Habari za Punde

Ujumbe Kutoka Manispaliti ya Sundsvalls Sweden Watembelea Makunduchi Zanzibar.


Waziri Kiongozi Mstaafu,Mhe Shamsi Vuai Nahodha   alikabidhiwa bendera ya Sweden na Mwenyekiti wa Kamati ya Elimu kutoka Baraza la Manispaliti ya Sundsvalls Ndg. Joao. Kiongozi wa Ujumbe wa Manispaliti ya Sundsvalls upo nchini kwa ziara ya siku 6 kwa lengo la kuimarisha uhusiano kati ya Wadi ya Makunduchi na Manispaliti hiyo
Kamati ya wadi ya Makunduchi ilikabidhiwa bendera ya Manispaliti ya Sundsvalls. Bendera hiyo alikabidhiwa mwalimu Mwita Masemo, mwenyekiti wa kamati ya wadi ya Makunduchi (hayupo kwenye picha) na Mwenyekiti wa Kamati ya elimu ya baraza (assembly) la Manispaliti ya Sundsvalls ndugu Joao.

Wajumbe wa Manispaliti ya Sundsvalls, Sweden ambao hawapo kwenye picha walipata nafasi kuelezewa sheria mpya ya serikali za mitaa.Maelezo hayo yalitolewa na afisa wa polisi ndugu Said Mohamed Said aliyesimama. Mkutano huu wa pamoja ulihudhuriwa pia na Waziri Kiongozi Mstaafu, ndugu Shamsi Vuai Nahodha ambaye alitoa mada ya Historia ya Zanzibar, hali ya uchumi na kisiasa pamoja na utawala wa Makunduchi kwa jumla.
Ujumbe wa Manispaliti ya Sundsvalls walitembelea msitu wa Jozani ili kujionea wenyewe vivutio vyetu vya kitalii. Kutoka kushoto ni ndugu Mohamed Muombwa akiwa na mtembezaji wa wageni bi Zena. kwa upande wa ujumbe wa Sundsvalls kutoka kushoto ni Christin, Ina, Joao na Hans.
Ujumbe wa Manispaliti ya Sundsvall, Sweden watembelea vikoba vya Makunduchi. Wajumbe hao wanaonekana na wanavikoba wa Shehia ya Nganani. Waliokaa kutoka kushoto ni Joao, Ina na waliosimama ni Hans na bi Christin. Kwa mujibu wa mratibu wa kamati ya Wadi ya Makunduchi ndugu Mohamed Muombwa  Manispaliti ya Sundsvalls na Wadi ya Makunduchi zimeanzisha mashirikiano katika sekta ya elimu hasa kuipa uwezo Wadi ya Makunduchi kusimamia vyema elimu ili skuli za Makunduchi zifanye vizuri zaidi kielimu. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.