Mratibu wa Jukwaa la Bioteknolojia Tanzania (OFAB), Philbert Nyinondi (kulia), akizungumza na wakulima na Washiriki wa Mafunzo ya kutumia simu za mkononi kupashana habari za kilimo yaliyofanyika Kijiji cha Kisamwene wilayani Butiama mkoani Mara leo mchana.
Mratibu wa Jukwaa la Bioteknolojia Tanzania (OFAB), Philbert Nyinondi (kulia), akiwaonesha wakulima wa Wilaya ya Butiama mkoani Mara zao la mhogo uliotokana na mbegu aina ya ukombozi iliyofanyiwa utafiti nchini. Nyinondi alikuwa akiwaonesha wakulima jinsi unavyoweza kupiga picha zao hilo na kulitafutia soko wakati akitoa mafunzo ya kutumia simu jinsi kupashana habari za kilimo katika mafunzo yaliyofanyika juzi wilayani humo.
Mratibu wa Jukwaa la Bioteknolojia za Kilimo Afrika (OFAB), Daniel Otunge akiwa katika shamba la mkulima wa mfano lililopo kijijini hapo.
Mratibu wa Jukwaa la Bioteknolojia za Kilimo Afrika (OFAB), Daniel Otunge akimpiga picha mmoja wa wakulima katika mafunzo hayo.
Wakulima washiriki wa mafunzo hayo wakiwa ukumbini.
Wakulima wakiwa katika shamba la mihogo.
Mkulima akichimba muhogo wa mafunzo kutoka shamba hilo. Muhogo huo ni wa miezi nane tu.
Shamba la muhogo lililotokana na mbegu bora ya mkombozi.
Wakulima wakiwa katika mafunzo hayo. |
Wakulima wakiwa katika mafunzo ya kupiga picha. |
Hapa wakulima hao wakibadilishana mawazo baada ya kupiga picha za mafunzo.
Na Dotto Mwaibale
JUKWAA la Bioteknolojia (OFAB) limetoa mafunzo ya kutumia simu katika kupashana habari kwa wakulima wilayani Butiama mkoani Mara ili kuwarahisishia kazi zao za kilimo.
Akizungumza katika mafunzo hayo Mratibu wa Jukwaa la Bioteknolojia Tanzania (OFAB), Philbert Nyinondi alisema mafunzo hayo ya siku moja yalifanyika katika Kijiji cha Kisamwene wilayani humo ili kuwasaidia wakulima kupashana habari za kilimo na changamoto zao.
"OFAB imeleta mafunzo haya kwa wakulima ambao ni wadau wetu ili waweze kupashana habari za kilimo, changamoto zinazo wakabili na kutafuta masoko ya mazao yao kwa njia ya simu badala ya kutumia simu hizo kupigiana kwa mambo ya kawaida" alisema Nyinondi.
Alisema kupitia mafunzo hayo wakulima hao wataweza kushirikiana na mitandao mingine ya kijamii ili kutatua changamoto zao za kilimo zikiwemo za wadudu waharibifu wa mazao, ukame na nyinginezo.
Alisema washiriki wa mafunzo hayo walikuwa ni 28 kutoka Kata tano zilizopo wilayani Butiama mkoani humo na yaliwahusisha viongozi wa vijiji, kata na wenyeviti wa serikali za mitaa.
No comments:
Post a Comment