Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akiangalia mikeka kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani iliyofumwa na wajasiriamali wanawake hapo katika Viwanja vya Kituo cha simulizi asili, Tamaduni na Lugha za Kiafrika {Eacrotanal } Mjini Zanzibar.
Balozi Seif akiangalia kiwango cha ufungaji wa bidhaa za viungo kilichofanywa na wajasiriamali wa Zanzibar kwenye maonyesho ya siku ya wanawake duniani hapo Eacrotanal.
Balozi Seif akiwa makini katika kuziangalia bidhaa za wajasiriamali za mikoba iliyotengenezwa kwa kutumia plastiki kwenye siku ya wanawake duniani.
Baadhi ya wanawake waliohudhuria maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani zilizofikia kilele chake hapo katika viwanja vya Kituo cha simulizi asili, Tamaduni na Lugha za Kiafrika { Eacrotanal } bila ya ujali mvua zilizokuwa zikinyesha mfululizo.
Kikundi cha maigizo cha Zapha + kikitoa burdani kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani zilizofanyika katika viwanja vya Kituo cha simulizi asili, Tamaduni na Lugha za Kiafrika { Eacrotanal .
Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia idadi ya watoto { UNFPA } Dr. Dr.Natalia Kamem akitoa salamu kwenye maadhimisho ya siku ya wanawake duniani hapo Eacrotanal.
Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Wanawake { UN WOMEN } Lucy Tesha akitoa salamu kwenye maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani hapo Eacrotanal.
baadhi ya wawakilishi wa vikundi vya wajasiriamali wakipokea mikopo kutoka kwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi.baadhi ya wawakilishi wa vikundi vya wajasiriamali wakipokea mikopo kutoka kwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi.
No comments:
Post a Comment