Habari za Punde

Aangukiwa na kifusi na kufariki, Chakechake Pemba

 WANANCHI mbali mbali wa mji wa Chake Chake wakiangalia fusi lililomfunika marehemu Seif Kibishi (33) mkazi wa Tibirinzi, baada ya kufunikwa na fusi la mawe baada ya kuporomoka wakati walipokuwa wakichimba msingi wa nyumba ya Ghorofa katika soko la Katari Chake Chake.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
 FUSI la mawe lililoporomoka na kusababisha kifo cha kijana Seif Kibishi (33)mkaazi wa Tibirinzi Chake Chake, katika eneo la soko la katari.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
 ASKARI wa kikosi cha zimamoto na uwokozi Chake Chake Pemba, wakivunja mawe kwa kutumia nyundo, ili kufukuwa fusi lililomfunika kijana Seif Kibishi(33)na kupelekea kupoteza maisha, baada ya fusi hilo la mawe wa fondesheni ya jingo la ghorofa, kumwangukia wakati alipokuwa akichimba msingi yeye na wenzake wanne katika soko katari.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
 ASKARI wa Polisi Mkoa wa kusini Pemba wakiweka ulinzi katika eneo lililoporomoka fusi la mawe na kusababisha kifo cha kijana Seif Kibishi (33)mkaazi wa Tibirinzi Chake Chake, huku vikosi vya uokozi vilipokuwa vikifanya kazi ya kufukuwa fusi hilo.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
 MKUU wa Mkoa wa kusini Pemba Mhe:Mwanajuma Majid Abdalla mwenye baibui, akiangalia kazi ya ufukuaji wa mwili wa kijana Seif Kibishi (33) mkaazi wa kibirinzi Chake Chake, iliyokuwa ikifanywa na vikosi mbali mbali vya ulinzi na usalama mkoa huo huko katika soko la katari.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)

 WANANCHI mbali mbali wakishuhudia kazi ya uokoji wa mwili wa kijana Seif Kibishi (33) mkaazi wa Tibirinzi Chake Chake, aliyefunikwa na fusi.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
 VIKOSI mbali mbali vya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Kusini Pemba, wakiutoa mwili wa kijana Seif Kibishi (33) mkaazi wa Tibirinzi Chake Chake, mara baada ya kufukiwa na fusi la mawe huko katika soko la katari, wakati alipokuwa akichimba msingi wa nyumba ya ghorofa.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
 VIKOSI vya ulinzi na Usalama Mkoa wa kusini Pemba, wakiubeba mwili wa marehemu Seif Kibishi(33)mkazi wa Tibirinzi Chake Chake, mara baada ya kuufukuwa katika kifusi na kupeleka katika gari ya wagonjwa kwa kupelekwa spitali.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
 KIKOSI Cha Huduma ya kwanza Red Cross Kisiwani Pemba, wakiongozwa na Dk Suleima Ali wa kwanza kushoto wakiwa wameubeba mwili wa mrehemu Seif Kibishi (33) aliyefukiwa na kifusi na kupeleka katika chumba maalumu cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya Chake Chake kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.).
 MKUU wa Mkoa wa kusini Pemba Mhe:Mwanajuma Majid Abdalla, akizungumza na waandishi wa habari mbali mbali kisiwani Pemba, mara baada ya kukabidhiwa kwa mwili wa mrehemu Seif Kibishi aliyepoteza maisha baada ya kufunikwa na fusi.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
Mkuu wa Wilaya ya Chake Chake Mhe: Hanuna Ibrahim Masoud akiwa na katibu tawala wake Rashid Khadid wakijadiliana na ndugu na jamaa wa marehemu kijana Seif Kibishi aliyepoteza maisha baada ya kufunikwa na fusi, juu ya maandalizi ya mazishi ya marehemu huyo.(picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.