Habari za Punde

Mkutano wa Hadhara wa CCM Jimbo la Kiembesamaki

 
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiwahutubia Wananchi wa CCM Jimbo la Kiembesamaki wakati wa mkutano wa hadhara wa jimbo hilo uliofanyika katika viwanja vya bustanini kiembesamaki Zanzibar.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Balozi Seif Ali Iddi, akizungumza na Wananchi wa Jimbo la Kiembesamaki katika viwanja vya bustanini na kuwataka kuipigia kura ya ndio kura ya maoni ya Katiba Mpya. 
Wananchi wa Jimbo la Kiembesamaki wakimsikiliza Mjumbe wa Kamati Kuu Balozi Seif Ali Iddi akiwahutubia katika viwanja vya bustanini kiembesamaki Zanzibar.

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Magharibi Ndg Yussuf Mohammed akizungumza katika mkutano huo uliofanyika katika viwanja vya kiembesamaki. 
Mwakilishi wa Wazee wa Kiembesamaki Ndg Ali Hassan akizungumza wakati wa mkutano huo kwa niaba ya wazee wa jimbo hilo, amewataka waheshimia kusimamia sheria ipasavyo. na kuwataka wananchi wa kimbo la kiembesamaki kuipigia kura ya ndio Katiba iliopendekezwa,   
Mwanachama wa Chama cha Mapinduzi Ndg Tambwe Hiza akiwahutubia wananchi wa jimbo la kiembesamaki wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja bustani kiembesamaki Zanzibar na kuwataka wananchi wa kiembesamaki kuacha kudanganywa na Viongozi wa vyama vya upimzani havina sera.

Mhe Tambwe akisisitiza jambo wakati akihutubia mkutano huo wa hadhara katika viwanja vya bustanini kiembesamaki 
            Waheshimiwa wa meza kuu wakimsikiliza Tambwe Hiza akihutubia katika mkutano huo.

Mhe Tambwev Hiza akisalimiana na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, baada ya kushuka jukwaani kuhutubia katika mkutano huo wa hadhara katika viwanja vya bustanini kiembesamaki.
Mwakilishi wa Jimbo la Kwamtipura akisisitiza jambo wakati akihutubia katika mkutano wa hadhara wa Chama cha Mapinduzi katika viwanja vya bustanini kiembesamaki Zanzibar. 
Mwakilishi wa Jimbo la Kiembesamaki Mhe. Mahmoud Thabit Kombo, akihutubia katika mkutano huo na kuwataka Wananchi wa kiembesamaki kushiriki kwa ukamilifu wakati ukifika wa kupiga kura ya maoni ya Katiba mpya iliopendekezwa.

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Mjini Ndg Burafya Silima, akizungumza na wananchi wa jimbo la kiembesamaki wakati wa mkutano wa hadhara katika viwanja vya bustanini kiembesamaki Zanzibar.
Naibu Katibu Mkuu wa UVCCM Ndg Shaka Hamdu Shaka akizungumza wakati wa mkutano huo wa jimbo la kiembesamaki uliofanyika katika viwanja vya bustanini kiembesamaki.
                            Wananchi wakiwa katika viwanja vya mkutano wakishangilia
Wanachama wa CCM wakichukua picha kwa simu zao ili kuweka kumbukumbu ya mkutano huo wa jimbo la Kiembesamaki 





No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.