Habari za Punde

Rais wa Zanzibar Dk Shein Amuapisha Naibu Katibu Mkuu Uwezeshaji

STATE HOUSE ZANZIBAR
OFFICE OF THE PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE
 Zanzibar                                                             11.2.2016
---
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein leo amemuapisha  Ndugu Hassan Khatib Hassan kuwa Naibu Katibu Mkuu (Uwezeshaji), katika Wizara ya Uwezeshaji Ustawi wa Jamii, Vijana, Wanawake na Watoto.

Hafla hiyo iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar ilihudhuriwa na viongozi mbali mbali wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar akiwemo Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Idd, baadhi ya Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Mhe. Said Hassan Said, Katibu Mkuu Kiongozi na Katibu wa Baraza la Mapinduzi Dk. Abdulhamid Yahaya Mzee.

Wengine ni Mkuu wa  Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe. Abdalla Mwinyi Khamis, Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabih, Naibu Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Hassan Othman Ngwali, Meya wa Manispaa ya Mji wa Zanzibar Khatib Abrahman Khatib  pamoja na Washauri wa Rais wa Zanzibar na viongozi wengine wa Serikali.

Kabla ya uteuzi huo ndugu Hassan Khatib Hassan alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Wete Pemba.

Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar

Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax: 024 2231822 
 E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.