Na Mwajuma Juma
KLABU ya soka ya Black Sailor imesema kuwa haijafunga mazoezi na wachezaji wake wamefuata wito wa kuja mazoezi kila kukicha licha ya kuchelewa kuanza kwa ligi.
Timu hiyo ambayo inashiriki ligi daraja la kwanza Taifa imekuwa ikifanyia mazoezi yake katika viwanja vya Amaan kwa Wazee ambapo hivi karibuni ilisafiri na kwenda Dar Es Salaam kuzidi kujiimarisha zaidi.
Alisema kuwa kiujumla timu yao inaendelea vizuri na mazoezi na wachjezaji wapo vizuri mpaka hapo ligi itakapoanza.
“Wachezaji wetu wameitikia vizuri wito wa mazoezi na uzuri wenyewe sisi hatujafunga mazoezi na tumeendelea moja kwa moja mpaka wakati wa ligi sisi tuko vizuri tena sana na tunamshukuru Mungu”, alisema.
Hata hivyo alisema kuwa nidhamu iliyotawala katika timu yao kuanzia mashabiki mpaka wachezaji na viongozi ndio silaha kubwa ya mafanikio ya kuweza kuendelea na mazoezi ikiwa na idadi kubwa ya wachezaji.
Aidha alisema kuwa wanajipanga kuhakikisha kuwa timu yao katika mzunguuko huo wa pili utakapoanza wanaendeleza wimbi lao la ushindi ili kuweza kupanda daraja.
Timu ya Black Sailor ipo katika Kundi A na imemaliza mzunguuko wa kwanza wa ligi ikiwa nafasi ya pili kwa kuwa na pointi 16 ambapo anaemtangulia timu ya Jang’ombe Boys inaongoza kwa kuwa na pointi 17
No comments:
Post a Comment