Habari za Punde

Kituo cha Sheria Pemba Chatowa Elimu ya Katiba

 Mratibu wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ZLSC Tawi la Pemba, Fatma Khamis Hemed, akielezea historia ya kituo hicho kwa wanafunzi wa skuli za sekondari za Mkoa wa kusini Pemba, kwenye mafunzo ya utayarishaji wa katiba na sheria, kulia ni Afisa Mdhamini elimu Pemba, Salum Kitwana Sururu na kushoto ni Afisa Mipango wa ZLSC Mohamed Hassan Ali
 Mratibu wa Mafunzo ya Utayarishaji wa Katiba na Sheria, Khalfan Amour Mohamed, akitoa ufafanuzi jinsi ya mafunzo hayo, kulia Afisa Mdhamini wizara ya elimu Pemba, Salum Kitwana Sururu mafunzo hayo, yalifanyika Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ZLSC tawi la Pemba
Mdhamini Elimu Pemba, Salum Kitwana Sururu akifungua mafunzo ya siku moja kwa wanafunzi wa skuli za sekondari za Mkoa wa kusini Pemba, juu ya utayarishaji wa katiba na sheria, kulia ni Mratibu wa mafunzo hayo, Khalfan Amour Mohamed na kushoto ni Mratibu wa ZLSC Fatma Khamis Hemed. 
Wanafunzi wa skuli za sekondari za Mkoa wa kusini Pemba, wakisiliza uwasilishaji wa mada, katika mafunzo ya utayarishaji wa katiba na sheria, yalioandaliwa na kufanyika Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ZLSC tawi la Pemba.
Mwanafunzi wa skuli za sekondari ya Mkoa wa kusini Pemba, akielezea maana ya katiba, mbele ya mtoa mada kutoka Kituo cha Huduma za Sheria Pemba, Fatma Khamis Hemed
Watendaji wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ZLSC tawi la Pemba, Afisa mdhamini  elimu Pemba na wanafunzi wa skuli za sekondari za mkoa wa kusini Pemba,  wakiwa katika picha ya pamoja baada ya mafunzo ya utayarishaji wa katiba na sheria

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.