Habari za Punde

Kamanda wa Matukio Blog Yapongwezwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa Coverage Nzuri ya Uchaguzi Mkuu 2015

 Mpiga Picha Mkuu wa gazeti hili, ambaye pia ni Mmiliki wa Blogu ya Kamanda wa Matukio, Richard Mwaikenda (kushoto) akikabidhiwa na Kaimu Mkuu wa Habari Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Clarence Nanyaro cheti maalumu cha kutambua mchango wa blogu hiyo namna ilivyoshiriki katika kurusha matangazo, mijadala, habari na michezo iliyoelimisha na kuhamasisha wananchi kujitokeza katika shughuli mbalimbali za Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015. Hafla hiyo ya kukabidhi vyeti kwa vyombo vya habari vilivyofanya vizuri kazi hiyo, ilifanyika Makao Makuu ya NEC Dar es Salaam leo.

Mwaikenda, alishiriki kikamilifu katika coverage ya kampeni za miezi miwili za Mgombea Urais wa CCM, Dk. John Magufuli katika mikoa mbalimbali nchini.Kazi zake zilikuwa zinatumika kwenye gazeti la Jambo Leo  analofanyia kazi na kusambazwa pia kwenye blogu mbalimbali nchini.

Pia alikuwa miongoni mwa wapigapicha waliofanya coverage wakati wa kutangazwa kwa matokeo,mshindi wa urais na kuapishwa Rais Dk John Magufuli Novemba 5, 2015, kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. (PICHA NA MARGARET CHAMBIRI-NEC)
 Mwaikenda akifurahia kupata cheti hicho




No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.