Na Mahmoud Ahmad,Arusha
SHIRIKA la ndege la Fastjet nchini Tanzania limesema litaendelea kutoa huduma za usafirishaji kwa bei nafuu pamoja na kusaidia makundi maalum katika jamii ikiwa ni pamoja na watoto yatima na watoto wenye ulemavu wa ngozi ili waweze kupata elimu hatimaye kukabliana na mazingira wanayoishi .
Meneja wa Fastjet Afrika Mashariki Jimmy Kibati akizungumza na waandishi wa Habari Jijini Arusha janaa wakati akitoa ufafanuzi wa safari mpya za Entebe Kilimanjaro na Mwanza kuwa hatua hiyo ni kuendelea kuboresha huduma ya usafiri wa anga ikiwa ni pamoja na kuzidi kupunguza bei kwa wateja wao ili wapate fursa ya kutumia usafiri huo.
Bw,Kibati alisema kuwa tayari pamoja kuwa wanatoa huduma za usafiri ,wameweza kuwawezesha madaktari bingwa sita wa meno kwenda Mkoa wa Shinyanga kwenda kuhudumia watoto wanaotoka katika mazingira magumu,wenye matatizo ya meno na kuwa suala la kuhudumia jamii linapewa kipaumbele na Shirika hilo .
Akitoa ufafanuzi wa huduma za Shirika hilo alisema kuwa wameanza kutoa safari tatu katika siku za Jumanne ,Alhamisi na Jumamosi na kuwa safari hizo ni za Kilimanjaro na Entebe na zitaanza tarehe 31 March 2015
Alisema kuwa Safari ya Entebe na Kilimanjaro itafungua fursa kwa wafanyabiashara na kuwa gharama yake ni Tshs 95,000
Pamoja na mambo mengine alisema kuwa Safari mpya kati ya Kilimanjaro na Mwanza inatarajia kuanza tarehe 30 Machi 2015 kwa nauli Tshs 35,000 na kuwa safari hiyo itakuwa mara nne kwa wiki ikiwa ni siku ya Jumatatu ,Jumatano na Jumapili
Kimsingi alisema kuwa wateja wanaweza kupanga safari zao kupitia tovuti ya Fastjet inayojulikana kwa www.fastjet.com
Alitaka wateja wa Shirika hilo kufanya utaratibu wa usafiri mapema ili waweze kulipa nauli nafuu
No comments:
Post a Comment