Habari za Punde

ZLSC yafika Shehia ya Matale kutoa elimu ya msaada wa sheria

 MRATIBU wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ZLSC tawi la Pemba Fatma Khamis Hemed, akifungua mkutano wa msaada wa kisheria, kwa wananchi wa shehia ya Matale Jimbo la Chonga wilaya ya Chakechake, kulia ni Naibu Mwenyekiti wa mahakama ya ardhi Chakechake, Salim Hassan Bakar na katikati ni sheha wa shehia ya Matale Mkubwa Hamad Hassan, (Picha na Haji Nassor, Pemba).

 NAIBU Mwenyekiti wa mahakama ya ardhi Chakechake Salim Hassan Bakar, akifafanua kuhusu sheria za umiliki wa ardhi, kwenye mkutano wa kutoa masaada wa kisheria, ulioandaliwa na Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ZLSC tawi la Pemba, na kufanyika shehia ya Matale Jimbo la Chonga wilaya ya Chakechake, (Picha na Haji Nassor, Pemba).

MTOTO wa shehia ya Matale Jimbo la Chonga wilaya ya Chakechake, akijifunza jinsi ya kusuka kuti bichi la Mnazi, ambapo aina hiyo ya makuti, ndio yaliokuwa maarufu visiwani Zanzibar kwa kuezekewa nyumba, (Picha na Haji Nassor, Pemba). 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.