanancha na wakuu hao.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)

 

MKUU wa Wilaya ya Chake Chake Pemba Mhe:Hanuna Ibrahim Massoud, akimkabidhi katiba 100, Afisa Mdhamini Wizara ya Miundombinu na Mwasiliano Pemba Mhe:Hamad Ahmed Baucha, hafla hiyo iliyofanyika mjini Chake Chake.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)


 
MKUU wa Wilaya ya Chake Chake Pemba, Mhe:Hanuna Ibrahim Massoud akimkabidhi katiba 50, mkuu wa kambi ya JKU Pemba Kepten Asaa Kombo.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)

 
MKUU wa Wilaya ya Chake Chake Pemba, Mhe:Hanuna Ibrahim Massoud akimkabidhi katiba 50 mwakilishi kutoka KVZ ambaye jina lake halikupatikana, halfa ya makabidhiano hayo yaliyofanyika Mjini Chake Chake.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)

 
MKUU wa Wilya ya Chake Chake Pemba Mhe:Hanuna Ibrahim Massoud, akimkabidhi katiba 100, Daktari dhamana wa Hospitali ya Chake Chake Dk Yussuf Hamad Iddi, hafla iliyofanyika mjini Chake Chake.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)

 
MKUU w Wilaya ya Chake Chake Pemba, Mhe:Hanuna Ibrahim Massoud akimkabidhi katiba 100 mwakilishi wa NGOs Pemba, Bikombo Hamad Rajaba hafla ya makabidhiano hayo imefanyika mjini Chake Chake.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.

 
MAAFISA mbali mbali wa vikosi vya ulinzi na usalama wilaya ya Chake Chake wakiwa na katiba zao, baada ya kukabidhiwa na Mkuu wa Wilaya hiyo, Mhe:Hanuna Ibrahi Massoud, hafla ya makabidhiano ya katiba hizo imefanyika mjini Chake Chake.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)


VIONGIZI mbali mbali wa Taasisi za serikali Kisiwani Pemba, wakichukuwa katiba zao mara baada ya kukabidhiwa na Mkuu wa Wilaya ya Chake Chake Mhe:Hanuna Ibrahim Massoud.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)

2 comments:

  1. Katiba iliyo pendekezwa na nani tena wapi? mbona wana pewa wana chama wa ccm watupu waliopo vikosini na kwenye wizara za serekali sisi wananchi wa kawaida ambao ndio wengi hatuna kazi au ajira za serekali tuna jituma wenyewe kwa uvuvi,kilimo, kuchuma karafuu, mifugo na biashara ndogo ndogo hatukupata taarifa hizi au ndio hatumo tuna baguliwa kwa kudhaniwa sote wapinzani wa sirikali yetu inayo ongozwa na baraza la mapinduzi.

    sisi ni raia kama hao majeshi lakini hatupati chochote japo kuwa hatuna wakati na vyama wengine tuna hangaika kutafuta riziki siku zote lakini bado tunashakiwa na kutiwa kwenye matatizo yasiyo tuhusu kweli kuna wananchi wengi wapinzani na wengine wanachama wa ccm japo kuwa sio wengi sana kwa sasa kila kukicha wanapungua sijui kumezidi nini lakini sie wengine watuonea tu hatu husiki na ugomvi wao.

    naomba wahusika watufikire na sie tusio kuwa na vyama kwa sababu mambo ya siasa sio lazima kujihusisha ni hiarie mtu sasa kwa nini wanatufanyia hivi, sisi tunataka kujua kilichomo ili tujue tupige kura ya ndio au hapana basi.

    Asante sana.

    mwananchi,Tibirinzi.

    ReplyDelete
  2. SAY NO FOR KATIBA YA CCM SIO YA WANANCHI WA TANZANIA....VOTE NO
    SAY NO FOR KATIBA YA CCM SIO YA WANANCHI WA TANZANIA....VOTE NO
    SAY NO FOR KATIBA YA CCM SIO YA WANANCHI WA TANZANIA....VOTE NO

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.